- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hakuna Habari Njema Kwenye Riba, Hakuna Baraka Kutoka kwa Mapato Yake
(Imetafsiriwa)
Habari:
Rais Erdogan alitaja habari njema kwa wakulima katika taarifa moja baada ya mkutano wa Baraza la Mawaziri. Katika taarifa yake, Erdogan alitumia maneno yafuatayo: "habari yetu ya tatu njema kwa wakulima wetu ni kwamba tunaongeza kikomo cha juu cha mikopo yenye riba inayofadhiliwa na hazina. Hivyo, tunarahisisha upatikanaji wa fedha kwa wakulima wetu. Nawatakia wakulima wetu mafanikio mema kwa hatua hizi tulizochukua katika unyunyiziaji maji, nishati na mikopo. (Shirika la Habari la Ihlas 15.03.2020)
Maoni:
Licha ya kuwa Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Taala alihubiri Sharia takatifu ambayo inafaa kwa umbile la mwanadamu, tunashuhudia jinsi watawala, wanaolitupa hili nyuma ya migongo yao, wanavyohangaika katika kinamasi cha haram na uhalifu. Kama inavyojulikana, ustadi wa Rais Erdogan katika kuchanganya ukweli na uwongo ni maarufu. Katika hotuba yake miezi kadhaa iliyopita, alitangaza kupinga hilo kwa jina, kwa kusema kwamba kuna andiko kuhusiana na riba ya kiwango cha juu. Mara tu baada ya hapo, Erdogan alieneza riba hadi mashinani katika kiwango kilichoongezeka zaidi chini ya jina la "Mfumo Uliolindwa wa Kuweka Akiba na Kiwango cha Ubadilishanaji" bila ya kumcha Mwenyezi Mungu. Ingawa ni dhahiri jinsi uchumi unaozungukwa na riba ambao wamekuwa wakiutabikisha kwa miaka 20 ulivyosababisha uharibifu, kudai kupinga kwa kusema kwamba kuna andiko, pamoja na kuendelea na "Mfumo wa Kiwango cha Ubadilishanaji na Uwekaji Akiba", ambayo ni riba iliyozidishwa, ni kuchanganya haki na batili kwa makusudi.
Kilimo bila shaka ni mojawapo ya sekta zilizoharibiwa zaidi na serikali ya sasa, ambayo imezamisha uchumi wa Uturuki ndani ya kinamasi mara nyingi zaidi katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, achilia mbali kuurekebisha. Ingawa tuko katika jiografia yenye udongo mwingi sana na wenye rutba, kilimo kimefikia hatua ya mwisho kwa manufaa ya walafi wachache.
Kwa kweli, matatizo katika ugavi na vita kati ya Urusi na Ukraine ambapo wao ni waagizaji wazi wa nafaka na mafuta. Tena, kutokana na uharibifu unaoletwa na msukosuko wa kiuchumi ambao umedumu kwa miezi kadhaa nchini, ununuzi wa mahitaji muhimu kama unga, mafuta na sukari umekaribiwa kuwa wa ziada, ambapo inaonyesha ni kwa kiwango gani kilimo nchini Uturuki kiko. Kwa jinsi mambo yalivyo, watawala wa Uturuki ambao hawajajifunza lolote wakati wa utawala wao, hawataacha kujenga dunia yao na kuharibu Akhera yao.
Yote ni ukatili tu kusubutu kutoa riba, ambayo Mola wetu ameharamisha bila shaka, kama habari njema kwa wakulima. Hata hivyo Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Taala anatangaza kwamba riba hupunguza mali na rutba, na sadaka hurutubisha mali.
(يَمْحَقُ اللّٰهُ الرِّبٰوا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِۜ وَاللّٰهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ اَث۪يمٍ)
“Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukanya na afanyae dhambi.” [Al-Baqarah: 276].
Hebu tumkumbushe Rais Erdogan, ambaye anataka mkulima wake alime kwa kushajiisha riba. Hakuna mbegu iliyonunuliwa kwa riba inaota katika eneo la Dar al-Islam.
Ingawa uzalishaji huongezeka kwa idadi na ujazo, hakuna baraka kutoka kwa uzalishaji huu. Ndiyo, kuna mamilioni ya hekta za mashamba sasa, lakini hakuna rutba. Kama hakuna amani ya kijamii, uaminifu. Kwa kutawala kwa fikra za makafiri wa Kimagharibi, daima umekuwa katika fedheha dhidi yao, huku sheria za Mwenyezi Mungu zikiwa zimesimama. Ulijaribu kuweka uadilifu kupitia sheria zao. Hatimaye, ulisababisha mateso kuenea kwa kila nyanja ya maisha. Kwa uchumi wa kibepari, unawapa Waislamu umaskini na machafuko makubwa zaidi.
Ikiwa amani, uaminifu, rutba, ustawi, uzalishaji, utu na heshima vinatakikana tena katika ardhi hizi, ni jambo lisilokuwa na budi kuunda utawala ambao kwanza utaondoa haram zote, hasa riba, na kuhukumu kwa dini ya Mwenyezi Mungu. Siku tutakapo fanya haya yatokee, ardhi na mbingu zitatushukishia rehma. Haya ni mapambano yanayostahili kujitolea na subira.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmet SAPA