Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Ripoti ya Habari 12/29/2022

Katika muendelezo wa amali za umma zilizoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan, kuhamasisha Umma wa Kiislamu na kunoa hamu yake ya kusimamisha tena Dola ya Khilafah Rashida, kwa kuunda rai jumla yenye ufahamu juu ya hukmu za Uislamu na masuluhisho yake, hizb ilifanya amali nyingi za halaiki katika maeneo mbalimbali ya nchi, kugusia makubaliano ya mfumo wa kisiasa, na fahamu ya ugaidi na itikadi kali, Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah, mechi za Kombe la Dunia, na sherehe za kile kinachoitwa Siku ya Uhuru.

Chini ya mada: "Kombe la Dunia na Ushindi wa Kweli wa Umma wa Kiislamu," hotuba hii ya kisiasa ilitolewa kwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika mji wa Gadharef, mnamo Alhamisi, Novemba 24, 2022, ambapo Ustadh Maysara Yahya alizungumzia yanayojiri nchini Qatar katika masuala ya burudani yanayoandaliwa na serikali, jinsi fedha za Waislamu zilivyofujwa na jinsi nchi hiyo ilivyofunguliwa na Magharibi kwa maadui wa Umma wa Kiislamu kwa kisingizio cha uvumilivu na uwazi.

Katika kipengele kingine, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika vyuo vikuu waliweka kona ya mazungumzo na majadiliano, yenye kichwa: "Ugaidi na misimamo mikali ni misamiati ya kuushambulia Uislamu", katika Chuo Kikuu cha Al-Neelain, Kitivo cha Masomo ya Kiuchumi na Kijamii, mnamo Novemba 26, 2022, na Ustadh Al-Fateh Abdullah alianza hotuba yake kwa ufafanuzi kwamba 'ugaidi' ni lugha na neno, na alionyesha kuwa mashirika ya kijasusi ya Amerika na Uingereza yalikubaliana kufafanua ugaidi kama "utekelezaji vitendo vya ghasia dhidi ya maslahi ya kiraia ili kufikia malengo ya kisiasa.” Kisha akatoa mifano kadhaa inayoonyesha kuwa fahamu ya ugaidi inakusudiwa kupiga vita Uislamu.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan katika vyuo vikuu pia waliweka kona kwa ajili ya mazungumzo na majadiliano, yenye kichwa: “Makubaliano ya Mfumo wa Kisiasa…Mlima Umezaa Panya”, katika Chuo Kikuu cha Al-Neelain, Kitivo cha Biashara, mnamo Disemba 8, 2022, ambapo Ustadh Ahmed Abkar alizungumza, ambapo alielezea uhalisia wa makubaliano hayo ambayo yalikuja kama maagizo ya kigeni na akataja taarifa zinazothibitisha hilo. Pamoja na msingi ambao makubaliano hayo yaliegemezwa; Ni katiba ya usimamizi wa wanasheria wa kisekula na pia imetungwa na nchi za kigeni. Alimnukuu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa UNITAMS, Volker Perthes, "Katiba ya mpito iliundwa na mwanachama wa Umoja wa Mataifa," na kuashiria kuwa makubaliano haya hayatatui mgogoro wa nchi kwa sababu yanatekeleza ajenda ya nje.

Katika muktadha huo huo, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika vyuo vikuu waliweka kona ya mazungumzo na majadiliano, yenye kichwa: “Makubaliano ya Kisiasa... Utafiti wa Kiuhalisia na Mtazamo wa Sharia”, katika Chuo Kikuu cha Sudan, mrengo wa magharibi, mnamo Disemba 13, 2022, ambapo Dkt. Muhammad Abdul Rahman alizungumzia mtego uliotegwa na wanajeshi kwa ajili ya sehemu ya kiraia baada ya kuwafurusha watu mabarabarani na wakapoteza umaarufu; badala yake, barabara zikawa dhidi yao. Hivyo lilikuwa ni pigo lililoelekezwa na jeshi dhidi ya Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko, Baraza Kuu, na wakagawanya sehemu ya kiraia katika kambi mbili, kambi iliyosaini makubaliano na kambi iliyokataa, na hii ni faida kwa jeshi. Ama kipengee cha pili ambacho Dkt. Muhammad alijadili msingi wa muundo wa makubaliano, yaani katiba ya usimamizi wa wanasheria, ambayo ni ya kisekula kikamilifu na inafungua njia ya mgawanyiko wa nchi kwa wazo la ufederali. Kadhalika, katiba hii ilisisitiza kubakia hai kwa ugomvi wa kikabila kupitia kutabanni haki ya kihistoria ya hawakeer, sheria ya umiliki wa ardhi ya Kiingereza. Akahitimisha hotuba yake kwamba makubaliano haya yote ni maovu yanayozidi kukithiri ambayo watu hawana budi kuyakataa na kufanya kazi kutafuta mfumo mbadala unaoshughulikia matatizo, ambao ni Uislamu kupitia dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Ama mzungumzaji wa pili, Ustadh Al-Fateh Abdullah ambaye alianza hotuba yake kwa kuvuta hisia za wanafunzi kwenye msingi ambao makubaliano na masuluhisho hayo yameegemezwa. Ni uraia, hivyo alieleza kuwa katiba yoyote iliyoegemezwa kwenye msingi wa uraia ni batili na haishughulikii matatizo; badala yake, inayafanya kuwa magumu. Suluhisho ni kuifanya imani ya Kiislamu kuwa ndio msingi wa katiba. Hivi ndivyo Hizb ut Tahrir imeonyesha katika rasimu ya katiba ambayo inaitabanni kutoka katika Uislamu.

"Suluhisho la kisiasa ni jengo dhaifu linalotishia wakaazi wake" chini ya anwani hii, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Omdurman Magharibi ilitoa hotuba ya kisiasa katika Soko la Libya mnamo Disemba 14, 2022, ambapo Ustadh Ishaq Muhammad Hussein alizungumza. Alisema suluhisho la kisiasa lililotiwa saini kati ya jeshi na Baraza Kuu la Vikosi kwa ajili ya Azimio la Uhuru na Mabadiliko limeegemezwa juu ya waraka wa wanasheria wa kisekula ambao wanataka kuanzisha maisha ya kiraia kwa mwelekeo wa Magharibi kafiri. Suluhisho hili ni jengo dhaifu linalotishia wakaazi wake na yeyote anayelikaribia, kupitia kutabanni ufederali, Hawakir, na Makubaliano ya Juba, ambayo yaliigawanya nchi hii katika maeneo matano.

[إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُمْ لِيَصُدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِلَىٰ جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ

“Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” [Al-Anfal: 36] Kuhusiana na maana ya aya hii tukufu, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Omdurman Magharibi ilitoa hotuba ya kisiasa katika soko la Libya mnamo tarehe 21 Disemba 2022, ambapo Ustadh Abdul Rahim Abdullah alisisitiza makubaliano yao mabaya (makubaliano ya muundo) ambayo yalitenga euro milioni 5 kwa wanawake na wanaharakati wa vijana kutekeleza njama hiyo. Uingiliaji huu wa wazi wa Makafiri unaonyesha dori yao katika kufanya maamuzi na kujadiliana na pande mbalimbali ili kufikia malengo yao.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika vyuo vikuu waliweka kona ya mazungumzo na majadiliano katika Chuo Kikuu cha Al-Neelain, Kitivo cha Uchumi, yenye kichwa: "Mapinduzi ya Disemba na Uhuru kwa Mukhtasari" mnamo Disemba 22, 2022, Mhandisi Hamdan alionyesha jinsi mapinduzi yalivyotokea kwa ghafla kama matokeo ya shida na migogoro. Hata hivyo, yalitekwa nyara na wapatilizaji fursa na kugeuzwa kuwa serikali ya kiraia ya kidemokrasia isiyo ya kisekula ambayo ina chuki na Uislamu na wakaiacha imani yao na kuitaka hiyo.

Mnamo tarehe 24 Disemba 2022, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan walifanya mkao wao la kawaida katika mji wa Gadharef. Waraka wa kwanza uliwasilishwa na Ustadh Haitham Ali, ambapo alishughulikia uhalisia wa makubaliano hayo, na kuyataja kuwa ni upotevu wa nchi za Magharibi na mabaki yake ambayo hayakuleta chochote na wala hayataleta chochote isipokuwa hasara na maangamivu, kwani alionyesha kwamba makubaliano hayo yanadhihirisha fahamu za Magharibi Kafiri na utekelezaji wa wazo la maridhiano, ambalo kwa hakika ni kugawanya maslahi ya nchi za kikoloni; Marekani na Ulaya kupitia zana zao (jeshi na raia) bila kujali suluhisho halisi la matatizo ya nchi hii. Vile vile alifafanua kutozingatiwa kwa makusudi matamanio ya watu wa nchi hii kama Waislamu, kwani wao ni asilimia 96 ya watu wote, hivyo mkataba huo unawalazimishia vifungu ambavyo vimeundwa ili tu kuuweka mbali Uislamu na maisha.

Chini ya anwani: "Dondoo kutoka kwa Katiba ya Dola ya Khilafah", Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Omdurman Magharibi ilitoa hotuba ya kisiasa katika Soko la Libya mnamo Jumatano, Disemba 28, 2022, ambapo Ustadh Ishaq Muhammad alizungumza, alipoanza hotuba yake kwa kukariri kifungu cha kwanza cha utangulizi wa rasimu ya katiba ya Dola ijayo ya Khilafah, biidhnillah. Alieleza kwamba dola huibuka kwa kuibuka mawazo mapya kwa msingi wake, na mamlaka ndani yake hubadilika kwa mabadiliko ya mawazo haya. Vile vile aliifafanua dola kuwa ni chombo cha utekelezaji  jumla ya fahamu, vipimo na ukinaifu, na kwa kubadilisha fahamu hizi kuwa za Uislamu, dola ya Uislamu inasimama; dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilaya Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu