Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Watawala wa Mfumo wa Kirasilimali Wana Ujanja Mkubwa Katika Kuwahadaa Watu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Rais Erdogan, katika taarifa alizozitoa baada ya Mkutano wa Rais wa Baraza la Mawaziri, alitangaza kuwa madeni ya watu milioni 5.5 ambao wako chini ya taratibu za utekelezaji yatafutwa. Kwa hivyo, wananchi wataondoa madeni yao ya lira elfu 2 na chini, ambayo yako chini ya taratibu za utekelezaji. (Chanzo: Mashirika ya Habari)

Maoni:

Kabla ya uchaguzi ujao wa urais wa 2023, Rais Erdogan anachukua hatua kadhaa kunyanyua kura yake inayoanguka na kushinda uchaguzi huo. Bila ya aibu anatoa habari kuu kwamba madeni ya watu milioni 5.5 yatafutwa kama injili kuu. Hata hivyo, idadi ya faili za utekelezaji, ambayo ilikuwa milioni 8 mwaka 2008, imeongezeka mara 3 tangu wakati huo na imefikia milioni 24. Kulingana na data ya UYAP, kufikia Machi 19, 2022, jumla ya faili za utekelezaji zilizo wazi zilivunja rekodi kwa kuona kiwango cha milioni 23 elfu 525.

Watawala wanaoongoza mfumo wa kibepari wana ustadi na hila kubwa katika kuhadaa na kughilibu watu. Sifa hii imekuwa ndio tabia yao. Wanaonyesha hata chembe ndogo wanayowapa watu wao kana kwamba ni mafanikio makubwa. Zaidi ya hayo wanajivunia. Wanatangaza, wanataka kuzungumzwa kwenye vyombo vya habari kwa siku nyingi. Kwa hatua kama hizo, serikali inataka kuweka katika jamii ufahamu kuwa inajali matatizo ya wananchi na inatatua matatizo ya wananchi.

Hata hivyo, wakati watu leo ​​hii wanapata ugumu wa kukidhi hata mahitaji yao ya kimsingi, ongezeko la karibu kila siku la mahitaji ya kimsingi la serikali linalazimisha maisha ya watu siku hadi siku. Hatua hii iliyochukuliwa na serikali haitoshi kutatua matatizo ya kiuchumi ya wananchi. Nchini Uturuki leo, mshahara wa chini ni lira 5500, wakati kikomo cha njaa ni kama lira elfu 7, mstari wa umaskini ni lira elfu 22, kufutwa kwa deni la lira elfu 2 za watu milioni 5.5 ambao wako chini ya kesi za utekelezaji katika kipindi fulani ambapo deni ni tone kwenye ndoo.

Kwa upande mmoja serikali inaepuka watu wenye vitu vidogo, kwa upande mwingine inafuta mabilioni ya lira za madeni ya makampuni makubwa na kuhamisha rasilimali zote za serikali kwao kana kwamba haitoshi. Vile vile, chini ya jina la ubinafsishaji, inazifukuza bidhaa za umma hadi kwa makampuni ya kibepari. Huku mameneja wakizidi kutajirika kila uchao, faida za mabenki zinazowanyonya umma na kutengeneza pesa kutokana na fedha hizo hufikia 500%, huku umma kwa upande mwingine ukizidi kuwa masikini kila siku.

Hata hivyo, Waziri wa Hazina na Fedha Nureddin Nebati, katika taarifa yake aliyoitoa katika miezi ya hivi karibuni, alisema kuwa mwaka 2002, wakati Chama cha AK kilipoingia madarakani, familia milioni 1 zilipokea usaidizi wa serikali, na mwaka wa 2021, idadi hii iliongezeka hadi milioni 4.3.

Waziri wa Hazina na Fedha Nebati anajigamba kwa kusema kuwa watu wanaopokea misaada ya kijamii kutoka serikalini wanaongezeka huku kwa upande mwingine hataji kuwa idadi ya watu masikini katika jamii inaongezeka kila kukicha. Tena, Rais Erdogan anatoa kama habari njema kubwa kwamba watu hawawezi kulipa madeni yao kutokana na ongezeko la faili za utekelezaji siku baada ya siku, na kisha kuanzishwa kwa msamaha wa madeni. Lakini haya hayapozi majeraha ya watu. Hata hivyo, kinachopaswa kutokea si kwa familia milioni 1 kupokea msaada kutoka kwa serikali au kufuta madeni yao, bali kupunguza idadi ya watu wasio na ajira, maskini na kuunda sera zinazolenga kukidhi mahitaji ya kimsingi ya hata mtu mmoja mmoja katika jamii. Hili haliwezekani kwa utaratibu wa kiuchumi wa mfumo fisadi wa kirasilimali, bali kwa kutekelezwa utaratibu wa kiuchumi wa Kiislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yılmaz ÇELİK

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu