Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ufisadi wa Kiutawala ni Matunda Maovu ya Itikikadi ya Kisekula ya Kiliberali

Habari:

Wawaniaji wa kiti cha urais Raila Odinga wa ODM na yule wa Muungano wa UDA naibu raisi William Ruto wanazunguka pembe zote za nchi katika kampeni zao za uchaguzi wa 2022 huku wawili hao wakiwaahidi wapiga kura: Kung’oa kabisa ufisadi! Akihutubia wajumbe takriban 500 huko Turkana, Odinga alisema; ‘tatizo kubwa linaloathiri Kenya ni ufisadi. Watu wamepora fedha za umma. Walipoingia serikalini mwanzoni walikuwa ni wembamba lakini sasa wamenona kama kupe’. Ruto naye kwa upande wake kwenye hadhira kadhaa amekuwa akishikilia kwamba punde tu akichaguliwa kuwa rais, serikali yake itang’oa kabisa tatizo hili sugu lililoota mizizi nchini Kenya.

Maoni:

Kenya inaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu wa 2022, tayari siasa zinaonekena kuteka hisia za umma. Matabaka mbalimbali ya watu wamekuwa wakijitosa kwenye mijadala ya kisiasa. Baadhi ya mijadala hasa ile ya waheshimiwa imegeuka na kuwa fujo na vurugu kama ilivyoshuhudiwa katika jumba la Agosti – bunge la Kenya pale wabunge walipozomeana na hata kupigana wakijadili kwenye mswada wa marekebisho ya vyama vya kisiasa. Kauli mbiu ya wanasiasa takriban wote ni kuondosha ufisadi na kujenga uchumi imara.

Mwaka huu wa uchaguzi mashindano katika kambi za kisiasa ni kati ya wale wanaoitwa kizazi cha watawala (Dynasty) dhidi ya Walalahoi (hustlers)” kauli mbiu hizi zinabuniwa ili jamii wasifikirie sababu msingi ambayo leo inawapelekea watu kuishi kwenye maisha ya dhiki na umasikini. Kila mwaniaji anadai kupigania kuondosha ufisadi katika asasi zote za serikali lakini kinaya ni kuwa imepita miaka hamsini sasa tokea uhuru bado hali ya kimaisha ya umma katika nyanja zote za kimaisha zinazidi kuwa mbaya na mbaya zaidi.

Kushutumiana na kutupiana lawama kwenye vita dhidi ya ufisadi kumekuwa ndio kikwazo kwenda kwenye ufanisi na ustawi wa kiuchumi. Ni muhimu kufahamu mwelekeo wa kikanuni unaohusiana na ufisadi kama ilivyo katika katiba: kuwa kosa lolote katika kifungu cha sehemu ya 39 hadi 44 na 47; b) Rushwa, c) wizi, d) Ufujwaji na ubadhirifu wa pesa za umma. E), utumizi mbaya wa afisi.

Kenya imeweka utaratibu maalum wa kisheria na taasisi za kupambana na ufisadi ambazo nazo zenyewe zimekuwa zikikumbwa na ufisadi. Juhudi za asasi hizi za kisheria ndio kwanza zimefanya mambo kuwa mabaya na magumu zaidi. Fauka ya hayo, aina zote za ufisadi chini ya kanuni zimevutia zaidi na kufanya ukubalike katika jamii. Jambo hili jipya la kawaida linahitaji kuchunguzwa na kuchambuliwa kwa kina kama limekuwa jambo la kimataifa!

Ufahamu wa kuhusu nini ufisadi kama ilivyo kwenye tawala nyingi zilizoko sasa hauko wazi bali hauelekei kuwashtaki watu binafsi. Ukosefu huu wa uwazi hufanya mtu binafsi kutatuliwa zaidi katika kufanya uhalifu. Pia, wasomi wa kisiasa wameunda "genge la mafia" ambalo hukiuka sheria na hakuna yeyote anayethubutu kulikemea juu ya kufanya uhalifu kama huo bila kuadhibiwa. Mianya hii kwenye ngazi za kisiasa na kisheria yanaufanya mfumo huu leo ushindwe kuangalia mambo ya watu.

Sheria hii ya kibinadamu haina ufahamu sahihi juu ya kitendo cha kheri na cha shari bali hauweki kipengele cha uroho hisia za kiroho kama msingi wa sharia ya nchi. Kukosekanwa kwa sifa ya kiroho ni suala la kimaumbile hasa ikizingatiwa kuwa huo ndio msingi wa itikadi ya kisekula unaomkana Mwenyezi Mungu muumba wa ulimwengu, mwanadamu na uhai kuwa Yeye ndiye mleta sheria. Fauka ya haya, kutofautiana kimawazo kwa wanadamu ndio kumefanya wanadamu leo duniani wakose kuarifisha maana halisi ya Ufisadi hivyo kujenga mazingira ya kupomoka kwa maadili.

Kwa hivyo sheria inahusisha ufisadi moja kwa moja na watu binafsi tuu huku ikiacha jamii kubakia mhanga, vilevile kuweka ubinafsi na kufungamanisha thamani ya ubinadamu kwa uzalishaji wa bidhaa na huduma anazo zalisha. Chini ya kibandiko cha uhuru wa kumiliki na uhuru wa kibinafsi mwanadamu amekuwa muovu tena wa kupatiliza akiangalia viti vya kisiasa kama njia moja wapo ya kujitajirisha na wala sio uwajibikaji.

Uislamu, mfumo unaotokamana na itikadi ambayo ni ya kiroho na kisiasa unaangalia ufisadi kikamilifu wala sio baadhi tu ya matendo. Yale matendo ambayo mfumo wa kibepari unayaangalia kama ufisadi, Uislamu unabaini matendo hayo asili ni natija ya ufisadi. Kiuhalisia ni kwamba ufisadi unatokamana na mfumo muovu ambao wenyewe una asasi za kuzalisha maovu. Mwenyezi Mungu SWT anasema katika Suratul Maida:

وَلْيَحْكُمْ أَهْلُ الْإِنجِيلِ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فِيهِ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ))

"Na wahukumu Watu wa Injili kwa yale aliyo teremsha Mwenyezi Mungu ndani yake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu." [Al-Maida 5:47]

Kwa ta’reef hii iliyo wazi ya ipi maana halisi ya ufisadi, Uislamu unapotabikishwa sheria zake hazitoki kwa yeyote yule ila kwa Mwenyezi Mungu (swt). Msingi wa Kisekula na mifumo yote ya kibinadamu ndio chanzo halisi cha ufisadi. Uislamu ni mfumo unaotokamana na Muumba wa Ulimwengu Mwanadamu na Maisha na unaambatana na maumbile ya mwanadamu hivyo huenda na wakati na maeneo.

Enyi wanafikra, uovu huu utaondoshwa na mfumo wa Uislamu pekee kwa kutabikishwa na serikali ya Khilafah. Enyi watu: mnaochukia maovu, fanyeni kazi ya kurudisha maisha ya Kiislamu kwani ndiyo yatakayo komboa wanadamu kutokana na aina zote za maovu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir na

Ali Omar Albeity

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu