Jumatatu, 03 Jumada al-awwal 1443 | 2021/12/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wasiwasi Bandia wa Amerika kwa Watoto wa Bangladesh ni Sehemu ya Sera yake ya Kigeni ya Kikoloni

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mfumo wa Upendeleo Jumla (GSP) kwa bidhaa za Bangladesh katika soko la Amerika ulisimamishwa mnamo mwaka wa 2013. Mojawapo ya masharti ya kuregesha manufaa ya GSP ilikuwa kukomeshwa kwa ajira ya watoto. Lakini ajira ya watoto bado ingalipo nchini Bangladesh katika uzalishaji wa nguo, bidhaa za ngozi, samaki waliokaushwa na matofali, kulingana na ripoti ya Wizara ya Leba ya Amerika. Huko, leba hii inatajwa kuwa hatari na mbaya zaidi. Katika hali kama hiyo, hivi karibuni Wizara ya Mambo ya Nje imeiandikia barua Wizara ya Leba na Ajira, Biashara na Masuala ya Wanawake na Watoto kuchukua hatua zinazostahili kukomesha ajira hatarishi kwa watoto. Habari hii imejulikana kutoka kwa vyanzo husika.

Wizara ya Mambo ya Nje ilisema katika barua moja kwamba aina mbaya zaidi za ajira ya watoto itabidi zikomeshwe ili kuregesha manufaa ya GSP katika soko la Amerika katika siku zijazo. Kwa hiyo, hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Bangladesh kuhusu kutokomeza ajira kwa watoto katika sekta rasmi na zisizo rasmi zilizotajwa katika ripoti hiyo na maeneo yanayowezekana ya majadiliano na ushirikiano kati ya Bangladesh na Serikali ya Amerika kuhusu masuala haya zinapaswa kutambuliwa na kutumwa kwa Wizara ya Mambo ya Nje. (Chanzo: “The US GSP will not return unless child labor is abolished”, Bonikbarta.net, 2 Novemba 2021).

Maoni:

Je, kweli Amerika ya Wakoloni inajali kuhusu ustawi wa watoto nchini Bangladesh au nchi nyingine yoyote ya Kiislamu? Je, iko katika nafasi ya kudai maadili ya hali ya juu katika kukomesha ajira ya watoto na kuhakikisha maisha ya kawaida na yenye tija ya watoto wetu? Bado tunakumbuka jinsi vikwazo vya kiuchumi vya Amerika dhidi ya Iraq katika miaka ya 90 vilivyo angamiza maisha ya mamilioni ya watoto huko. Mnamo Mei 1996, Madeleine Albright, ambaye wakati huo alikuwa balozi wa Clinton wa Umoja wa Mataifa, alihojiwa na mwandishi wa habari wa 60 Minutes Lesley Stahl akizungumzia miaka ya vikwazo vya kiuchumi vilivyoongozwa na Amerika dhidi ya Iraq. Wakati Lesley aliposema kwamba watoto nusu milioni wamekufa nchini Iraqi ambao walikuwa watoto zaidi ya waliokufa huko Hiroshima, na iwapo bado Albright alifikiria kuwa hiyo ndio gharama yake inayostahili, Albright alijibu, "Nadhani hilo ni chaguo gumu sana, lakini gharama yake, tunadhani, gharama inastahili”. Kwa sababu ya vita vya wakala vya kinyama kati ya Amerika na Uingereza kwa ajili ya ushawishi wa kisiasa nchini Yemen, watoto 10,000 tayari wameuawa au kujeruhiwa tangu mapigano yalipoanza Machi 2015. Amerika inatumia uwezo wake Mashariki ya Kati kuanzisha vita kwa ajili ya mafanikio yake ya kijiografia. Ili kuunda upya hali ya kisiasa ya Yemen, ambayo imekuwa ngome imara ya Uingereza kwa zaidi ya miaka 170, inakubalika kwa Amerika kuua maelfu ya watoto na raia wasio na hatia. Ni shinikizo lipi ililotia kwa mchinjaji Assad ili kukomesha mateso ya watoto wa Ash-Sham ambao maisha yao yameharibiwa kabisa na utawala unaoungwa mkono na Amerika, na wengine wao wengi waliokimbia nchi hiyo kutafuta hifadhi katika nchi za Ulaya lakini wanaishi huko katika hali mbaya zaidi! Kwa hivyo mbinu hii ya huduma GSP ya kukomesha ajira ya watoto nchini Bangladesh si chochote ila ni chombo imara cha Amerika ya kikoloni cha kutia shinikizo kwa tawala vibaraka za Bangladesh kufikia ajenda yake ovu.

Kutokana na tawala za vibaraka za saliti za nchi za Kiislamu, Amerika ya kikoloni na waovu wengine ya kimagharibi yanaweza kucheza na maisha ya watoto wetu. Ili kuregesha heshima ya Ummah huu, ni lazima tuiregeshe Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume iliyoahidiwa bila kuchelewa tena.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir na
Imadul Amin
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu