Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Janga la Mafuriko Laulemea Uongozi Tepetevu wa Pakistan

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mafuriko ya hivi karibuni nchini Pakistan sio tu yamesababisha uharibifu lakini ukubwa wa maafa umepita mafuriko ya awali ya 2010 na tetemeko la ardhi mwaka 2004. Zaidi ya theluthi moja ya nchi iko chini ya maji na zaidi ya watu milioni 33 wamekimbia makaazi yao. [CNN] Idadi ya vifo tayari imevuka alama ya 1000 na kuzuka kwa magonjwa, ukosefu wa chakula na maji safi, na makaazi duni inamaanisha kuwa idadi ya mwisho itakuwa kubwa zaidi. Kwa uchache, mwitiko kutoka kwa jumuiya ya kimataifa umekuwa duni sana, lakini hili limegubikwa na mchezo wa lawama wa ndani kati ya uongozi wa kiraia na kijeshi kwa kutofanya vya kutosha kuwasaidia wale walioathirika zaidi.

Maoni:

Mafuriko yamekuja wakati mbaya zaidi kwa Pakistan. Nchi ilikuwa tayari inakabiliwa na mgogoro wa kiuchumi uliochochewa na mfumko wa bei duniani, bei ya juu ya nishati, nakisi ya miamala ya kiuchumi ya ndani na nje ya nchi na masharti ya IMF. Ikiongezewa mchanganyiko huu, ni ukuaji duni wa uchumi uliowekwa na nchi wakati wa enzi ya Uviko-19. Hata hivyo, Uviko-19 na mzozo wa kiuchumi haukuharibu uchumi wa kilimo wa Pakistan, ambao ndio msingi mkuu wa Pato la Taifa la Pakistan. Kuwasili kwa mafuriko ya sasa kumeharibu kabisa sehemu kubwa ya mazao, ambayo ina athari mbili kuu.

Kwanza, mamilioni ya watu hawataweza kujilisha wenyewe na hii itaweka mzigo mkubwa kwa serikali ya shirikisho. Pili, uuzaji nje wa vyakula vya wanati utapunguzwa sana na hii itaathiri uwezo wa Pakistan kupata sarafu za kimataifa za kutosha kulipa riba ya deni lililorundikana.

Kutia msumari wa moto kidonga, misaada ya kigeni inayowasili kutoka ng'ambo haistahiki kuandika kuihusu. Marekani imetoa $30 milioni, ambazo ni sawa na chini ya $1 kwa kila mmoja ya watu milioni 33 waliokimbia makaazi yao. Canada imetoa $5 milioni, na hii ni chini ya senti 20 kwa kila mtu aliyehama. Wakati huo huo Uingereza imekabidhi pauni 800,000 na hii ni sawa na pensi 2 kwa kila mtu. Kwa kulinganisha, Ukraine yenye idadi ya watu 44 milioni imepokea msaada wa mabilioni ya dolari kutoka Magharibi.

Unafiki wa Kimagharibi haukomei kwenye misaada chembe inayotolewa kwa Pakistan. Chini ya usimamizi wa Magharibi, IMF kwa miongo minne iliyopita imeweka masharti magumu ya kiuchumi ambayo yamedhoofisha msingi wa viwanda wa Pakistan, kumomonyoa ubwana wake wa kiuchumi na kuongeza mzigo wake wa deni la nje hadi $ 132 bilioni. Sehemu kubwa ya deni hili linadaiwa na Magharibi na mashirika yao ya kimataifa kama vile IMF na WB. Iwapo Magharibi ilikuwa na nia ya dhati ya kuisaidia Pakistan katika nyakati hizi za mitihani, basi jambo la chini kabisa ambalo ingeweza kulifanya ni kusamehe deni hili. Hii ingeelekeza mabilioni ya dolari zilizotengwa kwa ajili ya malipo ya riba kwa fedha zinazohitajika sana kwa ajili ya juhudi zinazoendelea za usaidizi.

Uongozi wa kiraia na kijeshi una hatia zaidi kuliko Magharibi katika hali ambayo Pakistan inajipata. Iwapo uongozi wa Pakistan ungetabanni njia ya kujitosheleza kiuchumi na kukwepa mipango ya marekebisho ya kimuundo ya IMF (SAP), misingi ya kiuchumi ya nchi hiyo ingekuwa imara zaidi katika kukabiliana na majanga hayo. Zaidi ya hayo, uongozi wa Pakistan umetenda kidogo mno kujiandaa kwa tukio kama hili la sasa. Watu hawangepaswa kamwe kuruhusiwa kuishi karibu na maeneo yanayokumbwa na mafuriko, na rasilimali nyingi zilipaswa kuwekezwa katika juhudi za kudhibiti maafa. Aidha, mafunzo yaliyopatikana kutokana na maafa yaliyopita yalipaswa kupelekea hatua madhubuti za kutatua maafa hayo.

Hata hivyo, kinacho kera zaidi ni malumbano ya mara kwa mara kati ya viongozi wote wa Pakistan ili kujipatia sifa kwa juhudi ndogo kabisa za misaada ya mafuriko kwa gharama ya kusaidia watu wanaostahili zaidi. Wakati umewadia kwa watu wa Pakistan kukomesha mfumo wa dola ya kitaifa ambao umeufanya uongozi wa Pakistan kuwa tasa wakati wa majanga ya mara kwa mara na baya zaidi kuwafanya watiifu milele kwa dola za kigeni. Hili linaweza kutimizwa tu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume pekee.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Majeed Bhatti

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu