Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kikosi cha Mauaji cha Polisi Hupata Baraka za Tawala za Kisekula za Kibepari.

Habari:

Tarehe 21 Agosti 2021, tovuti ya gazeti la The Standard lilichapisha habari: “Polisi Wageuka kuwa Majambazi? IPOA sasa kuchunguza vifo 105.” Habari hii iliangazia kushamiri kwa visa ya ukatili wa maafisa wa polisi unaopelekea raia wengi kuwa walemavu hata wengine kukumbwa na vifo, ukatili huo kwa sasa umefika katika viwango vya kutamausha. Ikaendelea kusema kwamba “Kenya imesajili tarakimu za juu za raia waliofariki au kuachwa kuwa vilema wakiwa ndani ya seli za polisi. Takwimu kutoka Mamlaka huru ya uchunguzi wa matendo ya polisi (IPOA) zinaonesha kwamba kati ya mwezi Januari na Juni mwaka huu kesi za malalamishi 1324 ziliwasilishwa. Kati ya kesi hizi 105 ni madai ya vifo na majeruhi mabaya. Takwimu zinaonesha kuwa watu 21 wamekufa wakiwa ndani ya seli za polisi kwa kipindi cha miezi siti iliopita huku 55 wakifariki dunia kwa sababu ya kupigwa na polisi. Visa 15 vya kufyatuliwa risasi raia na kusababisha majeruhi pia vimeripotiwa huku visa 12 vya watu kupotezwa pamoja na visa viwili vinavyotokamana na ufyatuaji risasi kinyume cha sheria.

Maoni:

Ukatili unaofanywa na kikosi cha polisi umeanza kuonekanwa katika kipindi ambacho nchi  ilikuwa chini ya ukoloni wa Muingereza. Chini ya utawala huo wa kikoloni, polisi walikuwa na dori ya kulinda maslahi ya utawala. Haikuwa kazi ya polisi ni kulinda usalama na maslahi ya raia kwa ujumla. Serikali ya Uingereza ilipiga vita vugu vugu la Mau Mau kwa kuwafungia ndani ya makambi takriban Wakenya milioni na wakawa polisi wa kikoloni wanazunguka vijijini huku wakitekeleza mauaji ya kimfumo.

Hulka hii ya ukatili baadaye ikapenya kwenye viongozi waliokuja baada ya ukoloni ambao nao walitumia vikosi vya jeshi la polisi kulinda maslahi yao. Rais wa kwanza wa Kenya  Jomo Kenyatta, akatumia polisi kunyamazisha wakosoaji wa sera zake. Mfano wa haya ni yale mauaji ya halaiki ya Kisumu (Kisumu Massacre) mwaka 1969 ambapo polisi walivyatulia risasi halaiki ya watu waliokuwa wameandamana kupinga ziara ya rais Kenyatta. Kwenye purukushani hiyo takriban watu 11 waliuwawa huku mamia wakijeruhiwa. Mrithi wake Daniel Arap Moi, naye akatumia maafisa wa polisi kama zana za ukandamizaji na utekaji nyara kuwatia vizuizini na kuwatesa wapinzani wake wa Kisiasa. Jamii ya Kiislamu imekuwa ikilalamikia suala la kuuwawa kwa vijana wa Kiislamu kiholela holela na kupotezwa ikiaminika yote haya kutekelezwa na vikosi vya polisi.

Mchakato wa kuajiri polisi umegubikwa na Ufisadi, upendeleo, ukabila na utovu wa nidhamu ya kitaaluma yote haya yakichangia ukatili huu. Mbali na usawa wa kiwiliwili, vigezo vya busara ya akili, hisia zao havitiliwi maanani. Ufisadi wa polisi umechangia shida kubwa za kimfumo katika idara zote za vikosi vya polisi uliosababisha kutokuweko kwa misingi ya uwiano (checks nd balances) na taasisi dhaifu hivyo inafanya kuwa vigumu kuwawajibisha kwa matendo yao.

Ukatili wa polisi haushuhudiwi tu Kenya bali ni wenye kutapakaa barani Afrika na Ulimwengu kwa ujumla. Katika mataifa ya Kimagharibi ya Kibepari ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi yamekuwa ni masuala ya kawaida yanayotukia mara kwa mara kwa miongo na hata yamekuwa ni sehemu ya maisha. Chini ya mfumo wa Kisekula wa Kibepari ambao silaha yao zaidi ni mateso na ukatili ndio polisi na vikosi vyote vya usalama haviko katika kulinda maisha ya watu wala mali zao.

Katika Uislamu, kuwatesa watu ni kitendo kilichoharamishwa na afisa yeyote wa polisi atakayepatikana na hatia ya kumjeruhi na kumtesa raia yeyote awe Muislamu ama asiyekuwa Muislamu atawajibishwa kwa kitendo chake hicho na kuchukuliwa hatua stahiki. Na ni ndani ya Khilafah Raashidah pekee kwa mfumo wa Utume itakayosimamishwa katika mojawapo ya nchi za Kiislamu, ndio jeshi la polisi litakuwa likifanya kazi yake kwa mujibu wa sheria nayo ni kuhakakisha kuwa raia wanafuata sheria na hapo ndipo maisha na mali ya raia wote yatalindwa kikamilifu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut-Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu