Alhamisi, 05 Rabi' al-awwal 1442 | 2020/10/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ripoti ya Habari 02/10/2020

Kwa kuzingatia mateso makali waliyoyapata watu wetu nchini Sudan, ambao waliondolewa katika maeneo yao na mafuriko na mvua kubwa iliyoyakumba majimbo 17 nchini Sudan, na kwa kukosekana kwa dola yenye kuwajali watu ambayo inashughulikia maswala ya watu na kukosekana kwa mtazamo halali unaoshughulikia misiba na majanga kulingana na itikadi tukufu ya Uislamu, na maelezo ya utunzaji huu na ufafanuzi kwa mtazamo halali, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan - eneo la Omdurman, kaskazini, ilifanya kalima yake ya kila wiki siku ya Ijumaa 25/9/2020 katika Soko la Sabreen katikati ya umati mkubwa wa wafuasi na wafuasi wa chama hiki, na jukwaa lilikuwa na kichwa "Maafa ya mafuriko na mvua kubwa ... Mtazamo wa Kisheria kulingana na imani Tukufu ya Uislamu".

Siku na wakati huo huo, vijana kutoka eneo la Khartoum walikuwa wakiwahutubia waumini katika Msikiti wa Abdel Moneim jijini Khartoum (3) kuhusu "uhalifu wa usawazishaji mahusiano na umbile hali la Kiyahudi."

Mnamo siku ya Jumamosi, 9/26/2020, saa 3:40 alasiri, bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ilipandishwa, ikipeperuka katika angani ya soko hilo maarufu mjini Omdurman, na sauti za mashababu wa Hizb zikiwalingania watu kukusanyika kusikiliza hotuba muhimu ya umma kuhusu uhalifu wa usawazishaji mahusiano na umbile hali la Kiyahudi lililoinyakua ardhi ya Masra [Palestina].

Halafu, mnamo Jumanne, 9/29/2020, eneo la Omdurman Kaskazini ilifanya hotuba kubwa ya umma katika Thawrat al Harat al 17, iliyopewa kichwa: "Kutoka Imarati hadi Bahrain ... Kimbunga cha Maangamivu cha Usawazishaji Mahusiano Je, Kitaisweka Khartoum?"

Siku ya Jumatano 9/30/2020, eneo la Khartoum Bahri huko Dorshaab, kaskazini mwa jiji hilo, ilifanya hotuba kwa mada hiyo hiyo: "Uhalifu wa Usawazishaji Mahusiano na umbile la Kiyahudi."

Halafu, Alhamisi tarehe 10/1/2020, eneo la Kalakila ilitoa hotuba kubwa yenye kichwa: "Je! Gari ya Moshi ya usawazishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi itapitia Khartoum?"

Mwisho wa wiki, Ijumaa tarehe 10/2/2020, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iligawanya toleo katika misikiti ya mji mkuu na miji kadhaa nchini Sudan, lililokuwa na kichwa: "Kongamano la Kiuchumi ... Kuendelea kwa Sekta ya Umaskini na Kuua Maskini." Toleo hilo lilishughulikia matokeo ya kongamano la kiuchumi lililokuja na sera.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu