Jumanne, 17 Muharram 1446 | 2024/07/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hatua za Kwanza za Kupiga Marufuku Shule za Quran Uholanzi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Serikali ya Uholanzi inachukua hatua dhidi ya mashirika yasiyo rasmi ya elimu ya Kiislamu kama vile shule za Qur'an na shule nyingine za kibinafsi ambapo watoto wanaweza kujifunza Kiarabu na Quran. Hii inahusisha safu nzima ya hatua za vikwazo ili kuingilia kati, kufuatilia na kubadilisha mtaala wa elimu ya Kiislamu.

Maoni:

Hatua ya serikali ya Uholanzi kuingilia kati shule, vituo na nyumba zisizo rasmi za Qur'an ambako watoto wa Kiislamu wanafundishwa misingi ya dini yao, inaonyesha kwamba sera ya Uholanzi ya uoanishaji itafuata mtindo wenye misimamo mikali wa Ufaransa. Kwa kutoa mfano: Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron hivi karibuni alifunga misikiti na vituo vya Kiislamu na kuwataka Waislamu waache dini yao na wakubali usekula, demokrasia na kuundwa kwa “Islam wa Ufaransa.” Aliamuru shirika mwavuli, Baraza la Ufaransa la Imani ya Kiislamu (CFCM), kuja na hati ya Uislamu nchini Ufaransa ambayo kwayo wataidhinisha hili. Na kwa bahati mbaya, walitii.

Nyakati za mwenendo na majadiliano ya kifikra ya kuwatongoza Waislamu kuegemea upande wa demokrasia ya kiliberali na kuwashawish kwamba demokrasia ya kiliberali ni “bora” kuliko Uislamu imesukumizwa nyuma. Sasa, mwenendo wa nchi nyingi za Magharibi na Waislamu ni ule wa uliberali wa misuli kupitia kulazimisha fikra za Kimagharibi na kuzuia fikra za Kiislamu. Waislamu katika nchi za Kiislamu wamekumbana waziwazi na uliberali huu wa kutisha. Lakini sasa zimwi hili limewageukia Waislamu wanaoishi katika mujtamaa zao.

Ijapokuwa mikabala yote miwili, ule wa laini na ule mgumu, inapishana baina ya kila mmoja kulingana na wakati wake, mahali pake na dhurufu zake muafaka, kiini cha mwenendo wa nchi za Magharibi kwa Waislamu katika mutjamaa zao umeegemezwa kwenye fikra ya uoanishaji. Madhumuni ya sera hii ni kwamba Waislamu wajioanishe kikamilifu na kubadilishe tafakari yao ya Kiislamu kwa tafakari ya kisekula na hatimaye waondoke kwenye safu ya Uislamu. Uhalisia huu unalazimu ufahamu wa wazi na wa kina wa sera hii ya uoanishaji na ni muhimu mno kwa uwepo wa Waislamu katika nchi za Magharibi. Pia, ni muhimu kufahamu ni maeneo gani sera hii ya uoanishaji inalenga. Haya ni maeneo manne:

Nembo za kujieleza: Nembo na maelezo ya Kiislamu ya muonekano wa Uislamu katika maisha ya umma zimefanywa kuwa na matatizo, kwa mfano: misikiti, minara, mavazi ya kitamaduni kama hijab, jilbaab na niqab. Maelezo haya yote yamechafuliwa sura na kushambuliwa nchini Uholanzi.

Hukmu za Mwenyezi Mungu za Uislamu (ahkaam ash Shari'a): Hukmu za Mwenyezi Mungu za Uislamu na fikra za Kiislamu ambazo zinagongana na ruwaza ya kiliberali ya kisekula, kama vile haki za wanawake, tohara ya wavulana, mahusiano ya mwanamume na mwanamke, uchinjaji halal, ndoa, fahamu ya uchamungu, Ummah, Khilafah na jihad nk zinashambuliwa na kuchafuliwa.

Makundi huru yanayosimama kwa ajili ya Waislamu: Haya ni makundi na asasi zinazosimamia haki za Waislamu na zinazokashifu sera za chuki dhidi ya Uislamu. Mashirika ya aina hii yanachunguzwa, kuzuiwa, kunyamazishwa na kuchafuliwa sura.

Taasisi za Elimu ya Kiislamu: Hizi ni sehemu ambazo Uislamu unafunzwa na shakhsia za Kiislamu zinaundwa ili kitambulisho cha Kiislamu kienezwe na kuhifadhiwa, kama vile misikiti, shule za Quran, shule za lugha ya Kiarabu, elimu ya sekondari na shule za msingi. Haya ndiyo machimbuko msingi ambayo Waislamu hujifunza dini yao na thaqafa ya Kiislamu hupitishwa kutoka kizazi hadi kizazi. Sasa mashirika haya yanalengwa na serikali na kuchafuliwa katika siasa na vyombo vya habari.

Sera hizi zimedhamiria kuwakata Waislamu kutoka katika chimbuko la Uislamu na elimu ya Kiislamu ili kuathiri vizazi vijavyo vya Waislamu. Waislamu lazima waelewe hatari hii kubwa na wanapaswa kuifanyia kazi kama suala la uhai na kifo. Sera ya uoanishaji ni mchakato unaoendelea hatua kwa hatua. Ikiwa Waislamu hawatapambana na kila hatua wanayopiga, hatua moja zitafuata kwa haraka hatua nyingine, mpaka kuwe hakuna kitu kinachobaki.

Sisi Waislamu hatuna budi kuelewa na kufichua kufeli kwa demokrasia ya kiliberali na jaribio lake ovu la kuwapotosha Waislamu kutoka katika Uislamu kupitia kukimbilia kulazimisha fikra, kuingilia nyanja za faragha na kuwekea mipaka mafunzo na utekelezaji wa dini. Huu ni ukandamizaji na alama za tawala za kidikteta ambapo Uislamu uko huru kutokana na dhulma, na una masuluhisho kwa wanadamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahir Uholanzi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu