Jumanne, 10 Rabi' al-awwal 1442 | 2020/10/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ripoti ya Habari 11/10/2020

Mimbari ya kila wiki ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan – eneo la Omdurman, Kaskazini – ilifanywa mnamo siku ya Ijumaa Oktoba 2, 2020, katika Soko la Sabreen chini ya anwani: "Wimbi la Usawazishaji Mahusiano … Je, watawala wa Sudan watajiunga na kundi la wanaodhihirisha khiyana kubwa?"

Katika mpangilio wa shughuli zinazoendelea na mawasiliano ya moja kwa moja na Ummah, Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Sudan - eneo la Omdurman, Kaskazini - ilifanya muhadhara katika Msikiti wa zamani wa Mapinduzi ya 14 mnamo Jumatatu Oktoba 5, 2020, baada ya swala ya Maghrib kwa anwani: "Kadhia ya Mabadiliko kwa Mwangaza wa Hijra ya Mtume (saw)."

Halafu, mnamo siku ya Jumanne, Oktoba 6, 2020, Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Sudan - eneo la Omdurman kaskazini - iliweka jukwaa la kila wiki kama kawaida katika eneo la Al-Thawra 17 chini ya kichwa "Kongamano la Kitaifa la Uchumi ... Mlima Umezaa Panya."

Ama siku ya Jumatano, Oktoba 7, 2020, hotuba mbili zilitolewa wakati mmoja; Ya kwanza ilikuwa katika eneo la Bahri huko Al-Droshaab kaskazini, ambayo ilikuwa chini ya kichwa: "Uhalifu wa kile kinachoitwa Amani". Ama ya pili, ilikuwa baada ya alasiri siku ya Jumatano, Oktoba 7, 2020, katika eneo la Omdurman,  Magharibi, eneo la Sabreen katika Soko la Libya, na ilikuja chini ya kichwa: "Matokeo ya Kongamano la kiuchumi ... Ufukarishaji wa Waja na Uuwaji wa Masikini."

"Kongamano la Kitaifa la Uchumi ni Mithili ya Mangati ya Baqi'a ambayo kwa Mwenye Kiu Hufikiria kuwa ni maji" Chini ya kichwa hiki, mimbari ya kila wiki inayofanywa na Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Sudan - eneo la Omdurman, Kaskazini - ilifanyika katika Soko la Sabreen mnamo siku ya Ijumaa Oktoba 9, mbele ya hadhira kubwa ya wafuasi wa chama hiki na wafuasi wengineo.

Vilevile, Mashababu wa Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Sudan katika mji wa Gadharif waliandaa kisimamo mnamo siku ya Jumapili, Oktoba 11, 2020, saa tatu asubuhi mbele ya eneo lililo katikati ya soko la Gadharif, chini ya kichwa "Ugavi wa Mkate ni Wajibu wa Dola." Maudhui haya ambayo yamekuwa moja ya wasiwasi wa kimsingi wa kila familia, kwani zinateseka sana katika ugavi wake; kuanzia katika Uhaba, gharama na umasikini, chini ya serikali iliyoshindwa kikamilifu kutekeleza majukumu yake hata madogo kabisa.

Mashababu walibeba mabango yaliyo angazia mada kuu.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 17 Oktoba 2020 10:02

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu