Alhamisi, 07 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Urusi Yaimarisha Uwepo wa Kijeshi katika Asia ya Kati

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu alitangaza nia ya Moscow ya kuimarisha kambi za kijeshi nchini Tajikistan na Kyrgyzstan kuhusiana na hali nchini Afghanistan. Mkuu huyo wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi alitoa taarifa hiyo dhidi ya mazingira ya mazoezi ya kijeshi nchini Tajikistan "Ushirikiano wa Kikanda - 2022" pamoja na ushiriki wa nchi za Asia ya Kati, Amerika, Mongolia na Pakistan.

Sergei Shoigu alifichua mipango ya Moscow ya kuimarisha kambi za kijeshi huko Asia ya Kati katika mkutano wa nchi za SCO huko Tashkent, na kutangaza tishio linaloongezeka kwa usalama wa eneo hilo kutoka Afghanistan:

"Changamoto kubwa ya usalama katika Asia ya Kati inasalia kuwa hali ya mambo nchini Afghanistan, ambapo mashirika ya kimataifa ya kigaidi kama ISIS na Al-Qaeda yanazidi kuwa changamfu. Kutokana na hali ya makabiliano ya kisilaha yanayoendelea, hali ya kijamii na kiuchumi inazidi kuzorota, itikadi ya misimamo mikali ya kidini inapandikizwa, ulanguzi wa dawa za kulevya na uhalifu wa kuvuka mipaka unashamiri. Kwa upande wetu, tunaongeza utayari wa upambanaji wa kambi za kijeshi za Urusi nchini Kyrgyzstan na Tajikistan, pamoja na vikosi vyengine vya kukabiliana na hali za mgogoro zinazoweza kutokea", - Shoigu alisema.

Maoni:

Waangalizi wanaona kuwa kauli hii kimsingi ni kutokana na kudhoofika kwa ushawishi wa kijeshi na kisiasa wa Urusi katika eneo la Asia ya Kati dhidi ya mazingira ya kushindwa kwa uvamizi wa Ukraine, na sio kwa tishio lolote la kweli. Endapo kulikuwa na tishio kubwa la uingiliaji kati kutoka Afghanistan, basi Shirikisho la Urusi halingehamisha sehemu ya kikosi chake kilichowekwa Tajikistan kwenye vita vya Ukraine. Usalama wa eneo hilo ndio wa mwisho kwa wasiwasi wa Kremlin.

Mwanasayansi wa kisiasa wa Kyrgyz Adil Turdukulov anaamini kwamba Moscow inashikilia nukta za mvutano ili isipoteze ushawishi wake katika Asia ya Kati. Mfano wa hili, kwa maoni yake, ni uhusiano kati ya Taliban na Dushanbe:

"Shoigu, kwa upande mmoja, anazungumza kwa usahihi kuhusu baadhi ya changamoto zilizopo katika Asia ya Kati, mojawapo ni hali nchini Afghanistan. Hii ni hatari sana, haswa kwa Tajikistan, ambayo inapakana nayo. Kwa sababu kuna matatizo mengi kati ya Dushanbe na Kabul. Lakini sababu zingine zimefichika ndani ya maneno ya Shoigu. Kwa sababu msimamo wa siasa za kijiografia wa Urusi unadhoofika katika eneo hilo. Tunaona kwamba nchi za Asia ya Kati zinahama kutoka Kremlin na zinajaribu kufanya sera zao wenyewe za kigeni. Moscow ilikuwa na ukiritimba wa usalama wa kisiasa na kijeshi katika eneo hilo. Sasa wanaogopa kupoteza turufu yao, na hii inawatia wasiwasi sana. Sasa vitendo vya Urusi vinaelekezwa kwa Ukraine. Pia ni uwanja wa mapambano na Magharibi. Pengine, ikiwa eneo jengine moto la mzozo litajitokeza, Magharibi italazimika kujadiliana na Urusi. Kwa hivyo, Moscow ina sababu ya kuunda maeneo yenye migogoro katika kanda zengine”.

Ni muhimu kuzingatia kuwa mara tu baada ya taarifa ya Shoigu, baadhi ya machapisho yalionekana kwenye vyombo vya habari vya Urusi kuhusu Taliban walikuwa wakipeleka vikosi vya ziada na magari ya kivita kwenye mpaka na Tajikistan. Kwa mfano, mtandao wa Urusi wa Avia.Pro na Masuala ya Kijeshi unaripoti kwamba vifaru na magari mengine ya kivita ya harakati ya Taliban yalionekana yakielekea kwenye mpaka wa Tajikistan.

"Tunazungumzia kuhusu upelekaji wa kundi kubwa la magaidi katika eneo la karibu na mpaka na dola hii, ambao huenda ukawa ni ushahidi kwamba magaidi hao wanajiandaa kuishambulia Tajikistan", - Avia.Pro inabainisha.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu