Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Dori ya Dini katika Enzi ya Mfumo wa Kirasilimali wa Kisekula

Habari:

       Kasisi Ssebagala alitoa maagizo yafuatayo mnamo Jumamosi katika Kanisa la St Paul Kanjuki katika Wilayah ya Kayunga alipokuwa akitoa mkono wa kuwaaga Wakristo kabla kustaafu kwake mwaka huu. “Walimu wakuu wote, nataka kuwaambia kwamba hatutoruhusu wasichana wenye mimba au wanaonyonyesha darasani. Wasichana wote wakija, fanyeni ukaguzi wa kawaida wa kimatibabu ili wale watakaopatikana kuwa wana mimba waweze kurudishwa ili wakazae watarudi baada ya kujifungua.” Kwa kuongezea, alisema, “Chukulia mtu anayesema kuwa wanaonyonyesha waruhusiwe darasani. La, hili hatutolikubali kwa sababu shule zetu zilianzishwa kwa ajili ya kutoa maarifa bali hata pia kuwapa watoto nidhamu. Inawezekanaje kwa mwalimu kuwa anafundisha ilhali msichana anampa matiti mwanawe?”

Katika kujibu matamshi yaliyotolewa na kasisi, Waziri wa Ndani wa Elimu ya Juu, John Chrysestom Muyingo alisema, “Inaonekana rafiki yangu kasisi hajui msimamo wa serikali. Nitakwenda katika afisi yake na kuzungumza naye. Najua ataelewa ufafanuzi wangu na kubadilisha msimamo wake.”  (The East African, Jumatatu, 10/01/2022)

Maoni:

Ni jambo la kutiwa shaka kwa vyombo vya habari kupatiliza matamshi yaliyotolewa na Kasisi. Kwa upande mwingine, kujitia upofu kwa uhakika wa dori ya dini katika enzi ya mfumo wa kirasilimali wa kisekula kuwa ni ya kushikamana kiushirikiano. Katika hali ambayo dini imetengwa na kuwa pembezoni pale kunapohusiana na masuala ya uongozi na utawala, lakini hutumika pale ambapo uwiano wa kijamii unapotishiwa. Hivyo basi, dini inatumika kama zana na wale walioko mamlakani ili kutimiza ajenda zao ovu kupindukia.

Watu wengi wameikumbatia dini kwa muktadha wa nami nionekane pia ni mtu wa dini. Mtazamo ambao unashawishiwa na maadili ya kirasilimali ya kisekula ambayo yanachukia dini na matukufu yake. Kwa hiyo, watu wengi wakijumuisha kipote cha wachache watawala hudhihirisha hisia za kidini pale ambapo huona ni muafaka kufanya hivyo, lakini wanabakia kuwa watumwa na wanaoabudu mungu wa kidemokrasia. Mungu ambaye kuwepo kwake kumetokamana na akili zao zenye kikomo! Haishangazi kuwa viongozi wa ‘kidini’ wa  leo au zamani ima Waislamu au Wakristo nk. wanazingatiwa kuwa ndio mfano wa kuigwa wa walinganizi wa demokrasia na wanahudumu katika ngazi za juu katika tawala za kidemokrasia!

Natija yake ni Muislamu au Mkriso nk. ima kiongozi au la ambaye anakiri kuwa na mshikamano na mfumo wa kirasilimali wa kisekula sio chochote bali ni mchangiaji katika majanga yasiyoisha yaliyopo yanayoukumba ulimwengu leo. Naam. Kwa sababu kujisalimisha kwao kwa mfumo wa kirasilimali wa kisekula umewafanya kuwa dhaifu na wasiotegemeeka katika kutatua matatizo yayo hayo ambayo yamechipuza kutoka katika kujifunga kwao na mfumo batili wa kirasilimali wa kisekula na kutekeleza nidhamu zake zenye sumu. Hivyo basi, sio jambo kushangaza kuwa na hizi purukushani za sasa nchini Uganda. Mwanzoni alikuwa ni Rais aliyefariki wa Tanzania John Pombe Magufuli ambaye aliipatiliza karata ya maadili, lakini aliridhika na utawala wa kidemokrasia ambao unawapa wanadamu uhuru usiokuwa na mipaka!

Kwa kuhitimisha, tunahitaji wafuasi wa kweli wa dini. Dini ya kweli ambayo inachipuza kutoka kwa Muumba wa ulimwengu, uhai na mwanadamu. Dini ambayo kitabu chake cha muongozo hakijachafuliwa au kuchanganywa ili kukidhi maslahi ya watu binafsi. Dini hiyo ni Uislamu. Uislamu ni mfumo (mwenendo kamili wa maisha) ambao huhitajika kutekelezwa juu ya wanadamu. Ili wanadamu waweze kufurahia amani, utulivu na ustawi ambao wanaouhitaji, lakini hawaja ushuhudia chini ya enzi ya mfumo wa kirasilimali wa kisekula. Hakika, ni Uislamu pekee chini ya nidhamu ya utawala ya Kiislamu ya Khilafah iliyosimamishwa kwa njia ya Utume ndiyo itakayoleta utuli katika nyanja zote za maisha.

Khalifah, Muislamu mwanamume mwenye uwezo na mwenye kujisalimisha katika maamrisho ya Uislamu na kufanya kazi usiku na mchana kuzitekeleza nidhamu za Uislamu. Ni yeye pekee kupitia Khilafah ndiye atakaye rudisha nidhamu na mpangilio katika ulimwengu huu wa fujo wa kirasilimali wa kisekula wenye uhuru usiokuwa na mipaka.

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu