Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Je, kuna Mfumo Wowote Utakaokomesha Kiburi cha Amerika katika Ulimwengu wa Kiislamu?
(Imetafsiriwa)

Habari:

Pentagon hivi karibuni ilitangaza kwamba shambulizi la droni za Amerika jijini Kabul mnamo tarehe 29 Agosti na kuua raia 10 wasio na hatia, wakiwemo wanawake na watoto, lilikuwa kosa la kujutia lakini halikuwa utovu wa nidhamu wala ukiukaji wa sheria. Shambulizi hilo lilitokea karibu na makaazi ya watu karibu na uwanja wa ndege wa Kabul. Gari linaloshukiwa kuwa la ISIS lilishambuliwa pamoja na watoto saba na wanafamilia wao, akiwemo Zemarai Ahmadi, mfanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali la Amerika ambaye pia alikuwa ametuma maombi ya kuomba hifadhi nchini Amerika. [Associated Press, Novemba 4]

Maoni:

Baada ya miaka 20 ya ugaidi nchini Afghanistan, Amerika ilifanya shambulizi la kigaidi hata katika hatua za mwisho za kuondoka kwa wanajeshi wake ambapo hakuna mtu aliyeuawa isipokuwa baba wa familia moja pamoja na wanafamilia wake - wahasiriwa wote walikuwa wanawake na watoto. Hata hivyo, Dola hiyo ya Kigaidi haikufanya tu jinai hiyo ya kinyama bali kwa mara nyingine tena imezikonga nyoyo na hisia za Waislamu huku Wizara ya Ulinzi ikitangaza kuwa haijakiuka sheria yoyote wakati wa shambulizi hilo.

Ulimwengu ulipaswa kutambua Dola hii ya Ugaidi ambayo inazungumzia utetezi wa haki za binadamu na haki za wanawake kwa ulimwengu, haswa kwa ulimwengu wa Kiislamu, wakati, sera yake ya msingi imejengwa juu ya ugaidi na mauaji ya halaiki. Mauaji ya Waamerika wenyeji milioni 100; shambulizi la mabomu katika jiji la Dresden la Ujerumani katika Vita vya Pili vya Dunia ambalo lilisababisha mauaji ya zaidi ya watu 200,000; mlipuko wa mabomu ya nyuklia ya Hiroshima na Nagasaki katika Vita vya Pili vya Ulimwengu, na kusababisha mauaji ya mara moja ya watu 220,000 na mamia ya maelfu wakisibiwa na maradhi mbalimbali baada ya janga hilo; Vita vya Amerika na Vietnam ambavyo viliwaacha Wavietnam wapatao milioni 3 wakiwa wamekufa wakati wa vita vya miaka 16 ambapo vikosi vya Amerika vilikuwa vikidondosha tani 500,000 za mabomu kwa mwaka – huku wakiteketeza wanadamu, wanyama na misitu pamoja na Napalm. Kando na hayo, mamilioni ya Waislamu, wakiwemo wanawake na watoto waliuawa katika vita vilivyoongozwa na Amerika nchini Afghanistan na Iraq, na kusababisha mamilioni ya watu kuhama makaazi yao. Amerika ilidondosha hata mama wa mabomu yote (MOAB) nchini Afghanistan. Kwa hivyo, uhalifu wa kibinadamu wa Dola hii ya Ugaidi umekuwa na/au utakuwa hauhesabiki.

Luteni Jenerali D. Said, Inspekta Jenerali wa Idara ya Jeshi la Wanahewa la Amerika aliyeongoza uchunguzi huo alisema: kwamba hakuona “ukiukaji wa sheria au sheria ya vita.” Bila aibu aliwaambia waandishi wa habari kwamba huo haukuwa mwenendo wa uhalifu au uzembe, lakini wale waliohusika moja kwa moja katika shambulizi hilo kihakika waliamini kuwa kulikuwa na tishio lililokaribia. Kwa hivyo, haipendekezi hatua yoyote ya kinidhamu.

Ikumbukwe tena kwamba, usaliti wa watawala wa ardhi za Kiislamu na mizozo ya kisiasa baina ya Waislamu ndio sababu kuu ya kuendelea kwa uhalifu wa Amerika na Magharibi kwa sababu Waislamu hawana dola ya Kiislamu iliyosimamishwa kupitia utiifu wa Waislamu wenye nguvu. - ambayo ingetabikisha Uislamu juu ya Ummah na kuubeba duniani kwa njia ya Dawah na Jihad. Zaidi ya hayo, sababu kwa nini Waislamu bado hawajairegesha Dola kama hiyo ya Kiislamu baada ya kuporomoka ni kwa sababu tu ya tafsiri yao isiyo sahihi ya lengo la maisha - Waislamu, badala ya kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt) kufaulu Ibtilah (mtihani) katika ulimwengu huu, wamekimbilia kwenye malengo ambayo mataifa mengine tayari yameyafuata, kama vile kupata raha katika ulimwengu huu ambayo ndio lengo kuu la maisha kwa ulimwengu wa Magharibi, au kutoroka kutoka kwa mateso na shida ambayo ndio lengo kuu la maisha linalofafanuliwa na dini nchini India na China. Mawazo hayo na madhumuni ya maisha yanaonekana kuweweka 'Wahn: kupenda dunia na kuchukia kifo' katika nyoyo za Waislamu, na kuwafanya wafuate nyayo za mataifa yaliyopita ambayo yalilaaniwa na kuadhibiwa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa sababu tu ya mawazo kama hayo.

Hiyo basi, ni lazima turudi kwenye fahamu zetu kama Ummah mmoja! Ni lazima tufafanue upya Kibla cha matumaini yetu; lazima tutafute matumaini kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) badala ya Amerika, China, Ulaya na Umoja wa Mataifa; lazima tutambue kutimiza wajibu wetu kwa kuzingatia Uislamu; ni lazima tuondoe Wahn kutoka katika nyoyo zetu; ni lazima tuwawajibishe watawala wetu wasaliti na waovu na hata kuwaondoa madarakani kwa kuzipindua serikali zao zisizokuwa za Kiislamu, na badala yake tusimamishe Dola ya Kiislamu (Khilafah) kwa njia ya Utume. Vyenginevyo, tutaona hali mbaya kama hii ikiendelea kwa sababu sisi Waislamu, kama Umma mmoja, tuna mkataba na Mwenyezi Mungu (swt), mkataba wa kutekeleza Uislamu, kuudhihirisha Uislamu juu ya dini zote na kuubeba Uislamu kwa wanadamu wote – kadhia nyeti ambayo kwa bahati mbaya tumeisahau hadi sasa.

 [هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]

“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [At-Tawba: 33]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Saifullah Mustanir
Mkurugenzi wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu