Jumamosi, 15 Muharram 1444 | 2022/08/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mswada wa Khan wa Uhuru wa Maamuzi wa Benki Kuu ya Dola ya Pakistan Utaiwezesha IMF na Wakopeshaji wa Kimataifa Kutekeleza Wizi wa Mchana Peupe

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mswada mpya wa Khan unalenga kuifanya Benki Kuu ya Dola ya Pakistan (SBP) kuwa huru kimaamuzi na umelaaniwa na watu wengi. Waziri wa zamani wa fedha, Miftah Ismail alielezea mswada huo kama wenye kuibadilisha SBP kuwa "benki ya IMF". [aninews] Ismail pia alitangaza kuwa hatua hizo mpya zitaifanya SBP kuwa na nguvu zaidi kuliko bunge kwani "hakutakuwa na usimamizi wa sera ya uchumi na fedha". [thenews]

Maoni:

Ukosoaji wa Ismail ni halali na mengi ya madai yake yana manufaa. Uchunguzi wa haraka wa mswada huo unaonyesha kwamba kwa amri ya IMF, serikali ya Khan itapuuza kazi ya SBP kusaidia kazi ya maendeleo, kuzuia serikali za Pakistan kukopa kutoka kwa SBP na kukomesha jukumu la Bodi ya Fedha na Uratibu wa Fedha. [2] Hii ina maana kwamba serikali za Pakistan haziwezi kuitegemea SBP kusaidia shughuli za maendeleo kama vile miundombinu ya ujenzi, shule za serikali na hospitali na kazi nyingine kwa manufaa ya umma. Zaidi ya hayo, serikali za Pakistan zitalazimika kukopa kutoka benki za biashara kwa viwango vya juu vya riba ili kuziba mapengo ya nakisi ya fedha (na hivyo basi kuongeza deni la ndani), na serikali haitatumia tena udhibiti wa kuweka sera ya fedha kwa nchi. Kwa jumla, SBP itakoma kuhudumia mahitaji ya Pakistan na badala yake itazingatia sera huru ya fedha ambayo inalingana na mipango ya marekebisho ya kimuundo ya IMF (SAPs).

mipango ya marekebisho ya kimuundo (SAP) ya IMF inaendeshwa na Makubaliano ya Washington kwa lengo la pekee la upangiliaji upya wa uchumi wa nchi ili kukidhi mahitaji ya kilafi ya wakopeshaji fedha wa kimataifa. Kwa mfano, katika kipindi cha 2001 hadi 2020, Pakistan ilijisajili kwa SAPs 5 za IMF, ilikopa $113 bilioni na kurudisha katika kipindi kama hicho $118 bilioni kama rudisho la mkopo na riba. [ipr] Hata hivyo, licha ya malipo hayo makubwa, dhima za deni la nje la Pakistan ni $86 bilioni. Hii ni kwa sababu pesa zinazokopwa kutoka kwa wakopeshaji wa kimataifa kupitia IMF huenda katika kulipa madeni yaliyopo na hazirudishwi katika uchumi kama watu wengi wanavyofikiri.

Kuna shaka kidogo kwamba IMF SAPs imeunda upya uchumi wa Pakistan ili kutoa faida kubwa kwa wakopeshaji wa kimataifa. Hii inaeleza sababu ya ni kwa nini wakopeshaji wa kimataifa wako tayari kutoa mikopo kila wakati Pakistan inapokabiliwa na salio la nje la mgogoro wa malipo. Kito cha taji cha IMF ni kuifanya SBP kuwa huru kabisa kutoka kwa serikali za Pakistan, ili SBP iweze kuunda sera ya fedha itakayowawezesha wakopeshaji wa kimataifa kufyonza pesa zao (regesho la mkopo na riba) kwa gharama ya watu wa Pakistan, na hakuna yeyote inayeweza kuwazuia wakopeshaji wa kimataifa kutokana kwa uporaji wa mchana peupe. Kwa kweli, yule anayeitwa rafiki wa Pakistan Saudi Arabia aliufanya uanachama wa IMF kuwa sharti kwa mkopo mpya wa $3 bilioni.

Dori ya Bait-ul-Maal (Benki Kuu/Hazina ya Dola) katika Uislamu ni kulinda uchumi wa dola na kuhakikisha kwamba fedha zinapatikana ili zitumike kwa wananchi wa dola kama ilivyoainishwa na Shariah. Dola ya Khilafah ina uangalizi kamili wa jinsi fedha zinavyokusanywa na kutumika, na watu wanaweza kuihisabu dola. Uislamu unakataza wakopeshaji wa kimataifa kama vile IMF, WB, Paris Club, Benki ya Maendeleo ya Asia kutumia udhibiti wowote wa Bait-ul-Maal kupitia SAPs na masharti - achilia mbali kulipa mikopo yenye riba. Pindi Bait-ul-Maal inapofanya kazi pamoja na jamii ya Kiislamu yenye kutabikisha Uislamu kikamilifu, jamii hiyo huinuliwa katika ustawi na hadhi. Mfano wa Khilafah wa Rashida ni ushahidi wa jinsi Bait-ul-Maal ilivyotumikia jihad na sera za upanuzi za dola, na wakati huo huo kuinua viwango vya maisha vya raia wake. Khan anajigamba kuhusu kuunda upya dola ya Madina, lakini kivitendo haoni madhara yoyote katika kuisalimisha SBP kwa tai wa kimataifa kama vile IMF na wakopeshaji wao.

Fauka ya hayo, haoni aibu kujiandikisha kwa SAP ya IMF ambayo inamomonyoa uhuru wa uchumi wetu na kuwaweka watu kwenye utawala wa Magharibi. Lakini baya zaidi ya yote, Khan anajua kwamba kukopa zaidi kutaongeza tu dhima ya madeni yetu kwa nchi za Magharibi—hivi karibuni amelinganisha mlima wa deni la nje na usalama wa taifa—na kuwafanya Wapakistani kuwa watumwa wa taasisi za kirasilimali za Kimagharibi kwa vizazi vijavyo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Majeed Bhatti

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu