Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jumuiya Saliti ya Waarabu Yafungua Mlango Kuruhusu Utawala wa Syria kuingia kwenye Kundi lao

(Imetafsiriwa)

Habari:

Miaka 12 baada ya ghasia nchini Syria, Jumuiya ya Waarabu yakaribia kuukubali utawala wa Syria kuregea katika kundi la shirika hilo. Hili limeidhinishwa haswa na tawala za Saudia na Imarati, ambazo zimeshinikiza shirika hilo kuirudisha serikali ya Syria. Tawala hizi mbili zinasemekana kuwa na nia ya kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya Syria.

Maoni:

Baada ya miaka 12 ya uchinjaji na mauaji ya Waislamu nchini Syria, na miaka 12 ya uasi uliobarikiwa katika nchi hiyo, jumuiya saliti ya makhaini, ile inayoitwa Jumuiya ya Waarabu inaukumbatia utawala wa Syria baada ya kuuondoa kwenye jumuiya hiyo pale Bashar al-Assad alipoanza kuwafanyia unyama Waislamu nchini Syria. Mamia ya maelfu wameuawa na mamilioni wamelazimika kuyahama makaazi yao. Kwa msaada wa Wamarekani na vibaraka wao wapiganaji miongoni mwa tawala za Iran na wanamgambo tofauti tofauti, na vile vile tawala zilizovuruga na kujipenyeza katika mapinduzi ya Syria, utawala wa wahalifu wa Syria umesalia madarakani kwa njia ya bandia na kwa muda. Huu ni uthibitisho mwingine wa uadui wa tawala hizi kwa Ummah. Utawala wa Syria pamoja na tawala za Kiarabu ni vikaragosi vya Marekani na Magharibi. Wamewekwa kwa ajili ya kutumikia tu maslahi ya dola za kikoloni na kukandamiza maslahi na mahitaji ya nchi za Kiarabu na Waislamu.

Mazungumzo yoyote kuhusu muungano huu wa wasaliti wanaotetea haki za binadamu au kutumikia maslahi ya mataifa ni uongo na unafiki wa kuubakisha mfumo wa kikoloni mahali pake, hata kama itamaanisha kuhamishwa na kuuwawa kwa mamilioni ya Waislamu ambao wamekuwa na ujasiri mkubwa na kutoogopa kusimama dhidi ya madhalimu wakati wa uasi katika nchi za Kiarabu. Njia pekee ya kuuondoa utawala wa Syria, Jumuiya ya Waarabu na mshiko wa kikoloni kwenye ardhi zetu, Ummah wetu na rasilimali zetu ni kuungana chini ya Khalifa muongofu atakayetabikisha Uislamu na kuilinda Dini yetu, ardhi zetu, utajiri wetu, na kuupa Umma mamlaka juu ya ardhi zake.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Younes Piskorczyk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu