Jumapili, 22 Muharram 1446 | 2024/07/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vita nchini Ukraine Vimeonyesha Kutokuwa na Msaada na Kutokuwa na Maana kwa Umoja wa Mataifa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kufuatia kulipuliwa mabomu kiwanda cha nyuklia cha Zaporozhye cha Ukraine, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amezitaka nchi zenye silaha za nyuklia kuzingatia ahadi zao za kutokuwa wa kwanza kutumia silaha hizo.

Akizungumza nchini Japan, ambako alihudhuria sherehe za kumbukumbu ya miaka 77 tangu kutokea kwa mashambulizi mawili ya kwanza ya nyuklia duniani ya Hiroshima na Nagasaki, Guterres alisema.

"Shambulizi lolote dhidi ya kiwanda cha nguvu za nyuklia ni la kujitoa uhai na natumai kuwa mashambulizi haya yatakoma, na wakati huo huo natumai kuwa IAEA itaweza kupata njia ya kufikia kwa kiwanda hicho na kutekeleza mamlaka yake .... Naamini kuwa huu ndio wakati ambapo hatari ya makabiliano ya nyuklia inarudi, jambo ambalo tumelisahau kwa miongo mingi. Wakati huu, kama nilivyosema, unapaswa kutumika kutoa wito kwa nchi zote za nyuklia kujitolea kwa kanuni ya kutokuwa wa kwanza na uvamizi."

Na pia, Guterres, alipokuwa ziarani Odessa, alizungumza na kuegemea upande wa kukomeshwa kwa utumiaji kijeshi wa kiwanda cha nguvu za nyuklia cha Zaporozhye. (https://ru.euronews.com/2022/08/08/guterres-on-nuclear)

Maoni:

Ni rahisi kuona kwamba matamshi yote ya Guterres, kama msemaji wa msimamo wa Umoja wa Mataifa, kuhusu hali ya kiwanda cha nguvu za nyuklia cha Zaporozhye haswa, na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, kwa jumla, hayaleti chochote zaidi ya wasiwasi.

Anatoa wito, anatumai, anaonyesha hofu, nk. Kwa jumla, inatangaza msimamo laini, usio na uwiano na mizani ya tishio la kijeshi la Kirusi kwa kulipiga mabomu eneo la kiwanda cha kawi.

Ingawa, tunajua mifano ya msimamo mkali, thabiti zaidi wa UN, kwa mfano, kuhusu hali ya Yugoslavia ya zamani. Wakati huo maazimio husika yalipitishwa, na vikosi vya pamoja vya NATO vilitumiwa ... Ingawa, bila kuomba janga kwa matukio hayo, hata hivyo inapaswa kutambuliwa kuwa hatari ya janga kubwa la nyuklia kutokana na mashambulizi dhidi ya kiwanda cha kawi ya nyuklia cha Zaporozhye ni kubwa zaidi.

Kwa mara nyingine tena, tumekinaika kwamba Umoja wa Mataifa ni shirika lisilofaa kabisa katika muktadha wa kuhakikisha usalama, lakini "linafaa" kwa dola kuu katika michezo yao ya kisiasa.

Kwa kesi ya Yugoslavia, kazi ilikuwa ni kufufua na kuimarisha NATO kama ngome ya uwepo wake na ushawishi katika Ulaya. Na sasa, Marekani inatumia mgogoro huo ili kuidhoofisha zaidi EU, kuleta Shirikisho la Urusi katika "hali ya ulazima", yaani katika hali dhaifu, lakini bado yenye tishio, ambayo kwayo Marekani "inalinda" Ulaya.

Kwa kuongezea, Urusi inayodhibitiwa inahitajika kama kizuizi dhidi ya matarajio ya China.

Kwa hivyo, "kulemaa" kwa Umoja wa Mataifa sio aina fulani ya kuachwa kando, bali ni hatua ya maana kabisa, kama "taasisi" inayotumikia maslahi ya dola kuu, na isiyo husiana na usalama halisi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abu Adil
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu