Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mashambulizi ya Urusi kwa Wanawake na Watoto Yanaakisi Kanuni za Kinyama za Sheria za Kisekula

 (Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 17 Machi 2022, vikosi vya anga vya Urusi vililipua ukumbi mmoja wa michezo katika mji wa Mariupol. Jumuiya ya kimataifa ilianzisha kulaani kitendo hicho kote duniani kwani iliripotiwa kuwa neno la Kirusi la "watoto" liliwekwa wazi nje ya jengo hilo. Wakati wa shambulizi hilo la bomu, mamia ya raia walisemekana kuwa wamejihifadhi katika jengo hilo, wengi wao wakiwa familia zenye watoto.

Petro Andriushchenko, mshauri wa meya wa jiji hilo, awali alisema wafanyikazi wa dharura walikuwa wakihangaika kulifikia jengo hilo kutokana na kushambuliwa kwa makombora kila mara.

Maoni:

Ukatili usiobagua wa serikali zinazolenga wanawake na watoto katika hali ya mapigano sio jambo geni katika siasa za magharibi. Umma bado una kumbukumbu za kihakika kabisa za "mshtuko na hofu" ya mvua ya mabomu ambayo yaliyomiminwa kwa watoto wasio na hatia wa Iraq chini ya maagizo ya Marekani. Wapiganaji wa Urusi ni watendaji wenye uzoefu wa mauaji ya watoto huku majeshi yao yakiwa na mazoezi mengi nchini Syria. Damu takatifu, isiyo na ulinzi ya watoto wachanga waliozaliwa ililengwa sana kwani wodi za uzazi ziliharibiwa na nguvu kamili ya chuki ya Putin kwa watu wasio Warusi.

Vita haviwezi kuchukuliwa kuwa sehemu salama kwa binadamu yeyote, hata hivyo sheria za Kiislamu zinatambua kwamba kanuni za mapambano kamwe hazivuki mipaka mitakatifu ya kuwadhuru wasiokuwa wapiganaji, yaani wanawake, watoto na wanyama. Mwenyezi Mungu (swt) asema kwa uwazi katika Aya ya Quran Surah Al-Maida aya ya 32;

 (مِنْ أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَنْ قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِنْهُمْ بَعْدَ ذَٰلِكَ فِي الْأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ)

“Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.”

Katika mfano mtukufu wa Khalifa Abu-Bakr (ra), iliharamishwa kitendo cha mapigano ya kiholela, kauli yake maarufu ilitoa amri zifuatazo;

“Mnapokutana na maadui zenu vitani, fanyeni inavyowapasa Waislamu wema.... Mwenyezi Mungu akikupeni ushindi, basi msitumie vibaya faida zenu na jihadharini msichafue panga zenu kwa damu ya mwenye kujisalimisha, wala msiguse watoto, wanawake, na wasio na madhaifu, na wanaume pia, ambao mtawakuta miongoni maadui zenu."

Pia, “Mnapopita katika eneo la adui, msikate mitende, wala miti mingine ya matunda, wala msiharibu mazao ya nchi, msiharibu mashamba, msichome nyumba...Uharibifu wowote usiwepo bila ya haja.”

Inasemekana alikwenda mbali na kusema kwamba pindi majeshi ya Kiislamu yanapokosa chakula, wanapaswa kuchukua chakula tu kutoka kwa raia pekee katika eneo la adui cha kutosha kwa mlo mmoja.

Kutokana na dalili hizi tunaweza kuona kwamba ukatili wa sheria ya kisekula ndilo jambo la kihakika linalohusika na siasa za dunia na sio kuregea kwa uadilifu na usalama wa Khilafah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu