Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Dikteta Mmoja Ameondoka Mamlakani, Dikteta Mwengine Amewasili

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Januari 18, 2022, tovuti rasmi ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kazakhstan, Nursultan Nazarbayev, ilichapisha rufaa ya N. Nazarbayev, kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa maandamano makubwa nchini tangu Januari 2.

Katika rufaa yake, N. Nazarbayev alimhakikishia kila mmoja:

"Kujibu rufaa nyingi zilizoelekezwa kwangu, na kuhusiana na machapisho kwenye vyombo vya habari, ninawajulisha kwamba mnamo 2019 nilikabidhi mamlaka ya Rais kwa Kassym-Zhomart Tokayev na tangu wakati huo nimekuwa mstaafu, na sasa niko kwenye mapumziko yanayostahili katika mji mkuu wa Kazakhstan na sikuondoka kwenda popote.

Rais Kassym-Zhomart Tokayev ana mamlaka kamili. Yeye ndiye mwenyekiti wa Baraza la Usalama. Hivi karibuni, Rais huyo atachaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha Nur Otan.

Hiyo basi, hakuna mgongano au makabiliano katika kipote cha uongozi. Uvumi juu ya mada hii hauna msingi kabisa."

Maoni:

Hotuba ya N. Nazarbayev ni kama kujisalimisha kikamilifu. Kabla ya kuanza kwa maandamano makubwa nchini Kazakhstan, N. Nazarbayev alishiriki katika karibu matukio yote ya kisiasa nchini. Hata katika mkutano mkuu wa CIS mnamo Disemba 28, 2021 huko St. Petersburg, marais 2 wa Kazakhstan, wa zamani na wa sasa, walishiriki kwa wakati mmoja. Nani aliyemsikia rais wa zamani wa nchi, jinsi mkia unavyomfuata rais wa sasa na kushawishi maamuzi ya kisiasa?!

Nyuma mwishoni mwa miaka ya tisiini, N. Nazarbayev, akizungumza na waandishi wa habari, alisema kwa uwajibikaji kwamba jamaa zake hawatakuwa mamlakani, hakutakuwa na ufalme nchini, kwamba kila kitu kitakuwa, kama ilivyoandikwa katika Katiba ya nchi, na muda wake wa uongozi unaisha mwaka wa 2000. Lakini kama tunavyoona, N. Nazarbayev alivunja ahadi zake zote na kukaa mamlakani kwa zaidi ya miaka 30. Binti zake, wakwe, jamaa walikuwa mamlakani, na N. Nazarbayev yeye mwenyewe alitawala bila kikomo, hakutaka kuachana na mamlaka hadi, hatimaye, alipotakwa.

N. Nazarbayev hakuwepo kwa zaidi ya wiki 2 tangu mwanzo wa maandamano makali. Wakati huu, karibu wengi wa familia yake wakiwa kileleni mwa madaraka, kwa njia moja au nyingine, walipoteza nyadhifa zao. N. Nazarbayev alifukuzwa kutoka wadhifa wa mwenyekiti wa Baraza la Usalama na KZh Tokayev mwenyewe. Rais wa sasa wa nchi, Kassym-Zhormat Tokayev, anatoa sheria bila kuchoka na kufanya mabadiliko ya wafanyikazi katika maeneo yote.

Kuanzia mwanzo tu alipoingia madarakani, KZh Tokayev hakujiruhusu uhuru kama huo. Tangu kuanza kwa maandamano makali, idadi ya uteuzi mpya inaweza kusomwa kwenye tovuti rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Kazakhstan. Hii kawaida hufanywa baada ya rais mpya kuchukua madaraka, lakini hapa tulilazimika kungojea miaka 2 kwa mabadiliko mapya ya wafanyikazi. Mnamo Januari 11, KZh Tokayev alitoa amri juu ya muundo wa serikali mpya ya Jamhuri ya Kazakhstan. Mnamo Januari 19, alichukua nafasi ya waziri wa ulinzi wa nchi hiyo. Hii ina maana kwamba N. Nazarbayev hatimaye alistaafu kutoka kwa biashara na kupoteza nguvu zake.

Dhalimu mmoja ameondoka, dhalimu mwengine akachukua nafasi yake. Huu ndio uhalisia wa Waislamu wa Kazakhstan. Kwanza, Ukomunisti, na kisha Urasilimali, ulichangia kuwatenga Waislamu wa Kazakhstan na ufahamu wa Uislamu, na kwa hiyo wakawa mateka wa mawazo ya kisekula. Tofauti na jamhuri za jirani, Waislamu wa Kazakhstan mara nyingi huenda kwenye maandamano na kudai mageuzi. Hivyo ndivyo juhudi zao zote zinavyozunguka katika mawazo ya usekula. Na mwishowe, hupoteza kila wakati, kama ilivyo pia wakati huu.

Wakoloni kwa ustadi wanawapurukusha Waislamu kutokana na mabadiliko ya kimsingi. Mfumo wa serikali uliobuniwa na mwanadamu, ambao ulilazimishwa na wakoloni, ndio msingi wa shida na matatizo yote ya nyumbani, katika jamii, serikalini na kote ulimwenguni. Waislamu wanalazimishwa kimakusudi kuingia katika masuluhusho yenye manufaa tu kwa madhalimu na wakoloni wenye nguvu pekee, na masuluhisho haya husababisha matatizo mapya.

Suluhisho pekee sahihi, kwa Waislamu wa Kazakhstan na kwa Waislamu wa ulimwengu mzima, ni Uislamu. Ulimwengu ulipochoka kutokana na dhulma ya ujinga na desturi, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliteremsha Uislamu kuwa suluhisho la matatizo ya wanadamu. Leo tuko katika hali hiyo hiyo, ambapo ulimwengu unatawaliwa na dhulma, huku mwenye nguvu ndiye mwenye haki, na mnyonge, japo ana haki, anabaki bila haki.

Uislamu kama mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu, jamii na serikali ndio uamuzi pekee sahihi. Na kwa hiyo, suluhisho litakuwa ni kufanya kazi ya kuhuisha Dola ya Khilafah Rashida ya Pili. Hapo ndipo Waislamu wa Kazakhstan na ulimwengu mzima watapata amani na ufanisi, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyoahidi katika Kitabu chake Kitukufu:

 (وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [24:55].

 Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu