Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir/ Ardhi Iliyobarikiwa: Hizb ut Tahrir Yaandaa Maandamano Baridi Ikiyalingania Majeshi ya Waislamu Kuwanusuru Watu wa Jenin

(Imetafsiriwa)

Baada ya uvamizi wa kikatili na usio wa haki wa kambi ya Jenin na vikosi vya jeshi la Kiyahudi, ambapo vikosi hivyo vilisababisha vifo, uharibifu na ufisadi, Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina iliandaa maandamano makubwa baridi katika miji ya Hebron, Ramallah na Qalqilya, yenye kichwa “Ushindi kwa Jenin na Kutafuta Nusrah kutoka kwa Majeshi ya Waislamu.”

Kalima zilitolewa kuyahutubia majeshi ya Umma wa Kiislamu, na zilifunguliwa kwa maneno “Allahu Akbar... Ni lini ari ya wanaume itataharaki katika majeshi ya Waislamu, ili tuone majeshi yao yakiongezeka katika nyua za Msikiti wa Al-Aqsa. Allahu Akbar... Je, jeshi la Misri halina uwezo katika saa moja ya Siku wa kulitokomeza umbile la Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake?! Je, jeshi la Jordan haliwezi kuliangamiza umbile la Kiyahudi na kuliondoa katika uwepo wake?!... Je, majeshi ya Uturuki na Pakistan hayana uwezo wa kuikomboa Jerusalem na kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume Wake?!

Kalima hizo pia zilijumuisha mazungumzo juu ya ushujaa wa mujahidina katika mji wa Jenin na kambi yake, yakinukuu: “Katika Jenin, ardhi ya ushujaa, idadi ndogo ya mujahidina mashujaa walisimama kidete mbele ya ndege, magari ya kivita, na maelfu ya askari na hawakuziacha silaha zao, basi vipi kuhusu nyinyi enyi askari wa majeshi ya Waislamu?! Uimara na uthabiti wa mujahidina hawa. Wakimdhihaki adui yenu, kisha akatoka akiwa amevaa aibu, na hili linadhihirisha nguvu na dhamira ya Waumini katika kuwakabili maadui zao. Uimara wa mashujaa hawa na mapigano yao licha ya uchache wao na vifaa vyao unawafichua watawala madhalimu wanaoyafunga majeshi ya Ummah kutokana na kutekeleza wajibu wao wa Nusrah kwa Uislamu na kwa Msikiti wa Al-Aqsa.

Kalima hizo pia ziliashiria wadhifa wa aibu wa watawala kwa kuzingatia matukio haya kwa kusema: “Wale waliokasirikiwa wanaunajisi Msikiti wa Al-Aqsa asubuhi na jioni, wanavunja majumba na kumwaga damu, kisha anatujia mtu akisema tunaionya Israel dhidi ya kuvuka mistari mekundu! Ni mistari gani hiyo mekundu unayoizungumzia?! Wachunge mistari ipi mekundu baada ya kuvunja nyumba, watu kuhamishwa, umwagaji damu, na kunajisiwa kwa Msikiti wa Al-Aqsa?!

Maandamano hayo yalihitimishwa kwa kuwahutubia watu wa Ardhi Iliyobarikiwa kuwa na subira, ustahimilivu, na uchungaji mipaka katika imani, na bila kukata tamaa nayo, na kufanya kazi ya kuiathiri. Watu wa kambi ya Jenin walidhihirisha ujumbe mzito uliozifanya nyoyo zilie na kuchochea Aqidah ya Kiislamu na hisia katika kisimamo cha Hebron, ambapo walihutubia Umma wa Uislamu na majeshi yake kuja kuwanusuru watu na ndugu zenu huko Jenin. Ingekuwa vipi kama kulikuwa na fungamano la kweli nyuma yao?! Ingekuwaje lau wangekuwa na majeshi pamoja nao na mbele yao wakiwa na vifaru, ndege, makombora, na wanaume waliopata mafunzo ya kupigana, kama jeshi la Jordan, Misri, au nchi ya Hijaz...?! Mnasubiri nini na silaha zenu?! Je, hamutamani ukombozi wa Msikiti wa Al-Aqsa?! Je, hamutamani kuwa kama Salahuddin?! Hizi zilikuwa baadhi ya dondoo zilizozungumzwa.

Wazungumzaji waliukumbusha Ummah wajibu wake na kwamba ni Ummah ulio madhubuti wenye uwezo wa kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa na kwamba umbile la Kiyahudi halina nguvu za kutosha kukabiliana nao, na wakautahadharisha dhidi ya kushindwa kutekeleza wajibu wake kwa Palestina na watu wa Ardhi Iliyobarikiwa, kwa kuwa huo utakuwa ni usaliti na dhambi kubwa.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Sehemu ya Kisimamo katika mji wa Ramallah Kuwanusuru Watu wa Jenin al-Qassam

Sehemu ya Kisimamo katika mji wa Qalqilya Kuwanusuru Watu wa Jenin al-Qassam

Sehemu ya Kisimamo katika mji wa Khalil Al-Rahman (Hebron) Kuwanusuru Watu wa Jenin al-Qassam

Ripoti ya Habari kuhusu Visimamo vya Kuwanusuru Watu wa Jenin al-Qassam

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu