Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Machafuko ya Afghanistan hayawezi Kutatuliwa kwa Kiasi chochote cha Pesa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 12 Oktoba 2021, BBC iliripoti kuhusu Mkutano wa G20 wa nchi zenye uchumi mkubwa ambao umeahidi kusaidia Afghanistan kwa msaada wa mabilioni ya dolari ili kuepusha janga kubwa. Chansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema kwamba hii itahitajika hivyo taifa hilo "halipaswi kuruhusiwa kuingia katika machafuko". Rais wa Amerika Joe Biden alisisitiza kuwa misaada inapaswa kutolewa kupitia mashirika huru ya kimataifa na sio moja kwa moja kwa Taliban. Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen amejitolea kutoa €1bn na Ujerumani inapanga kutoa Euro milioni 600.

Maoni:

Kinachopaswa kueleweka ni kwamba matamshi haya yanatoa hisia potofu ya uhalisia kwa kuwa Afghanistan ilikuwa kwa namna fulani katika hali ya usalama na utulivu zaidi kabla ya kuchukuliwa na utawala wa Taliban. Ukweli ni kwamba taifa hili liliporwa na kupokonywa uhuru wake na serikali hizo hizo na kujifanya kuwa na wasiwasi bandia na mustakabali wake ni jambo la kuchekesha. Viongozi wawa hawa wa G20 wote wana mkono katika kushirikiana na ufisadi na kifo huku mikataba ya silaha na hongo ikiwa ndio wasiwasi wao mkubwa pindi wanapopanga utabiri wa kiuchumi. Kumwaga pesa ndani ya serikali isio na miundo msingi na ruwaza sahihi ambayo hutumikia wanadamu kikweli ni pazia ya kuficha ukweli kwamba watu wanaohitaji pesa hizi zaidi kamwe hawatawahi kuona manufaa yake. Vivyo hivyo, wakati wageni hawa walipoingia kwa hila katika eneo hilo, maisha ya kijamii na mahitaji ya kimsingi hayakuwa na matokeo chanya.

Kamwe hakutakuwa na mwisho wa mateso yanayowakabili watu wa Afghanistan huku hukmu ya Mwenyezi Mungu (swt) ikisalia pembeni na mpangilio mpana wa mfumo wa utawala wa Qur'an na Sunnah ukipuuzwa.

Mwenyezi Mungu (swt) anabainisha tatizo la kuwachukulia maadui wa Mwenyezi Mungu (swt) kama wasaidizi katika Sura ya 60:1,

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِمْ بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُمْ مِنَ الْحَقِّ يُخْرِجُونَ الرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ أَنْ تُؤْمِنُوا بِاللَّهِ رَبِّكُمْ إِنْ كُنْتُمْ خَرَجْتُمْ جِهَادًا فِي سَبِيلِي وَابْتِغَاءَ مَرْضَاتِي تُسِرُّونَ إِلَيْهِمْ بِالْمَوَدَّةِ وَأَنَا أَعْلَمُ بِمَا أَخْفَيْتُمْ وَمَا أَعْلَنْتُمْ وَمَنْ يَفْعَلْهُ مِنْكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwisha ikataa haki iliyo kujieni, wakamfukuza Mtume na nyinyi kwa sababu mnamuamini Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu. Mnapotoka kwa ajili ya Jihadi katika Njia yangu na kutafuta radhi yangu, mnafanya urafiki nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayo yaficha na mnayo dhihirisha. Na mwenye kufanya hayo kati yenu basi ameipotea njia ya sawa.”

Kwa kutilia maanani muongozo huu wa wazi sisi kama mashahidi kwa wanadamu lazima tusikubali suluhisho lolote isipokuwa mfumo sahihi wa utawala wa Kiislamu kama ulivyotolewa mfano wa Mtume (saw). Hadi hili litimie, matatizo ya Ummah huu kamwe hayatakoma kuwepo licha ya matrilioni mengi ya dolari yanatolewa kwa viongozi wanaoshindwa kutii njia sahihi ya Uislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammed
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

              #Afghanistan                           #أفغانستان                                         #Afganistan           

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu