Alhamisi, 06 Ramadan 1446 | 2025/03/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Kongamano la kila Mwaka la Khilafah: “Kujenga Mustakabali pamoja na Khilafah kutoka Istanbul hadi Al-Qudsi!”

Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 104 Hijria ya kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah (miaka 101 M), Hizb ut Tahrir/Wilayah Uturuki iliandaa Kongamano la kila mwaka la Khilafah kwa ushiriki mpana chini ya kichwa:

“Kujenga Mustakabali pamoja na Khilafah kutoka Istanbul hadi Al-Qudsi!”

Programu ya kongamano hilo lililofanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Nene Hatun huko Esenyurt, Istanbul, lilianza kwa usomaji wa Qur'an Tukufu, na kufuatiwa na hotuba ya ufunguzi.

Kongamano hilo lilisimamiwa na kufunguliwa na mjumbe wa Afisi ya Habari vya Hizb ut Tahrir, Ustadh Muhammad Amin Yildirim, na kuhudhuriwa na watu kadhaa mashuhuri, kama vile Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mshikamano wa Palestina, Muhammad Michinish, mwandishi na mwanatheolojia Dkt. Ahmad al-Tayyib, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Palestina, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mshikamano wa Palestina, Muhammad Yusuf wa Jumuiya ya Mshikamano wa Muhammad. Na Dkt Abdul Rahim Shen na mwanachuoni wa kidini Abdullah Imamoglu walishiriki katika kongamano kama wazungumzaji.

Katika hotuba ya ufunguzi ilisisitizwa kwamba kuondolewa kwa Khilafah ni moja ya maafa makubwa yaliyoukumba Umma wa Kiislamu, na ikakumbukwa kuwa Khilafah ilikuwa jijini Istanbul miaka 104 H iliyopita (101 M), na kwamba Al-Qudsi ilikuwa imelindwa kwa karne nyingi kutokana na Khilafah.

Mauaji ya halaiki huko Ghaza, mashambulizi dhidi ya Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa, na ufisadi na dhulma katika ardhi za Kiislamu vinahusiana moja kwa moja na kutokuwepo Khilafah. Aidha ilisisitizwa kuwa mwezi wa Ramadhan usiwe mwezi wa ibada kwa Umma pekee bali uwe mwezi wa mwamko na kuamsha.

Baada ya hotuba ya ufunguzi, Rais wa Jumuiya ya Mshikamano wa Palestina (FİDDER) Muhammed Mishinich alitoa hotuba ya kwanza ya kongamano hilo. Mishinich alianza hotuba yake kwa kuwasalimia watu wa Gaza. Mishinich alisisitiza kuwa anafuatilia kwa karibu matembezi, kauli na shughuli za Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki kuhusiana na Palestina na Gaza, na kwamba yeye binafsi anashiriki katika shughuli hizi na amefurahishwa sana na hilo. Alisema usitishaji vita unaoendelea huko Gaza ni wa muda, na kwamba umbile la Kiyahudi linalokalia kimabavu kamwe halitimizi ahadi yake, na kwa hivyo vita vitaendelea.

Mzungumzaji wa pili katika kongamano hilo ni mwanatheolojia na mwandishi Dkt. Abdul Rahim Shen alitoa tathmini muhimu kuhusu siku zilizopita, za sasa na zijazo za Khilafah. Alieleza kwa mifano chungu nzima jinsi Umma wa Kiislamu ulivyotoa mfumo wa ulimwengu kwa karne nyingi, na kuunda mazingira ya uadilifu na usalama kutokana na Khilafah, lakini kwa kuporomoka kwa Khilafah, Waislamu wakawa watumwa katika nchi yao wenyewe. Abdul Rahim Shen alisisitiza kuwa mfumo wa sasa wa ulimwengu umeporomoka na kwamba yanayojiri duniani kwa hakika yanaiita Khilafah katika medani ya kisiasa, na kubainisha kuwa Dola ya Khilafah pekee ndiyo yenye uwezo wa kujaza ombwe la kisiasa la sasa. Alisisitiza kuwa Waislamu lazima waungane katika kuijenga upya Khilafah.

Msemaji wa mwisho katika kongamano hilo, mwanachuoni na mwandishi wa kidini Abdullah İmamoğlu, alianza hotuba yake kwa hadith mbili za Mtume Muhammad. Katika Hadith ya kwanza: «الصيام جنة» “Saumu ni ngao,” na katika Hadith ya pili: «الإمام جنة» “Imam ni ngao.” Imamoglu alisisitiza kuwa, Waislamu wote wanajua kuwa Saumu ni kinga na ni ngao dhidi ya adhabu ya Akhera, lakini hawawezi kushuhudia jinsi Khalifa anavyoweza kuwa mlinzi na ngao kwao, kwa sababu Khilafah imeondolewa na Waislamu wamekuwa bila mwenza. Alieleza kuwa Rais Trump wa Marekani anataka kuinunua Gaza, kwa sababu hakuna khalifa wa kuwalinda Waislamu na ardhi iliyobarikiwa. Abdullah Imamoglu alitoa mifano mmoja baada ya mwingine ya ukandamizaji, uvamizi na mauaji ambayo Waislamu walifanyiwa baada ya kuporomoka kwa Khilafah, na akasema kwamba Machi 3 ilikuwa siku ya giza. Imamoglu aliendelea na hotuba yake kama ifuatavyo: “Wale walioivunja Khilafah walitaka kuufuta kutoka katika nyoyo zetu, lakini walishindwa!” Walitaka kunyamazisha sauti za wale waliotaka Khilafah, lakini hawakuweza! Leo tunailingania ili ardhi na mbingu zisikie: Jina la eneo ni Uislamu! Jina la wanajeshi wake ni Waislamu! Kamwe hawataweza kulitikisa lililoundwa na askari wa Uislamu! “Khilafah itasimama tena na majeshi yake yatavunja ngome za mchanga za madhalimu hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda!”

Hotuba ya Abdullah Imamoglu iliishia kwa dua, na iliingiliwa kati kwa Takbira za kurudiwa-rudiwa ndani ya ukumbi.

Na dua yetu ya mwisho ni kwamba sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Kwa Maelezo Zaidi Bonyeza Hapa

Jumapili, 02 Ramadhan Al-Mubarak 1446 H sawia na 02 Machi 2025 M

 

­- Video Kamili ya Amali za Kongamano la kila Mwaka la Khilafah -

- Picha za Amali Za Kongamano la kila Mwaka la Khilafah -

- Alama Ishara za Amali -

#أقيموا_الخلافة

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

#خلافت_کو_قائم_کرو

#TurudisheniKhilafah

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Kwa Maelezo zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Tovuti Rasmi: Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Facebook: Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Twitter: Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Instagram: Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

YouTube: Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Jarida la Koklu Degisim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu