Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uchumi wa Kirasilimali wa Pakistan Unayumba Baina ya Akaunti ya Sasa ya Upungufu na Ziada, lakini Kamwe Hauleti Ustawi Halisi na Maendeleo

Habari:

Mshauri wa Waziri Mkuu juu ya Fedha na Mapato Dkt Abdul Hafeez Shaikh alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter mnamo Alhamisi 19 Novemba 2020, kwamba "serikali ya PTI imerithi wa akaunti ya sasa ya upungufu wa $19.2B, tumepunguza hadi $3B katika mwaka wa fedha uliopita na sasa ziada ya $1.2B ya mwaka huu pamoja na ziada ya nne mfululizo ya kila mwezi.”

Maoni:

PTI imekuwa ikidai kwamba uchumi wa Pakistan uko katika hali mbaya haswa kwa sababu ya upungufu mkubwa wa akaunti ya sasa, uliorithi serikali zilizopita. Kwa bahati mbaya, licha ya idadi kubwa ya watu na maliasili nyingi, nyenzo pembejeo nyingi kwa viwanda pamoja na kilimo huagizwa kutoka ng'ambo, ambapo inasababisha viwango vikubwa vya uagizaji na nakisi ya akaunti ya sasa. Utawala wa PTI uliuendea mpango wa IMF mnamo 2019, ambao unaeleza kushuka kwa thamani ya Rupia, ili dolari iwe ghali na watu wakate tamaa kuagiza bidhaa. Wakati huo huo, kwa maagizo ya IMF, kiwango cha riba kiliongezeka hadi zaidi ya asilimia 13, wakati bei za nishati pia ziliongezeka, na kuongeza gharama ya kufanya biashara. Hatua hizi zilisababisha kubanwa sana kwa shughuli za kiuchumi, ikiburuta Pato la Taifa chini kutoka asilimia 5.84 hadi asilimia 0.99 kwa mwaka mmoja tu. Sasa kwa sababu ya sera hizi nakisi ya akaunti ya sasa sio tu ilipungua, ilikuwa ziada.

Walakini, ziada hii inanufaisha IMF pekee, pamoja na wakopeshaji wa kimataifa na wa ndani, kwani inahakikisha kurudi kwa maslahi na viwango asili kwa wakati. Malipo yanayofuatana na matakwa yao, ni kwa gharama ya kusimamisha magurudumu ya uchumi na kusababisha umasikini mkali kwa mtu wa kawaida. Sasa, kwa kuwa nakisi ya akaunti ya sasa imemakinika, serikali itazingatia kuongeza ukuaji, ambao pasi na budi unaongeza uagizaji, kwani Pakistan haitengezi nyingi ya nyezo pembejeo ndani ya nchi. Kwa hivyo katika miezi ijayo, tunaweza kuona ongezeko la Pato la Taifa, lakini pamoja na kuongezeka kwa nakisi ya akaunti ya sasa pia. Jambo hili la mzunguko limekuwa likiendelea kwa miongo kadhaa. Ni mzunguko unaofahamika kwa uchungu wa miaka ya uzalishaji, ambao huongeza upungufu wa akaunti ya sasa, ikifuatiwa na miaka ya kusinyaa, ambayo inapunguza nakisi ya akaunti ya sasa. Kwa hivyo Pakistan imekuwa ikicheza kati ya nakisi na ziada, lakini kamwe haisongi mbele.

Chini ya mfumo wa kiuchumi wa kirasilimali, Pakistan kamwe haitawahi kuwa nguvu ya kiuchumi, licha ya kuwa na ardhi ya kutosha, idadi ya watu, maliasili na kilimo. Chini ya usimamizi wa IMF, mfumo wa kiuchumi wa kirasilimali hufanya kazi kuhakikisha manufaa kwa warasilimali wakubwa wa ndani na wa kimataifa. Huku kukiwa na ongezeko kwa gharama na ushuru wa kawi, kamwe hatutawahi kuona mwamko wa kweli wa kiuchumi kwa pamoja. Badala yake, ustawi utakuwa tu kwa kikundi kidogo cha warasilimali, ambao wana makubaliano maalum kwa sekta zao za biashara, na vilevile haki za umiliki.

Pakistan inahitaji sana nidhamu ya kiuchumi wa Uislamu. Nidhamu ya kiuchumi ya Uislamu hukomesha riba, ukiwalazimisha wamiliki wa mitaji kuwekeza moja kwa moja katika miradi ya kiuchumi. Uislamu unaunganisha sarafu kwa dhahabu na fedha, na kumaliza utumwa wa dolari. Uislamu unatangaza rasilimali za kawi na madini kama mali ya umma, kwa hivyo uchumi hupokea pembejeo muhimu kwa bei rahisi. Uislamu hukomesha ushuru wa mapato, ushuru wa jumla wa mauzo na ushuru mwingine wowote ambao hautokani na Uislamu. Mazingira haya ya kiuchumi yatawezesha uzalishaji wa idadi kubwa ya nyenzo pembejeo, na kupunguza utegemezi kwa uagizaji wake kwa kiasi kikubwa, na kuongeza ukakamavu wetu wa kiuchumi. Mfumo wa sasa wa kikafiri kamwe hautatabikisha Uislamu, kwa hivyo yote haya yanaweza kutabikishwa tu baada ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume pekee.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Shaikh
Naibu wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 28 Novemba 2020 23:15

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu