Alhamisi, 09 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Habari & Maoni
Waislamu Warohingya wanaingia Mwaka Mpya wakiwa na hofu kwa kukosekana Khilafah

Habari:

BBC iliripoti kuhusiana na kupambamoto kwa janga la Rohingya huku idadi ya wanaotarajiwa kushtakiwa dhidi ya serikali ya Myanmar ikiwasilishwa katika mahakama za kimataifa na Venezuela na Gambia. Habari iliyotoka mnamo 19 Novemba 2019 inaelezea hadithi kwamba kijana wa miaka 11 anayeitwa Omar anayeishi pasina familia yoyote katika kambi ya wakimbizi ya Cox Bazaar ndani ya Bangladesh. Mamake na babake waliuliwa kinyama na wanajeshi wa Myanmar na kila siku huamka na kulia akikumbuka kuwapoteza wazazi wake wapendwa. Kaka zake watatu na dada zake wawili nao pia waliuliwa katika msururu wa usafishaji kabila.

Maoni:

Mnamo Septemba 2018, wachunguzi wa UN walihitimisha kwamba majenerali wa Myanmar wanastahiki kufikishwa kizimbani kutokana na vitendo vyao dhidi ya Waislamu wa Jimbo la Rakhine ambapo zaidi ya Warohingya 700,000 walifurushwa ndani ya Bangladesh. Lakini mpaka wa leo hakuna hata afisaa mmoja aliyefikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Huku udhuru unaotolewa kwa kukosekana kupatikana kwa haki unaelezewa na Laetitia van den Assum ambaye ni mwanachama wa tume huru kuhusiana na hali ya Rakhine ikiongozwa na Katibu wa Kudumu wa zamani wa UN – Kofi Annan. Nukuu kuhusiana na kukosekana ufuatiliaji ni kama ifuatavyo; “Ni kweli maendeleo yanaweza kuwa polepole, lau utakuwa na cheo katika uongozi mkuu utalindwa, hakuna atakayekupeleka Hague.” Suala jingine lenye kuleta tashwishi ni kwamba Mshindi wa Tuzo ya Nobel Aung San Suu Kyi anatumia ngao ya kutohusika na kwamba kikatiba hana udhibiti wa jeshi. Mauaji ya kila siku ya wanaume, wanawake na watoto wasiokuwa na hatia yataendelea tukiingia mwaka mpya pasina kusitishwa na mamlaka yoyote kwa kuwa mahakama hizi za kimataifa za uhalifu zipo tu kuwahesabu watu binafsi fulani na zinahudumikia malengo na ajenda za kimagharibi. Tukizingatia kwamba serikali za kimagharibi zinaruhusu biashara zao kufanyika na Myanmar na kutengeza mabilioni katika faida inathibitisha kutowajibika kiukamilifu katika kuwasaidia Waislamu wa Myanmar. Uwepo wa kiongozi wa kweli wa Kiislamu kwa sura ya Khilafah itakuwa ndio umbile pekee ambalo halitokubali Warohingya kutaabika huku na kule duniani au kutiwa korokoroni katika kambi kama wanyama. Ilhali viongozi Waislamu duniani wameamua kusahau tabu nzito zinazoukumba Ummah, Mwenyezi Mungu (swt) hatosahau kujitoa muhanga kutokana na Iman. Tunawaombea mashahidi na wale watakaokuja wakiwa washindi katika Maisha ya Akhera na wale wanaoingia mwaka mpya huku wakiwa na hofu tukumbukeni Ayah hii katika Qur’an kuhusiana na subra wakati wa mitihani.
[يَوْمَ يَأْتِ لاَ تَكَلَّمُ نَفْسٌ إِلاَّ بِإِذْنِهِ فَمِنْهُمْ شَقِيٌّ وَسَعِيدٌ[ “Na subiri, kwani Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wanao fanya wema.” [Hud: 115]

Je ni mayatima wangapi wanatakiwa kuwepo kama Omar, ni wangapi wapo lakini hawajaorodheshwa na wanatumiwa kutoka Syria, Iraq, Palestina, Afghanistan, Yemen na kwingineko? Tunawalingania Waislamu duniani kote kutumia njia zozote walizo nazo kunusuru na kufanyakazi ya kuishi chini ya Nidhamu ya Kisiasa ya Kiislamu na kujipatia nafasi miongoni mwa waliofaulu Kesho Akhera.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:10

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu