Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Miaka 88 Gerezani kwa Kulingania Uislamu!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Machi 10, shirika la habari la Interfax-Russia liliripoti: “Wakaazi watano wa Crimea walipokea koloni kwa miaka yote 88 kwa kushiriki katika Hizb ut-Tahrir iliyopigwa marufuku katika Shirikisho la Urusi. Mahakama ya Kijeshi ya Wilaya ya Kusini huko Rostov-on-Don mnamo siku ya Alhamisi iliwahukumu wakaazi hao watano wa Crimea kifungo cha muda mrefu jela kuanzia miaka 15 hadi 19 katika kesi ya Hizb ut-Tahrir (inayotambuliwa kama shirika la kigaidi nchini Urusi na kupigwa marufuku), vyombo vya habari vya mahakama vilisema.

Kwa hivyo, Riza Izetov na Remzi Bekirov walipokea miaka 19 katika koloni kali ya serikali, Shaban Umerov - miaka 18, Raim Aivazov - miaka 17 (wote lazima watumikie miaka mitano ya kwanza ya kifungo chao gerezani), Farhod Bazarov - miaka 15 koloni (miaka minne ya kwanza na miezi 10 gerezani).

Maoni:

Mnamo Machi 18, katika sehemu hiyo hiyo, Mahakama ya Wilaya ya Kusini huko Rostov-on-Don, iliwahukumu Waislamu wengine watano wa Kitatari wa Crimea katika kesi ya "kundi la pili la Simferopol" Hizb ut Tahrir. Akim Bekirov, Seitveli Seitabdiev na Rustem Seithalilov walifungwa miaka 14 gerezani. Eskender Suleymanov na Asan Yanikov walifungwa gerezani miaka 15 kila mmoja.

Tangu kukaliwa kimabavu kwa Crimea na Urusi mnamo 2014, serikali ya Kremlin imekuwa ikiwatesa Waislamu wa Crimea. Mashababu wa Hizb ut Tahrir wanatuhumiwa kwa kujaribu kunyakua mamlaka, kulingania wa itikadi kali au ugaidi. Zaidi ya watoto 100 wenye ikhlasi wa Ummah wa Kiislamu walikamatwa na kufichwa katika magereza ya utawala huo usiomcha Mungu. Mashababu hao wanateswa magerezani, wanawekwa karantini kwa miezi kadhaa, wanadhihakiwa, hata kuswali wanakatazwa.

Familia za Kiislamu zimeachwa bila baba, waume, kaka na ziko chini ya uangalizi wa karibu wa huduma za kudhabu za Kremlin. Mamlaka hizo huunda hali mbaya za maisha zisizoweza kuvumilika kwa familia hizi na hujaribu kwa kila njia kumzuia mtu yeyote anayetaka kuwasaidia kwa njia yoyote ile. Kwa mbinu kama hizo, mamlaka hizo zinataka kuwaritadisha Waislamu wa Crimea waache dini yao.

Lakini, licha ya mateso haya yote ya kinyama, mashababu na familia zao wanaendelea kulingania mwamko wa mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu. Hii sio mara ya kwanza kwa Waislamu wa Crimea kuteswa na Urusi. Kwanza ilikuwa Urusi ya ki-tsar, kisha utawala wa kikomunisti wa Kremlin, na sasa utawala wa kiimla wa Putin.

Leo Waislamu kote duniani wako katika dhiki, nchini Crimea, Iraq, Caucasus, Afghanistan, Turkestan au Syria! Pamoja na mitihani yote hii, Umma wa Mtume Muhammad (saw) unazinduka, unatarajia ahadi ya Muumba wake, unafanya kazi bila kuchoka kuhuisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu, na unajitahidi kufikia radhi ya Muumba wake, Mola Mlezi wa walimwengu wote Mwenyezi Mungu.

(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur 24: 55]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu