Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Imran Khan Anajaribu Kuficha Utumwa Wake wa Kisiasa na Kifikra kwa Magharibi kupitia Kuwathamini Waislamu wa Afghanistan

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri Mkuu Imran Khan mnamo Jumatatu, 16 Agosti 2021, alizindua Mtaala Mmoja wa Kitaifa katika sherehe jijini Islamabad. Alizungumza kuhusu jinsi ulazimishaji wa thaqafa ni sawa na 'utumwa wa akili," akisema kwamba Waafghan walikuwa "wamevunja pingu za utumwa." Maoni yake yamejiri huku Taliban ikichukua udhibiti wa Afghanistan, baada ya siku za kadhaa kusogea kwa haraka nchini. "Unapopata elimu ya kati ya Kiingereza, unachukua thaqafa nzima na ni hasara kubwa kwa sababu unakuwa mtumwa wa thaqafa hiyo," alisema.

Maoni:

Tangu kustaafu kwake kutoka kwa kriketi ya kimataifa mnamo 1992, na haswa tangu alipojiunga na siasa mnamo 1996, Imran Khan amekuwa akijionesha kama mtu aliye angazwa kikweli, ambaye anaelewa thaqafa ya Kimagharibi, lakini hajapagawishwa wala kutishika nayo, kwa hivyo hazingatii watu wake kuwa duni kuliko Wamagharibi. Alikosoa vikali kuasisiwa kwa laini ya usambazaji ya NATO nchini Pakistan na kuiunga mkono Taliban ya Afghanistan kwa kusema kuwa njia yao ni njia ya haki. Alisisitiza kwamba ataitoa Pakistan kutoka kwa muungano na Amerika, akifuata sera huru ya kigeni. Alimlaani Nawaz Sharif kwa ukaribu wake na Modi na kama msaliti kwa njia ya Kashmir. Alionya juu ya hatari kubwa za IMF na Benki ya Dunia kwa uchumi. Hata alidai kwamba ataifanya Pakistan kuwa dola kama Madinah iliyoanzishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Kwa hivyo, alijionyesha kama mtu aliyeifichua pakubwa elimu ya Kimagharibi na akazama sana ndani ya mazingira ya kipote cha wasomi wa Kimagharibi, lakini akiwa si mwenye kuathiriwa kabisa nacho, akibakia wa upande wa Mashariki na mwaminifu kwa watu wake.

Lakini, wakati Imran Khan alikuwa Waziri Mkuu wa Pakistan, aligeuza mgongo wake kwa kile alichokisema hapo awali. Alizidisha ushirikiano na Amerika, akawezesha mazungumzo na Taliban ili kulinda ushawishi wa Amerika baada ya kujiondoa na kudumisha laini za usambazaji hewani na ardhi hadi sasa. Kwa agizo la Amerika, alizuia Jeshi la Pakistan wakati Modi alipoiunganisha kwa nguvu Kashmir mnamo Agosti 2019, hata kufikia hatua zaidi ya kutangaza kuwa mtu yeyote anayevuka LoC kwa ajili ya Jihad, yeye ni msaliti. Badala ya kuikomboa Kashmir Iliyokaliwa kama Azad (iliyokombolewa) Kashmir ilivyokuwa, kwa kupigana, alielekeza njia ya Kashmir kwa agizo la kimataifa na mlezi wake Umoja wa Mataifa, ambao uliingilia kati mnamo 1948 kuzuia ukombozi wa Kashmir Iliyokaliwa hapo awali. Kwa IMF na Benki ya Dunia, Imran Khan ameharibu uchumi kwa kufuata kila agizo lao. Kuhusu Uislamu, amepuuza wito wa kumfukuza balozi wa Ufaransa baada ya Macron kuunga mkono kushambuliwa kwa heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na amewapa maliberali uhuru wa kuichafua jamii na ufisadi wao. Kwa hivyo, Imran Khan anatenda haswa kulingana na fikra aliyoibeba ya thaqafa yake ya Kimagharibi na ushawishi wa kisiasa unaotawala wa kipote cha wasomi wa Kimagharibi juu yake. Hakika bado hajavunja pingu za utumwa wa Magharibi.

Kwa sasa, baada ya kuanguka kwa Kabul, Amerika imekuwa kioja katika ulimwengu na vilevile vibaraka wake, akiwemo Imran Khan, wanajaribu kuokoa sura yake. Kwa hivyo kusema kwake kwamba Waafghan walikuwa "wamevunja pingu za utumwa" ni kuifinika tu aibu ya serikali zake mbele ya Waislamu wa Pakistan, wanapofurahi kushindwa kwa Amerika nchini Afghanistan. Hakika, yeye mwenyewe ndiye mfano bora wa utumwa wa kisiasa na kifikra wa Magharibi. Kwa kweli, Waislamu lazima wajitahidi kwa ajili ya Khilafah kwa Njia ya Utume ambayo itatabikisha Uislamu katika nyanja zote za maisha ikiwemo elimu. Hapo pekee ndipo tutakuwa na watawala ambao hawatakuwa watumwa wa Magharibi, ikinyanyuka na kuwa uongozi wa kifikra na kisiasa wa Kiislamu kwa ulimwengu mzima, na kuongoza ulimwengu kuelekea ustawi na ufanisi wa maisha yote, ya Dunia na Akhera. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

]قُلۡ يٰۤاَيُّهَا الۡكٰفِرُوۡنَۙ‏، لَاۤ اَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُوۡنَۙ]

“Sema: Enyi makafiri! Siabudu mnacho kiabudu.” [Surah Al-Kafirun 109:1-2]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Shaikh
Naibu Msemaji Rasmi Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

#Afghanistan    #Afganistan   أفغانستان#

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu