Ijumaa, 03 Rajab 1446 | 2025/01/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Visimamo vya Kulaani "Kamwe Hatutaitelekeza Turkestan Mashariki!"

Utawala katili wa China unaendelea na mauaji na ukatili katika eneo la Turkestan Mashariki ambayo iliikalia kimabavu kwa miongo kadhaa bila ya kupungua, ambapo dola ya China, ambayo imewafungia mamilioni ya Waislamu wa Uyghur katika kambi za uzuizi kwa jina la (utoaji elimu), inatumia mateso kama silaha ya kutaka kuwaondoa Waislamu wa Turkestan Mashariki kutoka kwenye kitambulisho chao cha Kiislamu kwa kushajiishwa na watawala walio kimya katika nchi za Kiislamu, mara hii China yenye chuki inatenda jinai mpya dhidi ya Waislamu wa Uyghur huko Turkestan Mashariki, haswa katika mji wa Golka, ambapo Wauyghur walifungwa majumbani mwao kwa miezi kadhaa na milango yao imefungwa kwa nje kwa kisingizio (kuzuia kuenea kwa janga la Korona), kwani picha za video kutoka mkoa huo zilionyesha kuwa watu wengi wasioruhusiwa kukidhi mahitaji yao ya kimsingi, hasa chakula na dawa, wanakabiliwa na balaa la njaa, na baadhi ya watu ambao watoto wao walizimia kwa kukosa chakula na kufia nyumbani.

Kuhusiana na hayo yote, Hizb ut-Tahrir/Wilayah Uturuki iliandaa visimamo viwili vya kulaani katika Msikiti wa Mehmet Al-Fateh jijini Istanbul na katika Msikiti wa Haji Bayram jijini Ankara ili kuwatetea ndugu zetu Waislamu wa Turkestan Mashariki dhidi ya ukatili unaofanywa na utawala wa kihalifu wa Kichina, na kuwataka watawala nchini Uturuki hasa na watawala wengine katika nchi za Kiislamu kwa jumla kusitisha kimya chao na kuwanusuru Waislamu wa Turkistan Mashariki.

Kwa Mengi zaidi Bonyeza Hapa

Ijumaa, 20 Safar Al-Khair 1444 H - 16 Septemba 2022 M

 

- Sehemu ya Amali ya Kisimamo cha Msikiti wa Haji Bayram jijini Ankara -

- Sehemu ya Amali ya Kisimamo cha Msikiti wa Mehmet Al-Fateh jijini Istanbul -

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Tovuti ya Jarida la Kokludegisim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu