Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mshtuko wa Mfumko wa Bei wa Marekani huku Wamarekani Wakiendelea Kulipia Zaidi Chakula bila ya chochote ila Mandhari ya Ukosefu wa Ajira Wakitarajia ikiwa Sera za Benki Kuu Zitafanikiwa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Leo, Rais Joe Biden alitoa taarifa kuhusu kupanda kwa Fahirisi ya Bei ya Watumizi (CPI) mnamo Septemba. Alichora takwimu za kukatisha tamaa kuhusu uchumi wa Marekani kwa njia chanya ya kushangaza: "Takwimu za leo zinaonyesha maendeleo zaidi katika kushusha mfumko wa bei duniani katika uchumi wa Marekani. Kwa jumla, bei zimekuwa shwari katika nchi yetu miezi hii miwili iliyopita: hizo ni habari njema kwa familia za Marekani, huku kukiwa na kazi zaidi ya kufanya. Bei ya gesi imeshuka kwa wastani wa $1.30 galoni tangu mwanzo wa kiangazi. Mwezi huu, tuliona ongezeko la bei polepole kutoka mwezi uliopita kwenye maduka ya mboga. Na mishahara halisi ilipanda tena kwa mwezi wa pili mfululizo, na kuzipa familia zinazofanya kazi kwa bidii afueni kidogo.

Itachukua muda na azma zaidi kupunguza mfumko wa bei, ndiyo maana tulipitisha Sheria ya Kupunguza Mfumko wa Bei ili kupunguza gharama ya huduma za afya, dawa na kawi. Na mpango wangu wa kiuchumi unaonyesha kuwa, huku tukipunguza bei, tunaunda kazi zenye kulipa vizuri na kurudisha utengezaji nchini Amerika.

Maoni:

Fahirisi ya Bei ya Watumizi ni kipimo cha mfumko wa bei, na kama vile Biden alivyosema; mfumko wa bei sasa ni tatizo la kiulimwengu. Hata hivyo, uchumi wa Marekani ndio mkubwa zaidi duniani, na sarafu za dunia zinafungamana nao. Hivyo basi Marekani sio mwathirika, kama ambavyo Rais wa Marekani angependa watu waamini; badala yake, ni injini inayoendesha mateso ya kiuchumi duniani.

Benki Kuu ya Marekani imekuwa ikiongeza viwango vya riba katika juhudi za kupunguza kasi ya mfumko wa bei, ambao ulifikia kiwango cha juu cha miaka arobaini cha 9.1% mwezi Juni na ulipungua kidogo katika miezi miwili iliyofuata. Hata hivyo, hiyo hupimwa kwa muda wa miezi 12 hadi mwezi wa kuripoti. Takwimu za kila mwezi zinaonyesha kuwa kulikuwa na ongezeko la 0.1% kwa Julai hadi Agosti, ambayo ilikuwa kinyume kabisa na kile wanauchumi walitarajia kulingana na CNN Business: "Wanauchumi walikadiria kuwa mfumko wa bei ungeshuka kutoka Julai hadi Agosti kwa 0.1%, baada ya kushikilia kasi ya ukuaji wa 0% kuanzia Juni hadi Julai. Mfumko wa bei wa Marekani ni wa juu sana kuliko shabaha ya 2% ambayo Benki Kuu inatarajia kufikia kwa kuongeza viwango vya riba, ambayo ni ushuru unaotumika sana kupunguza kasi ya uchumi wa kirasilimali, unaotegemea riba, kupitia kuongeza gharama ya kukopa. Hii haionekani kufanya kazi sasa.

Gharama ya petroli ilishuka kwa 10.6%, ambayo ni tete sana na inategemea zaidi juu ya matukio ya kisiasa kama vile vita vya Ukraine kuliko hali ya uchumi wa Marekani. Hata hivyo, karibu kila kitu kingine kimekuwa ghali zaidi. Kulingana na ripoti ya CPI (Septemba 13, 2022): "Fahirisi ya chakula cha nyumbani iliongezeka kwa asilimia 13.5 katika miezi 12 iliyopita, ongezeko kubwa zaidi la miezi 12 tangu kipindi kilichoishia Machi 1979." Mfumko wa bei unawaumiza maskini zaidi kuliko matajiri wakubwa. Masikini hulipia mara mbili. Kwanza, mishahara yao hununua kichache; na huku bei za vyakula zikipanda zaidi sasa, wale wanaotumia sehemu kubwa ya mapato yao kununua chakula ndio wanaoteseka zaidi. Pili, wakati hatimaye, mfumko wa bei unapodhibitiwa kitu chengine hutokea ambacho huathiri vibaya maskini: ukosefu wa ajira unaongezeka! Ikiwa shabaha ya mfumko wa bei ya 2% itafikiwa, ukosefu wa ajira unatarajiwa kuongezeka hadi karibu 6% na upotezaji wa kazi milioni 5.3 wa Amerika. Kwa hiyo, baada ya kujitahidi kumudu kupanda kwa gharama za chakula kwa miezi mingi, malipo ambayo Mmarekani mwenye bidii anaweza kutazamia endapo mfumko wa bei utaregeshwa chini ya udhibiti ni hatari kubwa zaidi ya kupoteza kazi yake na kutokuwa na mapato yoyote ya kununua nayo chakula.

Hivi ndivyo Mwenyekiti wa Benki Kuu ya Amerika Jerome Powell alimaanisha alipoonya kuwa kutakuwa na "maumivu kwa familia na biashara" kupitia kuongezeka viwango vya riba. Maumivu haya ni ya muda kwa kile anachokiita "kutua taratibu" ambapo uchumi, pamoja na mfumko wa bei, vipungua polepole na kisha kustawi. Vyenginevyo, kutakuwa na mporomoko wa kina na wa kudumu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu