Jumamosi, 09 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uadilifu Hupelekea kwenye Kutii Kanuni bila ya Haja ya kutumiwa Nguvu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Ijumaa, 16 Septemba 2022, BBC iliripoti juu ya kifo cha mwanamke mmoja wa Iran mwenye umri wa miaka 22 baada ya kukamatwa na polisi wa maadili kwa madai ya kutofuata sheria kali za kufinika kichwa. Kukamatwa kwake kulisababisha apelekwe hospitalini kwa jeraha la kichwa lililomsababishia kukosa fahamu kwa siku kadhaa.

Maoni:

Hadithi kama hizi husambaa lakini si mara zote kwa sababu sahihi. Inatisha kufikiria kuwa wanawake wanaweza kuchukuliwa na chombo cha usalama, kupata majeraha chini ya ulinzi na kisha kufa. Kamwe hapawezi kuwa na uhalali wa kupoteza maisha ya mwanadamu ambayo hayakuidhinishwa na Mwenyezi Mungu (swt). Hakuna mtu aliye na haki ya kutoa kifo kwa masharti yao wenyewe.

[اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنْ الْكِتَابِ وَأَقِمْ الصَّلاَةَ إِنَّ الصَّلاَةَ تَنْهَى عَنْ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنْكَرِ وَلَذِكْرُ اللَّهِ أَكْبَرُ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ]

“SOMA uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yatenda.” [Al-Ankabut: 45]

Kesi nyingi za wanawake wanaokufa mikononi mwa wale wanaotekeleza sheria kutoka kwa fikra zao wenyewe zinatokea kwa sababu ya ukosefu wa mamlaka sahihi.

Raia, vitendo vya polisi na hata wale wanaokaimu nafasi za mamlaka mara nyingi hufanya vitendo vinavyokiuka haki za binadamu na kutumia vibaya mamlaka waliyonayo juu ya wengine. Hoja za maadili sio udhuru. Mwenyezi Mungu (swt) alitoa sheria maalum za Hudud katika mifumo ya mahakama ya Uislamu ambazo zinaweza kusababisha kupoteza maisha au kiungo. Hata hivyo kukashifiwa kwa watekelezaji sheria hawa na kuwataja kuwa ni wa kishenzi hakuna msingi wowote kiuhalisia kwani mtu anapoangalia historia ya Khilafah, vitendo vya kihalifu vilivyo stahiki hatua hizi vilikuwa ni vichache.

Kwa hivyo je kiwango hicho cha juu cha maadili kilidumishwa vipi kwa hiari na raia, kiasi kwamba picha zipo nchini Palestina na Uturuki ambapo wanawake (wengine hata wasiokuwa Waislamu) walifinikwa kulingana na masharti ya Sharia?

Ukweli ni kwamba jamii zote zilizostaarabika zinahitaji kanuni, watu wanapohisi haki ya mfumo na kuwa na utiifu wa kuiamini Dola kwamba inafanya kazi kwa maslahi ya watu wote, hutii sheria bila ya haja ya kutumiwa nguvu. Ubaguzi wa rangi, kuyatenga makundi na kuwadhalilisha watu kwa ufupi hayakuwepo kama mambo ya kawaida ya kijamii.

Wanawake waliziona sheria kama sehemu ya kifurushi bora cha haki zinazohudumia maslahi ya wote. Lau wangetaka wangeweza kuiacha Khilafah kwa uhuru na kukandamizwa na hatari za tawala zengine dhalimu halisi. Hatujawahi kuona msafara mkubwa wa namna hii wa watu wanaoikimbia Khilafah kwa ajili ya kutafuta usalama mahali pengine, kwa hakika kulikuwa na kinyume chake, watu walitafuta hifadhi katika mipaka ya mfumo tegemewa na wenye utu na uaduilifu wa Mwenyezi Mungu (swt). Tunaomba kwamba vitendo hivi vya dhulma viondolewe kwenye habari milele kupitia kusimamishwa tena Dini ya Qur'an na Sunnah kwa mara nyingine tena na ni lazima kama Umma tutambue juhudi zetu za kila siku za kusimamia jambo hili binafsi kupitia kufanya kazi na kundi la watu wema ili kunali malipo makubwa ya Akhera.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu