Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Urusi Yakitambua Chama cha Mwamko wa Kiislamu cha Tajikistan kama Shirika la Kigaidi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mahakama ya Upeo ya Shirikisho la Urusi iliridhika na dai la Afisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu la kukitambua Chama cha Mwamko wa Kiislamu cha Tajikistan (IRPT) kuwa shirika la kigaidi. Imeripotiwa na RAPSI. Kesi sawia na hii iliwasilishwa mnamo Julai mwaka huu.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Urusi Igor Krasnov alimfahamisha Rais wa Tajik Emomali Rahmon kuhusu hili. Kesi hiyo iliwasilishwa kwa ombi la Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Tajik Yusuf Rahmon.

Maoni:

Ndani ya miaka 16, IRPT ilikuwa chama pekee cha Kiislamu kilichofanya kazi rasmi katika eneo la USSR ya zamani. Mnamo mwaka wa 2015, chama hicho kilituhumiwa kwa kuandaa mapinduzi ya kijeshi yanayodaiwa kupangwa na aliyekuwa naibu waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Abdukhalim Nazarzoda ambapo baada ya hapo Mahakama ya Upeo ya Tajik ilikitambua chama hicho kama shirika la kigaidi. Tangu wakati huo, Emomali Rahmon mara kwa mara amewataka washirika wake kukitambua IRPT kama cha kigaidi kwenye majukwaa ya CSTO, SCO na CIS.

Ikumbukwe kwamba IRPT ndiyo iliyokuwa mhimili wa Umoja wa Upinzani wa Tajik ambao utawala wa Rahmon kupitia upatanishi wa baadhi ya nchi ulitia saini makubaliano ya amani mwaka 1997. Wadhamini wakuu wa mikataba hiyo walikuwa ni Urusi iliyounga mkono National Front na Iran, iliyosimama nyuma ya mgongo wa UTO. Na masharti makuu ya makubaliano hayo yalikuwa uwakilishi wa 30% wa UTO katika miundo wa mamlaka.

Hatua kwa hatua akiimarisha nguvu zake, Emomali Rakhmon wa Moscow, kwa msaada wa Kremlin, aliwaondoa wawakilishi wa UTO katika miundo ya utawala na hata washirika wake wa zamani. Kulingana na waangalizi, katika miaka ya tisiini, Kremlin haikuwa na njia nyingine ya kuimarisha nafasi yake katika Tajikistan ya baada ya Usovieti, isipokuwa kujadiliana na upinzani wa Tajik.

Baada ya nguvu ya ulinzi wa Moscow kuimarishwa, upinzani hatimaye ulishindwa. Na Moscow, ambayo ni mdhamini wa utiifu wa mikataba hiyo, haikuchukua hatua yoyote, kwa sababu kila kitu kilifanyika kwa idhini ya Kremlin, ikiwa sio kwa amri yake. Ni wazi, makubaliano ya amani ya 1997 ndio sababu ya matukio haya yote, wakati upinzani wa Tajik ulipoiamini Urusi, hatima ilikuwa tayari imeshatabiriwa. Urusi ni adui wa kihistoria wa Uislamu na Waislamu, katika desturi ya kuweka vibaraka wao juu ya makoloni, watakaotumikia tu maslahi ya himaya hiyo pekee.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu