Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Wanawake na Watoto wa Kiislamu Wanakumbwa na Njaa Hadi Kufa Nchini Somalia huku Watawala wa Waislamu Wakiunga Mkono Ukandamizaji Ulimwenguni

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 5 Oktoba 2022, BBC iliripoti kuwa Somalia inakabiliwa na baa la njaa inayotokana na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40. Hadithi ya dada mmoja Muislamu inayofichuliwa na waandishi wa habari, ni ile ya Fatima Omar ambaye alimzika mtoto mmoja wa kiume kutokana na njaa na tayari alikuwa ameshamzika bintiye wa miaka 3 ambaye alifariki huku akitembea kwa siku 10 kutafuta msaada. Anawaambia waandishi wa habari kwamba hakuwa na nguvu za kumzika mtoto wake na alilazimika kuuacha mwili wake kando ya barabara huku akijua kuwa Fisi walikuwa wanakaribia kuingia ndani. Anasema; "Siwezi kuomboleza, nahitaji kutafuta kazi na chakula ili kumweka mwingine hai".

Maoni:

Kambi zinazotumika kama kimbilio la Ummah maskini wa Somalia zimefanyiwa utafiti na matokeo yanaonyesha kuwa theluthi mbili ya wanawake na watoto wana utapiamlo.

Wanawake huachwa kutanga-tanga katika nchi kavu kwa muda wa siku nyingi bila chakula ili kujaribu kufika mahali ambapo wanaweza kupata afueni kwa mateso yao. Wazee na vijana vilevile hawajaepushwa na mateso haya na kuna mamilioni katika Pembe ya Afrika ambao wanahangaika bila msaada wowote unaokuja kupitia mataifa tajiri ya Kiislamu ambayo yana mabilioni ya dolari kusaidia.

Madaktari katika maeneo hayo hutoka kitanda hadi kitanda wakisubiri watu waliokonda mno kufa. Hakuna vifaa vya kutibu hali zao na ujuzi wao pekee haufai chochote.

Kuongeza katika janga hili, mkurupuko wa ukambi pia unaikumba Somalia na wanawake na watoto wanabidi kustahimili mtihani huu vilevile.

Daktari mmoja anasimulia juu ya kujitahidi hata kuunganisha mipira ya kupitishia dawa ndani ya ngozi ambayo imeharibiwa vibaya sana na njaa kali ya muda mrefu. Hofu ya maisha ya kawaida ya kila siku katika nchi zetu haivumiliki. Inakuwaje kwamba kina dada watukufu wanakaa kwenye udongo mkavu, peke yao, wakijenga vibanda kujikinga na jua kutokana na takataka wanazopata na lazima wawatazame watoto waliowabeba kwa muda wa miezi 9, wakifa, mmoja baada ya mwengine!

Viongozi hawa wahalifu wa nchi zetu wako wapi na kwa nini wanaachwa kufuja matrilioni ya dolari zetu kununua silaha kusaidia uchumi wa mataifa ya magharibi?

Inakuwaje kwamba tani za chakula zinaweza kutupwa kwenye majaa ya taka ili kuwezika bei kuwa juu kwa biashara za kiulimwengu na watoto wetu wadogo kuachwa na uchungu wa tumbo tupu.

Huenda Mwenyezi Mungu ameandika mvua inyeshe kwenye ardhi au la, lakini haikuandikwa kwa Ummah kuwa na watendaji wa haramu wanaoizuia Quran na Sunnah kuishi katika sura za Khilafah. Tulichokifanya kurudisha hukmu sahihi za Sharia kitaandikwa katika vitabu vyetu vya maadili siku ya kiama. Hatuwezi kuwatelekeza watoto wetu wafe kabla hata hawajapata nafasi ya kuishi.

Wingi wa utajiri wa Ummah huu unajulikana sana, lakini mgao wa haki za watu kwa chakula, mavazi na malazi umeachiwa mikono ya ulafi ya makhaini wanaoendesha nchi zetu.

Waziri mmoja wa Somalia alisema; "Kama hatutapokea misaada tunayohitaji, mamia kwa maelfu ya watu watakufa. Mambo tunayofanya sasa tulihitaji kuyafanya miezi mitatu iliyopita. Kwa kweli tuko nyuma. Isipokuwa kitu kitokee [haraka] nadhani janga litatokea katika eneo hili."

Angefanya vyema zaidi kulingania Khilafah kwani maneno yake yote ni dhaifu na hayana mfumo mpana wa kuondoa mgawanyiko wa utaifa na maadui wa kikoloni kudhibiti rasilimali zetu. Majeshi yetu pekee yangeweza kubeba chakula katika Pembe nzima ya Afrika kama yasingekuwa yanapoteza muda kuzubaa au kuua Waislamu wengine ili kuwatumikia viongozi wa kigeni.

Imesimuliwa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ فِي الْمَاءِ وَالْكَلَإِ وَالنَّارِ، وَثَمَنُهُ حَرَامٌ»

“Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: maji, malisho na moto - na thamani yake ni haramu”.

Tunawaombea ndugu zetu barani Afrika kwamba hivi karibuni wataziona haki za Uislamu katika Amir-ul-Muslimin ili kuhakikisha kwamba aya hizi na maandiko ya Uislamu yanaishi ndani ya maisha ya Ummah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu