Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Imarati Yafungua Mlango Kuuza Pombe

ili Kushajiisha “Uvumilivu” kwa Haram Hiyo

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 3 Januari, 2023, The National iliripoti kwamba Imarati itakuwa ikiondoa ushuru wake wa 30% kwa mauzo ya pombe. Hatua hizo zilielezwa kuwa ni mpango wa kukuza sekta ya utalii na kuimarisha uhamiaji wa msimu wa wageni ambao hushindana na mashirika ya kikanda ambayo yanavutia wageni wasiokuwa Waislamu wanaotafuta starehe katika msimu wa likizo ya kimataifa. Leseni za kunywa pombe pia zitarahisishwa kupata. Watalii wasiokuwa Waislamu wanaweza kupata kibali cha pombe bila malipo kinachotumika kwa mwezi mmoja wanapoingia Imarati.

Maoni:

Uwezeshaji wa vitendo vya Haramu nchini Imarati ni sehemu ya mashambulizi yaliyoratibiwa dhidi ya maadili ya Kiislamu kote duniani. Tunaona jinsi usasa ulivyochafua jamii ya Saudi Arabia kwa kuanzisha vilabu vingi vya usiku, viwanja vya kijamii kwa ajili ya uhuru wa kuchanganyika na kupata vyanzo vya burudani vinavyokuza mitazamo ya kithaqafa dhidi ya Uislamu. Imarati imetumia upataji pombe kuwavutia watalii kuchuma mapato katika eneo hilo. Pia imewezesha kwa njia isiyo ya moja kwa moja uhalalishaji wa Waislamu wa Imarati na Waislamu wa nje kukubali matendo ya ukafiri yanayochukiwa katika ardhi zao. Hii ni chini ya bendera ya uvumilivu na kukubalika kwa utofauti na ushirikishwaji wa mataifa yote. Hata hivyo, kuna kushindwa kuelewa kwamba katika Sharia, hakuwezi kuwa na ulegezaji msimamo katika kuwaruhusu wasiokuwa Waislamu kuwa na mtindo wao wa maisha pale inapoleta madhara katika maisha ya kijamii ya Khilafah na inagongana na maamrisho ya wazi ya Mwenyezi Mungu (swt).

Ndani ya Khilafah, endapo Amir wa Dola ataanzisha sera kama hizo za kukuza maendeleo ya kiuchumi, atastahiki kuondolewa kwenye wadhifa wake. Umma wote utasimama kulaani kupinga sheria za Quran na Sunnah. Urahisishaji wa hivi majuzi wa usambazaji wa pombe ni kipimo cha majaribio ili kuruhusu maovu mengine kuingia kwenye jamii. Sisi kama Waislamu lazima tuwahesabu watawala wetu kwa kuuacha mfumo wa utawala wa Kiislamu na kamwe tusikubali vipimo vya wanadamu juu ya sheria za Mwenyezi Mungu (swt). Hakika, adhabu ya Jahannam inatusubiri endapo tutafanya hivyo!

(وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى ءَامَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنَ السَّمَآءِ وَالاَرْضِ وَلَكِن كَذَّبُوا فَاَخَذْنَاهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ)

“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.” [7: 96]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu