Alhamisi, 21 Rabi' al-awwal 1443 | 2021/10/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia Yaandaa Maandamano Mawili kwa Ajili ya Kumnusuru Mtume Muhammad (saw)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia iliandaa visimamo viwili vya kumnusuru Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kupinga vita vya kimsalaba vilivyoongozwa na Ufaransa dhidi ya Uislamu, Nabii wa Uislamu na Umma wa Uislamu chini ya pazia la "uhuru wa kujieleza".

Mamlaka ilizuia amali hii ya Hizb na kulenga umati wa watu uliokuwa ukielekea Barabara ya Al-Thawra katika mji mkuu kuwatawanya, huku ikizuia kisimamo ambacho kilipangwa kufanyika asubuhi ya Alhamisi, Oktoba 29 mbele ya ukumbi wa michezo wa Manispaa.

Vikosi vya usalama vilifunga kituo hicho na kuwakamata idadi kadhaa ya Mashababu wa Hizb, ambao ni Ndugu Muhammad Alaa al-Din Arfaoui, Ndugu Muhammad Ali al-Salmi, Ndugu Muhammad Amin al-Zawatni na Ndugu Sufyan al-Abbasi.

Walakini, Mashababu wa Hizb waliweza kusambaza idadi kubwa ya kampeni laini katika barabara za mji mkuu, kuhusu umuhimu wa kumnusuru Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Vyombo vya habari vya nchini vilinakili matukio ya shambulizi kwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika mji mkuu huu.

Kwa kushirikiana na amali za chama katika mji mkuu, Mashababu wa Hizb ut Tahrir huko Kairouan walisajili uwepo wao kwa kutekeleza kisimamo dhidi ya vitendo vya uhasama vya Ufaransa kwa Nabii wa Ummah huu (saw) huko Bab Djalladine, ambapo Ndugu Ezzedine Aouishawi alitoa hotuba ambayo alitaja uhalifu wa Ufaransa na majibu ya Khilafah wakati wa enzi ya Sultan Abdul Hamid II. Katika hilo, aliwataka watu wa Tunisia, juu yao watu wa nguvu na mamlaka, kusimama nasi katika kuipigia debe Dini hii na Mtume wetu mtukufu (saw) ili kusimamisha dola inayotekeleza Shariah ya Mwenyezi Mungu na inayoongozwa kwa mwongozo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Kampeni hizi laini zilitumika kuwakumbusha watu juu ya umuhimu wa kuunusuru Uislamu na Nabii wa Uislamu kupitia kusimamisha dola ya Uislamu, Khilafah Rashidah wa pili kwa njia ya Utume.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Tunisia

Amali za Pembeni za Hafla Hii

Matangazo ya Vyombo vya Habari ya Hafla Hii

Bonyeza Hapa kwa Linki za Kiarabu

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 10 Novemba 2020 10:44

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu