Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Wakulima Tisa wa Kiislamu wa Moro Wauwawa Mchana Peupe

Habari:

Taarifa ya habari za Manilla imeripoti wakulima tisa wa Kiislamu wa Moro wameuawa huko Kabacan, Cotabato kaskazini, Ufilipino tarehe 29 Agosti 2020. Mauaji haya yamezua hasira miongoni mwa jamii za Waislamu. Polisi walihusika katika mauaji ya mchana ya wakulima hawa Waislamu kulingana na tangazo la kifo la mmoja wa wahasiriwa, kwa mujibu wa mkurugenzi eneo wa Tume ya Haki za Binadamu katika Eneo la 12 (CHR-12).

Jamaa wa mwathiriwa wa tisa waliwaambia wachunguzi wa CHR-12 kabla ya kufa kwake hospitalini kwamba polisi walisimama na kuwapiga risasi. "Tangazo hili la kifo la mwathiriwa ambaye alifanikiwa kuzungumza na jamaa zake kabla ya kufa akidai polisi walikuwa nyuma ya mauaji hayo litakuwa muhimu sana kwa kesi hiyo." CHR-12 inachukulia mauaji ya wakulima tisa wa Kiislamu wa Moro kama "mauaji ya yaliyokiuka sheria".

Eneo Huru la Bangsamoro katika Mindanao ya Waislamu (BARMM) limetangaza litafanya uchunguzi juu ya mauaji hayo hata kama yako nje ya mipaka yake, likitaja kwamba "wahasiriwa wote walitambuliwa kama watu wa Bangsamoro."

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti yake ya Facebook, Sammy Al Mansor, mkuu wa Wanajeshi wa Vikosi vya Kiislamu vya Bangsamoro (BIAF), alilaani mauaji hayo, akisema kwamba ni mauaji ya halaiki. Tukio hilo alisema "linatukumbusha kipindi cha giza katika siku zetu za hivi karibuni, wakati watu wa Bangsamoro walipozingirwa na kuzungukwa katika nchi yao ya mababu, na vikosi ambavyo vilipewa fadhila na kutojali sheria kuhakikishiwa harakati isiyodhibitiwa katika mauaji ya kishenzi na ya kinyama ya raia wasio na silaha. Mauaji mengi ya mchana peupe katika barabara ya mkoa yanaonyesha imani kwamba hakuna mtu atakayewazuia, na hakuna mtu atakayewaandama. ” Alisema.

Maoni:

Ingawa kwa sasa Waislamu wachache wa Moro nchini Ufilipino wana serikali yao huru chini ya mwavuli wa Sheria ya Kikaboni ya Bangsamoro ambayo ni sehemu ya makubaliano ya amani kati ya Harakati ya Kiislamu ya Ukombozi ya Moro (MILF) na serikali ya Ufilipino, imeonekana kuwa usalama wa Waislamu wa Moro ungali katika hatari kubwa. Dalili za kuhusika kwa polisi katika mauaji huko Kabacan zinaonyesha ukosefu wa hatua za usalama kwa maisha ya Waislamu wa Moro ingawa imeandikwa katika kipengee cha Sheria ya Kikaboni ya Bangsamoro Sehemu ya 12 ya Kifungu cha VI kinachosema kwamba "Serikali ya Kitaifa itahakikisha ulinzi wa haki za watu wa Bangsamoro wanaoishi katika jamii nje ya Eneo Huru la Bangsamoro”.

Hii ni kwa sababu uhuru wa Bangsamoro ni uhuru bandia; hawawezi kuwa na vikosi vyao wenyewe vya jeshi na polisi, ingawa wana udhibiti kamili juu ya uchumi, pamoja na mfumo wake wa kimahakama na bunge, lakini serikali ya Bangsamoro bado lazima izingatie masharti ya Katiba ya Ufilipino. Sheria hii ya uhuru, kwa kweli, kamwe haitaunda uhuru msingi kwa Waislamu wachache wa Moro, pamoja na wanawake wa Kiislamu na watoto wa Moro ambao wameonewa kwa miongo kadhaa na zaidi ya maisha ya Waislamu wa Moro 120,000 wamepotea kwa karibu miaka 50. Sheria yoyote inayopeanwa na utawala wa kisekula wa kikafiri kwa kweli haitawaruhusu Waislamu kuiweka Qur'an kama katiba yake kuu zaidi ingawaje imepewa mamlaka zaidi katika sera ya uchumi na mamlaka kidogo ya hukmu ya sharia. Sheria hii ni mtego tu wa kuwafanya Waislamu wawe wa wastani na wa kisasa. Jitihada zote zinazofanywa na Duterte na asasi za kimataifa zinalenga kufikia lengo moja, nalo ni kwamba Uislamu haupaswi kuwa kusimama wima kusini mwa Ufilipino.

Hakuna kilicho tofauti na ndugu zetu katika eneo la Kabacan, kama ilivyo hali katika nchi nyingine ambazo aghlabu sio za Kiislamu ambapo ubaguzi dhidi ya Waislamu wachache ni mkubwa. Waislamu wa Moro kusini mwa Ufilipino hawatofautiani nao. Ikilinganishwa na raia wao wasio Waislamu, Waislamu wengi ambao wanaishi katika Kisiwa cha Mindanao wamesalia nyuma sana katika maisha yao. Hii ni kwa sababu serikali ya Ufilipino huwaona kama waasi. Ijapokuwa eneo hilo ni eneo lenye rutuba zaidi na tajiri kwa maliasili nchini Ufilipino, lakini ukweli unaonyesha, eneo hili limekuwa eneo maskini zaidi nchini humo bila maendeleo, baada ya mzozo ulioanza miongo minne iliyopita. Serikali ya Ufilipino imewakataza Waislamu kutawala katika eneo lao wenyewe na kudhibiti utajiri wao.

Kwa kunukuu taarifa ya al Manshoor "Mauaji mengi mchana peupe katika barabara ya mkoa yanaonyesha ujasiri kwamba hakuna mtu atakayewazuia, na hakuna mtu atakayewaandama" anatuachia swali moja la msingi. Kwa nini maisha ya Ummah wa Muhammad hayana thamani katika zama hizi za kisasa? Wakati Mtume wetu mtukufu (saw) amesema:

«لَزَوَالُ الدُّنْيَا أَهْوَنُ عِنْدَ اللهِ مِنْ قَتْلِ رَجُلٍ مُسْلِمٍ»

“Kuondoka kwa dunia ni sahali zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, kumuuliwa Muislamu mmoja.” (Imesimuliwa na An Nasa’i)

Hivi karibuni chini ya uongozi wa Duterte, utawala huo unazidi kuwakandamiza Waislamu kwa niaba ya ajenda ya kupambana na ugaidi. Kwa miongo kadhaa, wamekuwa wahasiriwa wanyonge wa mtawala katili wa kikafiri ambaye ameruhusiwa kuwepo na mfumo wa ulimwengu unaowabagua Waislamu. Maadamu mfumo huu wa ulimwengu bado ungalivyo kama ulivyo hivi leo, bila shaka mateso ya Ummah wa Muhammad (saw) katika ulimwengu wa Kiislamu kamwe hayatakwisha. Ni kwa sababu mizizi wa mateso yote haya si chochote isipokuwa ni kukosekana kwa Khilafah ambayo ni ngao kwa Waislamu ambayo ingeondoa udhibiti wa makafiri kwa Waislamu na kulinda heshima ya wanawake na watoto wa Kiislamu katika ulimwengu wote wa Kiislamu. Kumbuka maneno ya Mtume (saw):

«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika Imam (Khalifah) ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujilinda kwayo...” (Imesimuliwa na Muslim)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Fika Komara
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu