- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Amali za Hizb ut Tahrir kwa Ajili ya Kuvunjwa Khilafah
1443 H – 2022 M
Katika mwezi wa Mtukufu wa Rajab mwaka huu 1443 H / 2022 M na kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mbaya ya wahalifu kuivunja Dola ya Kiislamu na kuondolewa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab 1342 Hijria sawia na Tarehe 3 Machi 1924 M.
Ukurasa huu tutaangazia amali zilizoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Uturuki katika mwezi wa Rajab wa 1443 H katika kumbukumbu ya miaka 101 ya kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah tarehe 28 Rajab 1342 H kama sehemu ya amali za kimataifa za Hizb ut Tahrir.
Twamuomba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa’la aharakishe kusimama kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya hili.
Ijumaa, 03 Rajab 1443 H - 04 Februari 2022 M
- Video ya Ripoti kuhusu Amali "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi" -
Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki Enyi Waislamu! Je, Haijatosha kwamba Mumekaa Karne Moja bila ya Khilafah?! |
Mpangilio wa Makongamano ya Kiuchumi
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Halaqa ya Mjadala Mjini Karaman Kutafuta Suluhisho la Kiislamu kwa mgogoro wa kiuchumi
Ndani ya wigo wa msururu wa makongamano, semina na halaqa za mjadala zilizoandaliwa na Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki chini ya kichwa "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi", sanjari na mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 101 ya kuvunjwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, Hizb ilikutana na wawakilishi wa vyama vya kisiasa, mashirika yasiyo ya kiserikali, wawakilishi wa vyombo vya habari vya ndani na walezi katika mji wa Karaman.
Katika mkutano huo uliofunguliwa na Ndugu Burhanuddin Kirjilan, Ustadh Suleiman Ugarlua (Mhariri Mkuu wa Jarida la Kokludegisim), ambaye aliwasilisha utafiti wenye mada "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi katika Nukta Kumi". Baada ya uwasilishaji, kipindi cha maswali na majib