Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Ugawanyaji Matoleo dhidi ya Muundo wa Makubaliano!

Ndani ya wigo wa kampeni ya kukataa muundo wa makubaliano unaoanzisha maisha ya Sudan juu msingi wa itikadi ya Magharibi Kafiri na kuondosha zile zilizobakia katika hukmu za Uislamu kutoka katika maisha na mujtamaa, na kwa kuitikia amri ya Mwenyezi Mungu (swt) ya kukemea maovu, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, mnamo Jumamosi, 31 Disemba 2022, baada ya swala ya adhuhuri, iligawanya matoleo kwa waumini katika Msikiti Mkuu wa Khartoum, ambayo yalibeba fikra kama vile: “Ndugu yangu Muislamu, kwa nini ni wajibu juu yako kisheria kukataa muundo huu wa makubaliano na kuupinga? Kwa sababu yanaeleza katika kifungu cha kwanza/3 kwamba “Sudan ni nchi ya kiraia na ya kidemokrasia ambamo ubwana ni wa watu.” Hili ni kinyume na Uislamu kwa sababu dola ya kiraia kwa nafsi yake ni dola ya kisekula ambayo inatenganisha dini na mifumo ya maisha na sheria, na demokrasia hujaalia utungaji sheria kuwa ni wa wanadamu. Ama Uislamu, Aqidah ya Kiislamu ndio msingi wa dola, mifumo ya maisha na sheria, na mfumo wa utawala ni Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na ubwana ndani yake ni kwa ajili ya Sharia.”

Waumini waliingiliana na fikra zilizomo kwenye karatasi hizo kwa maswali na mijadala, na baadhi ya waumini walionyesha kukataa kwao kimsingi muundo wa makubaliano hayo na wakatangaza kuunga mkono fikra za Hizb ut Tahrir.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Sudan

- Ripoti ya picha juu ya Ufanisi wa Zoezi la Ugawanyaji wa Matoleo -

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Vyuo Vikuu vya Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu