- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Ewe Mgeuzaji Nyoyo, Zigeuze Nyoyo Zao
(Imetafsiriwa)
Habari:
Serikali ya Pakistan imemchagua mkuu wa zamani wa shirika la kijasusi Asim Munir kama mkuu wake mpya wa jeshi, wadhifa ambao umeamuru kwa kiasi kikubwa utawala wa nchi hiyo ya Asia Kusini, yenye silaha za nyuklia huko nyuma. (Chanzo)
Maoni:
Pakistan tangu wakati wa kuzaliwa kwake imekuwa nchi muhimu sana kwa sababu ya eneo lake la kimkakati na watu wake jasiri, wanaopenda Uislamu. Tangu iibuke kama dola ya kinyuklia imekuwa mwiba kwa maadui zake wa wazi na waliojificha. Ijapokuwa Waingereza waliligawanya Bara Ndogo mara mbili na waziwazi walipendelea India, hawakuiachilia Pakistan na walihakikisha kwamba Dola hii mpya iliyozaliwa kamwe haitawahi kujisimamia yenyewe. Vikosi vya kijeshi vya India na Pakistan vilibakia chini ya amri ya maafisa wa Uingereza. Jenerali Messervy alikuwa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Pakistan, huku Field Marshal Auchinleck akiwa Kamanda Mkuu wa majeshi ya India na Pakistan. Messervy alichaguliwa na Muhammad Ali Jinnah na ni mfano wa utiifu wa kitaifa. Waislamu wa India walipata hasara upande wa maisha, heshima, mali na uaminifu. Kashmir ilikuwa moja ya hasara hizo na mnamo Oktoba 1947, watu wa kabila la Pashtun walikusanyika kwa ajili ya uhuru wa Kashmir. Messervy wakati huo alikuwa jijini London na kaimu Kiongozi Mkuu wa Majeshi (C in C) alikuwa Jenerali Gracy ambaye alipoamriwa na Bw. Jinnah kusaidia kuirudisha Kashmir, alikataa kutii. Field Marshal Auchinleck aliruka hadi Lahore na kumshawishi Jinnah kubatilisha agizo lake. Wakati huu aliandika dori za siku za baadaye za uhusiano wa serikali ya kijeshi na kiraia wa Pakistan na vuta ni kuvute hii inaendelea hadi sasa.
Wakuu wengi wenye majina ya Kiislamu na nyoyo na akili za kikoloni wameongoza jeshi la Pakistan katika miaka 75 iliyopita, wakipinga jukumu la heshima walilopewa na Mwenyezi Mungu (swt). Waislamu wa Afghanistan, Bangladesh, Kashmir na India ni majirani zetu na wanatapatapa wakihitaji msaada, wakati askari wetu wanatumwa kwenye misheni za Umoja wa Mataifa na mazoezi ya pamoja na nchi zinazokandamiza ndugu na dada zetu Waislamu. Tunaona jeshi letu linatoa ulinzi kwa watu wa China wanaofanya kazi Pakistan, wakiwachukua kama wasaidizi na marafiki, huku Waislamu wa Uyghur wakiteseka nchini China na haiwaonei huruma hata kidogo. Miungano yote jeshi la Pakistan inayoitazama haina hofu ya kuipoteza kwani wanajua jinsi gani walivyonaswa katika biashara hii, ambayo sio tu inahusisha mipaka bali ujenzi wa mali za kibinafsi pia.
Uchunguzi na ufuatiliaji wote wa uteuzi wa mkuu wa jeshi unahusisha manufaa ya wanasiasa na wanajeshi wenye uchu wa madaraka na unafuatiliwa kwa karibu na nchi za Magharibi. Jeshi la Pakistan lina nguvu, mafunzo na uwezo wa kusimama mbele ya adui jambo ambalo si tu kwamba litaleta ulinzi kwa Waislamu duniani kote bali pia watapendwa na kuheshimiwa kwa njia ya heshima. Njia ya Khalid bin Walid, shujaa, kamanda ambaye anakumbukwa kwa ushujaa wake, ushindi na mikakati yake ya vita, sio kwa visiwa alivyoviacha, na Khalid bin Walid (rh) alikuwa akipigana na kushinda chini ya ulinzi wa Khalifa Muislamu. Ni mifumo ya upatanifu ya Uislamu pekee chini ya kivuli cha Khalifa wetu mwongofu ndiyo italeta amani na utulivu kwa ulimwengu wa Kiislamu na kuwasilisha mfano wa Dola kwa ulimwengu mzima.
Mwenyezi Mungu azigeuze nyoyo za wenye uwezo wa kutoa Nusrah na awaunganishe na wenye nyoyo zinazomcha Mwenyezi Mungu pekee.
Abdullah b. Amr b. Al-‘As ameripoti kwamba alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema:
«إِنَّ قُلُوبَ بَنِي آدَمَ كُلَّهَا بَيْنَ إِصْبَعَيْنِ مِنْ أَصَابِعِ الرَّحْمَنِ كَقَلْبٍ وَاحِدٍ يُصَرِّفُهُ حَيْثُ يَشَاءُ»
“Hakika nyoyo za wana wa Adam ziko baina ya vidole viwili kati ya vidole vya Mola Mwenye Huruma, kama moyo mmoja. Huzigeuza kwa (mwelekeo) wowote aupendao.” Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema:
«اللَّهُمَّ مُصَرِّفَ الْقُلُوبِ صَرِّفْ قُلُوبَنَا عَلَى طَاعَتِكَ»
“Ewe Mwenyezi Mungu, Mgeuzaji nyoyo, zigeuze nyoyo zetu kwenye utiifu wako” (Sahih Muslim)
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan