- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Tafsiri Al-Baqarah [Muhkam na Mutashabiha]
Kutoka Kitabu, Utangulizi wa Tafsiri ya Quran,
cha Amiri wa Hizb ut Tahrir, Faqihi Mkubwa na Mwanadola, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
Muhkam na Mutashabiha (المحكم والمتشابه Zilizo na maana dhahiri na zinazoshabihiana maana)
(Imetafsiriwa)
Jambo muhimu katika sayansi ya Quran linalohusiana na tafsiri ya aya za Mwenyezi Mungu, mbali na maana halisi na ya kimajazi, ni kuwepo kwa yaliyo wazi na yaliyo na utata katika Kitabu. Mwenyezi Mungu (saw) amesema,
[هُوَ الَّذِيَ أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ في قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاء الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاء تَأْوِيلِهِ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلاَّ اللّهُ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلاَّ أُوْلُواْ الألْبَابِ]
“Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili.” [Aali Imran: 7]
Je, tafsiri ya aya zinazoshabihiana inajulikana kwa Mwenyezi Mungu pekee (swt), au kwa Mwenyezi Mungu pekee (swt) na wale walio na msingi imara katika elimu?
Kwa maana nyengine, je, herufi “waw” katika [وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ] “Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu” ni kwa ajili ya kiunganishi, ili [وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ] “Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu” wawe wameunganishwa na Mwenyezi Mungu (swt), na hivyo wanajua tafsiri ya zinazoshabihiana, au ni “waw” kwa ajili ya mwendelezo wa kuendelea, ili kusimama iwe ni lazima baada ya [إِلاَّ اللّهُ] “isipokuwa Mwenyezi Mungu,” ili kwamba Mwenyezi Mungu pekee (swt) ndiye anayejua tafsiri ya zinazoshabihiana, na zile zilizo imara katika maarifa ndio mwanzo wa sentensi mpya inayoendelea tena katika mwendelezo?
Kwa kutafakari aya hii tukufu, inakuwa wazi kwamba maana inayowezekana zaidi ya herufi “wa” bila shaka ni kiunganishi (atf), sio mwendelezo wa kurudia (istinaaf), kwa sababu zifuatazo:
1. Mwenyezi Mungu (swt) asema, [هَٰذَا بَيَانٌ لِّلنَّاسِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ] “Hii ni bayana kwa watu wote, na ni uwongofu, na mawaidha kwa wachamngu.” [Surah Aali Imran 3:138]. Ikiwa kiunganishi “wa” (na) kinatumika kuashiria mwanzo mpya, ikimaanisha kwamba Mwenyezi Mungu (swt) pekee ndiye anayejua tafsiri ya aya zinazoshabihiana za Quran, basi hii ina maana kwamba kuna aya katika Quran ambazo watu hawazielewi. Hii itamaanisha kwamba Quran si kauli iliyo wazi kwa wanadamu, kwani ina aya ambazo maana yake watu hawawezi kuelewa. Kwa hivyo, kutafsiri “wa” kama kuashiria mwanzo mpya kunagongana na maana ya aya, [هَٰذَا بَيَانٌ لِّلنَّاسِ] “Hii ni bayana kwa watu wote” [Surah Aali Imran 3:138].
Ama kuhusu kuifanya “waw” kuwa ni ya kiunganishi, hutoa maana: kwamba utata unaweza kuelezewa kwa watu kupitia wale walio na msingi imara katika elimu, na hii inaendana na Quran kuwa ni ufafanuzi kwa watu.
2. Mwenyezi Mungu (swt) ametaja sifa ya ziada kwa Maulamaa, ambayo ni msingi imara katika elimu. Katika Kiarabu, kutaja sifa ya ziada kunafaa kwa hukmu inayohusiana nayo. Ikiwa kiunganishi “wa” (na) ni cha mwendelezo wa kurudia, basi sentensi ifuatayo ni mpya, ikimaanisha usomaji unaanza nayo, [وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ] “Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: ‘Sisi tumeziamini’” Hii ina maana kwamba sifa hii ya ziada ya msingi imara katika elimu inahusiana na [يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ] “husema: ‘Sisi tumeziamini” Kwa kuwa imani haihitaji sifa ya ziada ya elimu, na kwa kweli Maulamaa na hata wasio Maulamaa wana uwezo wa kumwamini Mwenyezi Mungu (swt) na hawahitaji msingi imara katika elimu ili kuamini, sifa hii ya ziada ya msingi imara katika elimu haiendani na kinachofuata, [يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ] “husema: ‘Sisi tumeziamini” pamoja na hiyo.
Hata hivyo, ukiifanya “wa” kwa ajili ya kuunganisha (atf), basi uthabiti katika elimu unatokana na kujua tafsiri ya utata, na hili kwa hakika linahitaji uthabiti katika elimu, kwa sababu Aya zenye utata ni zile zenye maana zaidi ya moja na ni vigumu kubainisha maana iliyokusudiwa, na hivyo maana yake ni ya kutatanisha kwa msikilizaji na msomaji, kama vile, [يَدُ اللَّهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ] “Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao.” [Surah Al-Fath 10] [وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ] “Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi” [Surah Ar-Rahman], na kama [وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ] “Na wanawake walio achwa wangoje peke yao mpaka t'ahara (au hedhi) tatu zipite.” [Surah Al-Baqarah 228], kwa hivyo hii sio maana (dalaalah) ambayo ni ya kukatikiwa (qaati'ah) kama ile iliyo wazi ambayo ina maana moja pekee.
Katika hali hii, aya usioeleweka kihakika inahitaji msingi imara wa maarifa ili kuelewa tafsiri yake; yaani, hauhitaji tu maulamaa kuelewa tafsiri yake, bali pia maulamaa walio na msingi imara wa elimu.
Maelezo ya ziada ya uthabiti katika elimu yanafaa ili kuelewa tafsiri ya utata. Kiunganishi “waw” (na) kinafadhilishwa katika uunganishi, na usomaji ni, [وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلاَّ اللّهُ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ] “na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu.”
Kutokana na hili, ni dhahiri kwamba tafsiri inayowezekana zaidi ya “waw” iliyotajwa hapo juu ni ile ya kiunganishi.
Maana ya aya tukufu ni kwamba Quran ina aya zilizo wazi na zilizo na utata, ambazo maana zake ziko wazi na hazihitaji juhudi kubwa kuzielewa. Badala yake, zinaweza kueleweka na wale ambao Mwenyezi Mungu amewapa ujuzi unaofaa.
Na pia ina aya zengine ambazo zina utata, ambazo maana zake hubadilika kati ya tafsiri zaidi ya moja. Hizi zinahitaji juhudi kubwa ili kubaini maana inayowezekana zaidi, na haihitaji tu maulamaa bali wale walio na ujuzi zaidi, wale walio na msingi imara katika maarifa, kuzitafsiri na kubaini maana inayowezekana zaidi.
Aya hiyo pia inafafanua mambo mawili muhimu:
1. Aya za muhkam (wazi) ndizo msingi wa Kitabu, ikimaanisha asili yake na kile kinacho kusudia. Hii ina maanisha kwamba ikiwa maandiko mawili yanazungumzia suala moja, moja ikiwa na maana moja, iliyo wazi na isiyo na utata, na nyengine yenye maana nyingi, mutashabiha (iliyo na utata), basi aya iliyo wazi inashinda ile isiyo na utata, na maana ya aya iliyo na utata lazima itafsiriwe kwa kuzingatia ile iliyo wazi.
2. Wale ambao nyoyo zao zina shaka na kupotoka kutoka kwenye ukweli huingia kwenye aya zilizo na utata, bila ya kuwa na sifa zinazohitajika, wakitafuta kupanda ugomvi na kupotosha ukweli kupitia tafsiri potofu na uwasilishaji wa makosa, wakilenga kusababisha mkanganyiko na upotoshaji.
Kwa hivyo, wale wanaoingia kwenye aya zilizo na utata bila sifa zinazohitajika wanaweza kutenda dhambi kubwa, ambalo linaweza kusababisha ukafiri, na kusababisha kukataa kiungo msingi cha Iman au hukmu ya Sharia inayojulikana kwa udharura katika Uislamu (معلوم من الدين بالضرورة ma’loom min ad-Din bidharurah).
Yeyote asiyejua tafsiri ya aya zilizo na utata anapaswa kusema, “Sijui,” kwani jambo hilo ni zito na halihitaji elimu tu bali pia ufahamu wa kina. Ikiwa mtu hana sifa hiyo, basi anapaswa kutafuta mwongozo kutoka kwa mujtahiduna (mafaqihi wenye uwezo wa kuvua hukmu) ambao wana sifa na kujifunza kutoka kwao, ili asije akapata Ghadhabu kubwa ya Mwenyezi Mungu (swt).



