Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kifungo cha Miaka 50 kwa Watuhumiwa wa Ugaidi ni Kushindwa kwa Propaganda ya Vita vya Ugaidi Tanzania

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 16/12/2022, Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Kanda ya Songea, Kusini mwa Tanzania iliwahukumu Waislamu sita akiwemo kikongwe wa miaka 73 kifungo cha miaka 50 jela baada ya kupatikana na “hatia” ya kuendesha vitendo vya kigaidi na kupanga kuiangusha serikali.

Maoni:

Kwa mujibu wa Jaji Yose Mlyambina, washtakiwa hao walikuwa na uhusiano na kundi la kigaidi nje ya nchi wakipanga njama za kuvuruga amani ya nchi na kupindua serikali.

Ni jambo la kusikitisha sana kwamba washtakiwa hawa Waislamu wamedhulumiwa kwa kunajisiwa taratibu za kisheria. Walikamatwa tangu Julai, 2020 na wakawekwa kizuizini kwa miaka takriban miwili na miezi mitano wakisubiri upelelezi. Hii inamaanisha walikamatwa kwanza, baadaye upelelezi ukafuatia. Zaidi ya hayo, Waislamu hawa walinyimwa haki zao za msingi kama uwakilishi wa kisheria, kutembelewa na ndugu, kupelekwa sehemu zisizojulikana na kulazimishwa kuweka sahihi katika nyaraka za kisheria.

Katika hukumu hii, ni jambo linalotia shaka kuamini kuwa familia ya wanakijiji sita wasio na silaha wanaweza kuipindua serikali yenye zana zote za kijeshi ambayo ipo Dodoma zaidi ya km 700 au Dar es Salaam ambayo ni zaidi ya km 900 kutoka Songea walipokuwa wanaishi washtakiwa. Je, ni kweli serikali ya Tanzania inaweza kupinduliwa na kikundi cha wanakijiji sita ndugu wasio na silaha? Sote tunajua jambo hili haliwezekani.

Kiuhalisia, hukumu haioneshi chochote isipokuwa uovu wa propaganda chafu iliyolazimishwa na Wamagharibi ya vita vya ugaidi nchini Tanzania. Pia hukumu hii inaonesha imelengwa kuwa chachu ya amsha amsha ya kampeni ya vita vya ugaidi kufuatia hatua za Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai kufutilia mbali kesi kadhaa za “ugaidi” akikiri kuwa zimekosa ushahidi thabiti wa kuendelea nazo.

Katika kesi zote za ugaidi kuna maswali ya msingi huibuka, mfano: Kwa nini watuhumiwa hawapewi haki ya kusikilizwa kesi zao kwa muda muwafaka? Kwa nini watuhumiwa ambao sheria inawahesabu hawana hatia hawapewi dhamana? Kwa nini huwa kunakuwa na hali ya vitisho na udhalilishwaji (wa watuhumiwa) katika kesi za aina hii? Na muhimu zaidi, ni kwa nini watu hukamatwa kwanza, na kuwekwa kizuizini kwa miaka mingi ilhali waendesha mashtaka hukiri kuwa upelelezi bado unaendelea, wakimaanisha bado hawana ushahidi wa kuwatia watuhumiwa hao hatiani hata baada ya miaka mingi? Haya yote ni hali inayodhihirisha uwepo wa ajenda ya wazi ya kuwadhulumu (watuhumiwa) kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi huku kukiwa na ukiukwaji wa haki msingi za kiutu.

Hakika vita vya ugaidi ni nyenzo inayotumiwa na Wamagharibi Mabepari kunyonya nchi zinazoendelea na kuingilia mifumo ya ulinzi na usalama ya nchi hizo kupitia kuwahonga fedha watawala wa nchi hizo kwa jina la fedha za kupambana na ugaidi. Kama ilivyowahi kusemwa mwaka 2016 na aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump kuwa waliounda kikundi cha kigaidi cha ISIS ni Barrack Obama na Hilary Clinton.

Ni muda muwafaka sasa kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kukomesha ubepari na sheria yake (kandamizi) ya Kuzuia Ugaidi ambayo si tu imejidhihirisha kuwa ni ya kikoloni na yenye ajenda ya nje, bali pia inalenga kundi moja tu la watu katika jamii (yaani Waislamu). Badala yake waunge mkono mfumo mbadala wa Uislamu ambao una haki na uadilifu kwa watu wote.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzani

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu