Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Janga la Maambukizi ya COVID-19 – Kipimo kwa Serikali katika Kuhakikisha Maisha Mazuri ya Raia Wake

(Imetafsiriwa)

Habari:

Leo ni tarehe 26 Juni 2021 na Malaysia imefungwa kabisa (Movement Control Order 3.0) kwa karibu mwezi sasa. Kufungwa huku kunahusisha marufuku ya jumla ya harakati za watu na mikusanyiko kote nchini. Misikiti imefungwa. Taasisi zote za elimu zimefungwa. Biashara ambazo sio muhimu zimefungwa. COVID-19 hakika imechukua mkondo mkali kwa kila mtu tangu serikali ilipoanza kuweka maagizo anuwai ya kudhibiti matembezi nchini. Wakati mmoja, polisi waliwasilisha kwa ufahari takwimu zao kwamba kiwango cha uhalifu nchini kilipungua kwa asilimia 46.7 wakati wa siku 84 za kwanza za Amri ya Udhibiti wa Matembezi (MCO). Leo, hii inapungua ikilinganishwa na kuongezeka kwa kuendelea kwa viwango vya wazimu, kupoteza kazi na athari zingine kadhaa za COVID-19 kwa jamii. Kwa kweli, imeripotiwa kuwa katika maeneo fulani, kiwango cha ujambazi kilionyesha ongezeko kubwa wakati wa vipindi vya MCO.

Maoni:

Tangu mwanzo wa janga hili, serikali ya Malaysia imetekeleza maagizo anuwai ya kudhibiti matembezi kulingana na kiwango cha maambukizo ya COVID-19. Hapo awali, watu kwa ujumla walikuwa wanaunga mkono sana sera hizo. Lakini, baada ya miaka 2 ya ubadilishaji MCO anuwai, hali ingali sio nzuri. Kwa kweli, kutoka kwa moja ya nchi zilizoonyesha viwango vya chini kabisa vya maambukizi ya COVID-19, Malaysia iliipiku India mwezi uliopita kwa maambukizo ya COVID-19 kwa kila milioni ya idadi ya watu. Cha kusikitisha, athari za MCOs kwa jamii hazionyeshwi tu na sauti zenye hasira za umma lakini pia na idadi halisi ya watu walioathiriwa. Utafiti wa hivi karibuni wa JobStreet umebaini kuwa hadi asilimia 20 ya wahojiwa wameachishwa kazi. Utafiti huo pia ulionyesha kwamba mtu mmoja kati ya watu watano wa Malaysia ambao hapo awali walikuwa wakifanya kazi wamepoteza kazi zao kutokana na janga hilo. Pia ulifichua kuwa zaidi ya milioni mbili ya watu wa Malaysia wanatarajiwa kuishia bila ya kazi ikiwa MCOs zitaendelea kutekelezwa. Janga hilo pia limeathiri hali ya akili ya idadi ya watu. Nambari ya usaidizi wa kisaikolojia ya kijamii inayoendeshwa na Wizara ya Afya na Mercy Malaysia imeongezeka mara mbili hadi sasa mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana. Asilimia 63.7 ya wanaopiga simu walihitaji msaada wa kihemko kutokana na kuhisi kuwa na msongo wa mawazo, hofu, wasiwasi, huzuni, kutokuwa na tumaini na unyonge kwa sababu ya kutokuwa na uhakika juu ya siku zijazo. Hali mbaya ya kihemko pia inaonekana katika ongezeko la kiwango cha kujiua kati ya idadi ya watu wakati wa MCO.

Kwa kweli, janga hili limeathiri sana Malaysia na ulimwengu wote. Janga hili linaondoa utoshelevu wa wanadamu wa  ulimwengu huu na kama Mwislamu, tunajua kwamba hii ni aina ya mtihani wa Mwenyezi Mungu (swt) kwa waja wake. Mtihani humaanisha majibu. Na ni aina ya jibu hili ambalo litahukumiwa na Mwenyezi Mungu (swt) Siku ya Kiyama. Kwa mtihani huu muhimu, wale walio madarakani wanabeba mzigo mkubwa zaidi kwenye mabega yao. Viongozi wa Malaysia hawajawahi kihakika kuufanya Uislamu kuwa msingi wa kufanya maamuzi yao na kuunda sera zao. Kwa hivyo, haitarajiwi kuwa Uislamu utacheza dori kubwa katika sera zozote za serikali zinazohusiana na kushughulikia janga hili. Na hili sio mbali na ukweli. Kwa kufanya uadilifu kwa serikali, hatua za kuchochea uchumi na msaada wa kijamii kwa makundi yaliyo hatarini yametekelezwa. Lakini, juhudi hizi, pamoja na utekelezaji wake wote wa kimatata, hailingani na idadi mbaya iliyowasilishwa hapo awali. Kwa sababu ya kuzingatia uchumi, kufungwa kwa misikiti, kwa mfano, inaonekana kuwa ya maana ikilinganishwa na kufungwa kwa vituo vya ununuzi. Kutegemea kupita kiasi chanjo za kigeni, polepole na kutoridhika katika kutengeza chanjo nchini na kiwango cha chini cha chanjo kwa idadi ya watu huonyesha wazi udhaifu wa serikali - ukosefu wa wasiwasi na juhudi katika kutafuta tiba ya janga hili na kujiruhusu kutishiwa na kampuni za dawa za kimataifa na Magharibi. Na ulegevu wa serikali katika kuruhusu utumiaji wa dawa salama zdhidi ya virusi, ambazo zinaweza kuokoa maisha, licha ya shinikizo kutoka kwa wataalamu wa matibabu ni jambo la kusikitisha sana. Maswala haya ni ncha tu ya mlima wa barafu na leo, ukosoaji dhidi ya sera za serikali katika kushughulikia COVID-19 ni kubwa mno.

Kuna wale ambao watakaoitetea serikali kwa kusema kwamba yale ambayo viongozi wanayafanya ni kama ya 'Kiislamu' kama wanaweza. Kuna tofauti kubwa. Uongozi wa kweli wa Kiislamu, Khilafah, utashughulikia janga hili kuhakikisha ustawi wa Umma kama moja ya majukumu yake katika kutimiza amri za Mwenyezi Mungu (swt). Uislamu kama mfumo utakuwa ndio msingi wa maamuzi na sera zote. Uongozi huu unabeba jukumu la kuuokoa Ummah kutoka kwa janga hili, badala ya mara kwa mara kuunasa Ummah katika vifungo na mifadhaiko. Ummah unajua kwamba janga hili linafichua uovu wa utawala wa kisekula, wa kirasilimali. Ummah unajua kwamba uongozi wenye ikhlasi, mkweli, uwajibikaji, busara, uongozi unaomcha Mwenyezi Mungu utaweza kuwaokoa kutoka mikononi mwa janga hili. Uongozi kwa huo tutapata tu katika Khilafah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Mohammad – Malaysia

#Covid19    #Korona     كورونا#

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu