Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Magharibi inawatakia nini Waislamu kupitia Thaqafa yake wa Kimagharibi?
(Imetafsiriwa)

Habari:

KUN.UZ na tovuti zingine za habari ziliripoti kwamba mnamo Novemba 14-16, Tashkent iliandaa “Kongamano la Pili la Ulimwengu la Malezi na Elimu ya Mtoto Wadogo  (WCECCE).” Akizungumza katika kongamano hilo, Rais wa Uzbekistan, Shavkat Mirziyoyev, alipendekeza kupitisha azimio maalum la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu matokeo ya Kongamano hilo la Kiulimwengu, kuhusu umuhimu wa kuwasomesha watoto, kama jambo muhimu katika kufikia maendeleo ya wanadamu wote. Pia imependekezwa kuasisiwa kituo cha kikanda cha UNESCO huko Tashkent.

Maoni:

Inajulikana vyema kwamba kiongozi wa ukafiri, Amerika na Magharibi, hawasazi juhudi zozote katika kuupiga vita Uislamu na Waislamu kwa njia zote. Njia hatari zaidi yazo ni shambulizi la kithaqafa na kifikra, ambalo ni hatari zaidi kuliko shambulizi la kijeshi. Shambulizi la kijeshi linaua tu mtu kimwili kwenye uwanja wa vita.

Hata hivyo, shambulizi la kithaqafa linamwezesha adui kupenya majumbani na kutia sumu akili za watu hasa akili za vijana na watoto na kuwageuza watumwa watiifu kwake! Wakoloni makafiri hutekeleza mashambulizi haya kupitia mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa na UNESCO ambayo hutumikia maslahi yao kwa usaidizi wa zana zao, watawala vibaraka.

Kutokana na mada ya kongamano hili la Tashkent, ni wazi kwamba watoto wadogo ndio walengwa! Hii ni kwa sababu watoto ndio mustakabali wa Ummah. Na mpango wa wakoloni makafiri ni kuharibu mustakabali wa Ummah huu! Bila shaka, maendeleo ya Amerika na Magharibi, kama yanavyoitwa, yamefungwa kwa karatasi yenye kung'aa yenye misemo yenye kuchachawiza kama vile “ufanisi, maendeleo, na ubora wa elimu...”. Hili linathibitishwa na maneno ya Mirziyoyev kwamba hili ni “sababu muhimu katika kufikia maendeleo ya wanadamu wote.”

Katika kitabu chake “Vita vya Kifikra katika Vita dhidi ya Ugaidi (The Battle of Ideas in the War on Terror),” Robert Satloff, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Washington ya Sera ya Mashariki ya Karibu (WINEP), anazingatia umuhimu wa kujishindia akili za vijana katika Mashariki ya Kati. Vijana katika Asia ya Kati, ikiwemo Uzbekistan, bila shaka hawajatengwa. Hakuna shaka kwamba mashambulizi ya kithaqafa pia yamechukua nafasi yake katika mkakati mpya wa Marekani kwa Asia ya Kati kwa kipindi cha 2019-2025. Kongamano hili la Tashkent linaweza kuchukuliwa kama lenye kufanya kazi ndani ya muundo wa mkakati huu.

Tabia hii kutoka Magharibi inaashiria uchungu wa kifo, wakati Magharibi inapoelekea kifo. Sababu ya hili ni kuporomoka kwa maadili ya kidini, kifamilia, kielimu na kiakhlaqi na nchi kwa nchi za Magharibi. Katika nchi za Magharibi, uzinzi, uavyaji mimba, ulawiti wa jinsia moja na maovu mengine yanachukuliwa kuwa ya kawaida na hata halali! Kwa mfano, tarehe 30 Juni, 2017, bunge la Ujerumani liliidhinisha mswada wa kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja. Wabunge 393 wa Bunge la Ujerumani walipiga kura kuunga mkono kuhalalisha ndoa hiyo! Mfano mwingine wa kuzorota kwa akhlaqi katika nchi za Magharibi ni kwamba gazeti la ‘The Guardian’ lilifuatilia dhulma kadhaa za kingono mikononi mwa wabunge kutoka vyama tofauti, vikiwemo Conservatives na Labour.

Kwa hivyo ni wazi kutokana na hili aina ya maisha ambayo Magharibi inawatakia Waislamu kupitia kuingiza thaqafa yake.

“Mapinduzi ya kingono yameanza kumeza watoto wao,” aliandika Patrick J. Buchanan, mshauri wa marais watatu wa zamani wa Marekani, katika kitabu chake “Kifo cha Magharibi (The Death of the West),” akisisitiza kuporomoka kwa Amerika, Ulaya, na dola ya Kiyahudi. “Takwimu za uavyaji mimba, talaka, kuporomoka kwa viwango vya uzazi, nyumba zenye mzazi mmoja, kujiua kwa vijana, ufyatuliaji risasi shuleni, matumizi ya dawa za kulevya, unyanyasaji wa watoto, unyanyasaji wa wenzi wa ndoa, uhalifu wa ghasia, viwango vya kufungwa gerezani, uasherati, na kushuka kwa alama za mtihani zinaonyesha jinsi jamii hii, ambayo mapinduzi ya kithaqafa yanapanda, inaoza na kufa. Vyumba vitupu vya kuzalia na vyumba vya mapokezi vilivyo jaa nje ya afisi ya daktari wa akili vinashuhudia kwamba hali haiko sawa. Lakini kabla ya thaqafa hii mbovu kuanza njia yake, huenda ikaiangusha Magharibi pamoja nayo.” Anaandika kwa hofu, “Mashoga na wasagaji wameishawishi elimu ya ngono katika shule za taifa letu na mashoga na wasagaji wamechukua udhibiti mpana wa kamati za vitivo katika vyuo vya taifa letu. Mabunge ya dola yamebatilisha sheria dhidi ya ulawiti.” Pia anaandika, “Tangu uamuzi wa Jaji Blackmun, uavyaji mimba milioni 40 umefanywa nchini Marekani. Asilimia thelathini ya mimba zote sasa huishia juu ya meza kwenye kliniki ya waavyaji mimba.”

Huu ni ushuhuda wa mtu kutoka miongoni mwao. Hii ni ncha tu ya mlima wa barafu ya maovu katika nchi za Magharibi! Kwa hiyo nchi za Magharibi, pamoja na thaqafa yake fisadi na ovu, zinataka kuwaburuza Waislamu, hasa vijana na watoto katika dimbwi la maangamivu!

Hivyo basi, wenye ufahamu wa kisiasa, wanasiasa, wanafikra, wasomi, ‘Ulamaa, wanablogu na wazazi lazima watoe tahadhari kuhusu hatari hii. Mwenyezi Mungu (swt) ametuonya kwamba wao kamwe hawatokuwa radhi nasi mpaka tufuate dini yao; kwa hiyo, hakuna kheri yoyote inayoweza kutarajiwa kutoka kwao na thaqafa yao, na kheri na izza viko katika Uislamu pekee. Kama alivyosema Khalifa Umar (ra): كنا أذل أمة فأعزنا الله بالإسلام، ومهما ابتغينا العزة في غيره أذلنا الله “Sisi tulikuwa watu wadhalilifu zaidi katika Ummah, basi Mwenyezi Mungu (swt) akatupa izza kwa Uislamu. Na pinidi tutakapo tafuta izza kwengine badala ya Uislamu, Mwenyezi Mungu (swt) atatudhalilisha.” Kutafuta izza kwengine kando na Uislamu kunaleta udhalilifu tu na tunashuhudia haya kwa uhalisia. Njia pekee ya kubadilisha uhalisia huu mchungu ni kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu. Hili halitapatikana isipokuwa chini ya utawala wa Khilafah Rashida, ambao utasimamishwa hivi karibuni, inshaAllah.

(لِمِثْلِ هَذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ)

“Kwa mfano wa haya nawatende watendao.” [Surah As-Saffat 37:61]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Islam Abu Khalil – Uzbekistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu