- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Uadilifu wa Kweli Ni Kuliondoa Umbile Vamizi la Kiyahudi
Habari:
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imekataa pingamizi dhidi ya 'uamuzi wa kutoihukumu 'Israel' uliochukuliwa na Afisi ya Mashtaka kuhusiana na meli ya Mavi Marmara ambayo Waturuki 9 waliuwawa. Kiongozi wa Mashtaka wa ICC Fatou Bensouda alikuwa ameikataa kwa mara ya tatu faili ya uchunguzi mnamo Disemba 2019, kwa hoja kuwa "hakukuwa na hoja yoyote ya kufanya uchunguzi". Mahakimu wa ICC alitangaza kuwa wamekataa ombi la Ngazija ambako meli ya Mavi Marmara imesajiliwa na ambao ndio walioileta kadhia hii jijini The Hague, kwa ajili ya kutathmini upya uamuzi wa Bensouda.
Maoni:
Kama ambavyo mtakumbuka na katu hamtasahau, kaka zetu Waislamu 10 waliuwawa mashahidi na 50 kujeruhiwa katika shambulizi la umbile la Kiyahudi kwa meli ya Mavi Marmara, ambayo ilikuwa imeleta msaada wa kibinadamu huko Gaza. Na hapa tunawaombea toba na msamaha kaka zetu hawa waliopoteza maisha katika mshambulizi hilo kutoka kwa Mola wetu. Makaazi yao yajaaliwe kuwa peponi InshaAllah.
Ama uamuzi wa ICC, kamwe si uamuzi wa kushangaza. Kinachofadhaisha baada ya kupitia yote hayo ni kuendelea kutarajia haki kutoka kwa asasi zilizobuniwa na kusimamiwa na mabepari makafiri, ambao lengo lao pekee ni kuangalia maslahi yao wenyewe.
Wakati huo huo, kesi hiyo kiuhalisia tayari ilikuwa ishafungwa mnamo 2016. Uturuki na umbile la Kiyahudi zilikuwa zimekubaliana badali ya fidia ya dolari milioni 20, maombi yote yalikataliwa. Zaidi ya hayo, baada ya makubaliano hayo iliamuliwa kwamba Uturuki inapaswa kuziba hasara kutokea kutokana na kwa kesi yoyote ya kisheria kuhusiana na umbile la Kiyahudi.
Hivyo basi, mashtaka dhidi ya ICC na pingamizi zilizofanywa tayari kisheria zilikuwa hazina maana yoyote. Pengine majaribio haya huenda yakakadiriwa kuwa ni kama deni la kinafsiya kwa Waislamu waliotoa maisha yao na kumwaga damu zao ndani ya Mavi Marmara. Lakini ikiwa majaribio kama haya yanamfunika mkosaji halisi, bila shaka, jambo hilo halikubaliki.
Mkosaji halisi ni nani? Umbile la Kiyahudi?
Uharamishaji wa umbile la Kiyahudi, kulinyoshea kidole cha lawama, si chochote ila ni wepesi wa kawaida. Kihakika, kulikadiria umbile la Kiyahudi kama mkosaji halisi sio adilifu. Ni dola vamizi, mwizi, jambazi, muuwaji wa watoto, na dola yenye kuhangaisha. Yote haya ni kweli! Lakini vipi kuhusu watawala, dola, majeshi wanaoipa fursa ya kutekeleza uhalifu huu? Na vipi kuhusu watu, vyama, CSO, wanachuoni, viongozi wa rai na mashabiki wanaokuja na nyudhuru za kuwafanya viongozi wao waonekane kama wasio na hatia? Je, wao kamwe si wa kulaumiwa? Au wao ndio wakosaji halisi?
Hebu fikiri! Vuta taswira!
Vuta taswira kwamba nchi ambazo watu wake ni Waislamu zimeungana chini ya paa la dola moja. Vuta taswira kwamba jeshi lao ni jeshi moja, kwamba utajiri wao na njia zao zote, pembejeo zao za kilimo, uchumi wao, nguvu-kazi yao ni moja. Na pia, vuta taswira kwamba dola hii inatawaliwa na kiongozi, Khalifah kama Abdul Hamid, Suleiman Mtukufu, Al-Mu'tasim Billah, Harun al-Rashid, Umar ibn Abd al-Aziz.
Na ujibu!
Ni nani atakayeweza kusubutu kwenda dhidi ya dola hii? Ni nani atakayeweza kuwa na jicho juu ya shubiri moja ya ardhi ya dola hii? Ni nani atakayeweza kumvamia mtu miongoni mwa watu wa dola hii? Je, Msikiti wa Aqsa, uliobarikiwa na Mwenyezi Mungu, ungebakia chini ya uvamizi wa umbile la Kiyahudi? Inawezekana vipi kwamba Mayahudi hawa wavamizi, ambao wanaogopa hata vivuli vyao wenyewe, kubakia nchini Palestina? Je, Amerika, Uingereza, Ufaransa, Urusi, China zingeweza kuamiliana na Waislamu kwa kiburi, jeuri kama zinavyofanya leo? Je, kungekuwa na tatizo kama Turkestan Mashariki? Je, Kashmir ingesalimishwa kwa Mabaniani wapagani? Je, ardhi za Kiislamu zingegawanywa kaskazini, kusini, mashariki na magharibi? La muhimu zaidi, ni nani angemtusi mwenye thamani zaidi kwetu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) chini ya jina la uhuru wa rai? Je, wale wanaosubutu kumtusi hawangeonja mkono wa chuma wa majeshi ya Uislamu?
Ndio, tungekuwa mkono wa chuma na mkanyago na moto na kuchoma wale walio na jicho juu ya ardhi za Kiislamu, wale wanaovamia maisha, utajiri na heshima ya Waislamu, wale wanaomtusi Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na umbile vamizi la Kiyahudi!
Sasa, fungueni macho yenu na rudini leo. Simameni ili mzifanye ndoto zenu kuwa kweli! Jikukuteni utandu! Msiwaamini tena viongozi hawa juu yenu, wanaowauza na kuwavunja moyo katika kila fursa! Wao tayari wamekwisha kwama ndani ya khiyana ya kudumu, mithili ya maiti. Nyinyi ndio mtakaofanya hili! Nyinyi ndio mtakaozifanya ndoto zenu ziwe kweli! Nyinyi ndio mtakaoiokoa Palestina, Msikiti wa Aqsa! Nyinyi ndio mtakaosimamisha Khilafah Rashida (kwa Njia ya Utume)!
Msisahau! Kumbukeni na mkumbushe!
Ummah wa Kiislamu ni taifa bora lililotolewa kwa watu. Uwepo wake wa kimaumbile ni thabiti mno kurudisha kila kitu ulichokipoteza, kwa sababu ni Ummah wa Muhammad (saw), asiyekubali kusalimu amri, asiyekubali kusalimisha, asiyedhoofika, asiyekata tamaa na kushinda katika da'wah aliyoianzisha peke yake!
Msisahau! Kumbukeni na mkumbushe!
Ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli! Bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ni ya kweli! Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wamesema kweli!
Mwenyezi Mungu huwanusuru waumini, watiifu, wale wanaojitolea kwa ikhlasi, wenye ikhlasi na kujitolea na atawapa ukhalifa juu ya ardhi. Itakuwepo tena Khilafah kwa njia ya Utume.
Basi, ndoto zenu kihakika ndio ukweli wenyewe! Na mko karibu sana kufikia na kunyakua!
Kile ambacho mwapaswa kufanya ni kukamata mkono ulionyoshwa wa Hizb ut Tahrir ili kuuangana pambizoni mwa ukweli pekee, na kufanya kazi kwa ikhlasi!
Mola wetu aturuzuku kushuhudia namna ambavyo umbile la Kiyahudi litakavyo furushwa kutoka katika maeneo yaliyobarikiwa ya Palestina kupitia mkono wetu kabla hatujafa, Allahumma Ameen! Allahumma Ameen, Allahumma Ameen.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Süleyman Uğurlu