Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wafanyi Biashara wa Silaha wa Uingereza Hawana Tabia Njema na Ni Wanafiki! Ni Nani Aliyejua?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kati ya 2011 - 2020, Uingereza ilizipa leseni za silaha zenye kugharimu £16.8 bilioni nchi zinazokashifiwa na Freedom House, kundi la kutetea haki za binadamu linalofadhiliwa na serikali ya Amerika.

Kati ya nchi 53 zinazokashifiwa kuwa na rekodi mbaya ya haki za kisiasa na za binadamu zilizo katika orodha ya kundi hilo, Uingereza uliziuzia silaha na zana za kijeshi nchi 39.

Wapokeaji mashuhuri ni pamoja na Libya, ambayo ilipokea bunduki za kushambulia, vifaa vya gari la jeshi na risasi zenye thamani ya Pauni 9.3 milioni. Wiki iliyopita ilikuwa ndio angazo la mazungumzo ya amani ya kimataifa kuleta utulivu nchi ambayo vikundi vyenye silaha na dola za kigeni zinashindania ushawishi.

Uchambuzi zaidi wa shirika lenye makao yake London la Kampeni Dhidi ya Biashara ya Silaha (CAAT) uligundua kuwa pauni bilioni 11.8 za silaha zilikuwa zimeidhinishwa na serikali ya Uingereza wakati huo huo kwa orodha ya Afisi ya Mambo ya Nje ya "nchi zenye kuzipa kipaumbele haki za binadamu". Thuluthi mbili ya nchi hizi - 21 kati ya 30 - kwenye orodha ya serikali ya Uingereza ya serikali za ukandamizaji zilikuwa zimepokea zana za kijeshi za Uingereza.

Idara ya Biashara ya Kimataifa pia imeyatambulisha mataifa tisa kama "masoko ya msingi" kwa mauzo ya nje ya silaha ambayo makundi yanasema yanahatia ya ukiukaji mwingi wa haki za binadamu, yakiwemo Misri, Bahrain, Qatar, Saudi Arabia, Thailand na Uturuki.

Serikali ya Uingereza tayari imekiri kwamba muungano unaoongozwa na Saudi Arabia umeshambulia Yemen kwa kutumia silaha zilizotengenezwa na kampuni za Uingereza na Uingereza ikisambaza zaidi ya nusu ya ndege za kivita zinazotumiwa na ufalme  huo wa Mashariki ya Kati kwa uvamizi wake wa mabomu.

"Mahali popote panapokuwa na ukandamizaji na mzozo daima kutakuweko na kampuni za silaha zinazojaribu kufaidika kutokana na hali hiyo, na kushawishi serikali kuwasaidia kufanya hivyo," alisema Andrew Smith wa CAAT. “Mauzo mengi haya yanaenda kwa tawala za kiimla, kidikteta na tawala zinazokiuka haki za binadamu. Hazijatokea kwa bahati mbaya. Hakuna hata moja katika mauzo haya ya silaha ambayo yangewezekana bila msaada wa moja kwa moja wa Boris Johnson na wenzake," aliongeza Smith. (Chanzo: The Guardian)

Maoni:

Bila msaada wa serikali za Magharibi, tawala za ukandamizaji na za kidikteta za ulimwengu hazingeweza kubakia. Wao ni wakala wa sera za wakoloni ambazo serikali za "ulimwengu huru" zinafanya dhidi ya watu wengi wa sayari hii. Kwa kweli haishangazi kwamba tabia ya serikali za Magharibi ni mbaya kiasi hiki, kwani wao wenyewe ni mawakala wa mashirika yenye nguvu na vikundi vyao vya ushawishi, ambao kati yao ni kampuni zinazoshughulikia silaha. Urasilimali umejengwa juu ya itikadi ya ubinafsi ya kisekula ambayo inaruhusu wafuasi wake kuitazama fursa yoyote kuipatiliza kama mchezo mzuri, bila kujali mazingatio ya kimaadili au mateso ambayo watasababisha. Uingereza ni nchi ile ile yenye mzinzi na muongo wa kawaida kama waziri mkuu wake, ambaye alikataa kumkemea Waziri wake wa Afya, ambaye pia anatuhumiwa kwa kudanganya, ambaye yeye mwenyewe pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Pritti Patel, wamepelekwa kwa afisi kuu ya kupambana na udanganyifu kwa uwezekano wa biashara fisadi katika kupeana kandarasi kubwa za kupeleka visambaza hewa na PPE muhimu (vifaa vya kinga binafsi) kwa wafanyikazi wa hospitali.

Hawa ni watu wafisadi zaidi duniani ambao wanapeleka silaha kwa madikteta waovu zaidi duniani ili kutekeleza vita kwa ajili ya pato lao la kibinafsi.

Mfumo unaovumilia na kuidhinisha ufisadi kama huu haustahiki kuzingatiwa na mtu yeyote, achilia mbali Waislamu walio na hamu ya haki na uadilifu zitawale. Mfumo wa sasa wa kiulimwengu wa kidemokrasia ndio mzizi wa udhalimu katika sehemu kubwa ya ulimwengu.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), amesema,

«يُحْشَرُ الْمُتَكَبِّرُونَ الْجَبَّارُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِي صُوَرِ الذَّرِّ يَطَؤُهُمُ النَّاسُ لِهَوَانِهِمْ عَلَى اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ»

“Wenye kiburi na majabari watakusanywa Siku ya Kiyama kwa sura za tembe ndogo ndogo. Watu watawakanyaga kwa sababu ya udhalilifu wao kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Yahya Nisbet

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu