Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Gesi ya Bahari Nyeusi ni Mali ya Umma Inapaswa Kutumika kama Ilivyoamrishwa na Uislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Gesi ya Bahari Nyeusi, iliyogunduliwa katika uwanja wa gesi wa Sakarya na ni mojawapo ya miradi muhimu ya nishati katika historia ya Uturuki, ililetwa ufuoni kwa mara ya kwanza kwenye Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Filyos. Gesi asilia iliyozalishwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo, ambapo zaidi ya wafanyikazi elfu 8 wanafanya kazi ardhini na elfu 2 baharini, iliagizwa kwa ushiriki wa Rais Recep Tayyip Erdogan. Erdogan, katika hotuba yake katika "Sherehe ya Uzinduzi wa Gesi ya Bahari Nyeusi", alisema kuwa pamoja na mradi huu, sio tu utegemezi wa kigeni wa nchi juu ya gesi asilia umepungua kwa kiasi kikubwa, lakini pia eneo la Filyos na Zonguldak linageuzwa kuwa kambi ya kawi, teknolojia, usambazaji muhimu. (TRT News, 20/04/2023)

Maoni:

Utajiri alioujaalia Mwenyezi Mungu (swt) katika ardhi za Umma wa Kiislamu hauishii kwenye kuhesabiwa. Gesi ya Bahari Nyeusi iliyogunduliwa katika uwanja wa gesi wa Sakarya ni mojawapo ya utajiri huu. Kwa hiyo, kwa kuwa ni rasilimali ya Kiislamu, ugunduzi wa utajiri huu ni muhimu sana na wa thamani, bila kujali ni katika eneo la Uturuki, baharini au nchi kavu. Kwa sababu kawi inamaanisha nguvu na utajiri. Kama alivyotajwa katika hotuba yake, Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Marekani Henry Kissinger, "Dhibiti mafuta na utayadhibiti mataifa; dhibiti chakula na utawadhibiti watu..." Rasilimali za kawi ni utajiri muhimu sana unaozifanya dola zenye kawi kuwa bora kuliko dola nyenginezo, hasa zile ambazo ni maadui.

Inapaswa pia kusisitizwa kuwa ni mafanikio muhimu ambayo Uturuki imefikia hili katika miaka 3, wakati makampuni makubwa ya kawi duniani yamefanya hifadhi ya gesi iliyogunduliwa kutumika tu katika miaka 5-6. Ni muhimu kushiriki mafanikio haya na umma kwa njia ya uwazi na inayoeleweka. Kwa njia hii, aina yoyote ya udanganyifu huzuiwa.

Suala jengine ni iwapo kiasi cha akiba kilichogunduliwa kitatosha kukidhi mahitaji ya gesi ya Uturuki. Hapo awali ilitangazwa kuwa kiasi cha gesi kilichogunduliwa na mamlaka za serikali kimefikia jumla ya mita za ujazo bilioni 710. Kwa mara nyengine tena, kwa mujibu wa taarifa za mamlaka, mita za ujazo milioni 10 za gesi kwa siku na mita za ujazo bilioni 3.5 kwa mwaka zitatolewa kutoka kwa hifadhi ya Bahari Nyeusi. Kwa kuzingatia kwamba kiwango hiki kitaongezeka kwa mara 3-4 na visima vipya vilivyochimbwa, inamaanisha kuchimba mita za ujazo bilioni 15 za gesi kwa mwaka.

Matumizi ya gesi ya Uturuki ni karibu mita za ujazo bilioni 60 kwa mwaka. Kwa mujibu wa data ya Bodi ya Usimamizi wa Soko la Kawi (EMRA), Uturuki iliagiza takriban mita za ujazo bilioni 58.704 za gesi asilia mwaka 2021. Kati ya hizi, asilimia 44.87 ilichukuliwa kutoka Urusi, huku kiasi kilichobaki kikichukuliwa kutoka Iran, Azerbaijan na Algeria. Kwa njia hiyo hiyo, kulingana na data ya EMRA, Uturuki ilitumia mita za ujazo bilioni 59 za gesi asilia mwaka 2021. Kulingana na akaunti hii, wakati gesi ya Bahari ya Black inafikia uwezo kamili, inaweza kukidhi 25% tu ya mahitaji yetu ya kila mwaka. Bila shaka, ni bora zaidi kuliko kukosa kabisa. Lakini katika hali hii, kusema kwamba gesi ya Bahari Nyeusi itasafirishwa kwa nchi zinazoongoza haimaanishi chochote isipokuwa tu kujipa umaarufu kabla ya uchaguzi.

Ingawa tunasema "kazi nzuri" kwa gesi ya Bahari Nyeusi, takwimu hizi zinaonyesha kwamba tunahitaji kufanya kazi kwa uvumbuzi mpya wa gesi kwa sababu ni muhimu kupunguza uagizaji wa kawi ili kupata uhuru wa kisiasa na kiuchumi.

Kilicho muhimu zaidi kuliko haya yote ni kuwa na mfumo ambao utatumia mali ya Ummah kwa usahihi na kwa ufanisi. Bila shaka mfumo huo ni Uislamu. Kama Uturuki na nchi nyingine za Kiislamu, tunaweza tu kulinda utajiri wetu na kuuendeleza kwa kutekeleza mfumo wa Kiislamu. Ni mfumo wa Kiislamu pekee ndio unaoweza kuregesha utajiri wetu wote, wa zamani na mpya, ulioibwa na makafiri wakoloni.

Kwa mujibu wa mfumo wa Kiislamu, rasilimali za kawi ni mali ya umma; kwa maana nyengine, kwa Ummah. Kamwe hairuhusiwi neema hizi kuhamishwa kwa makampuni ya kibepari na makampuni ya kimataifa ya kigeni kuwa na hisa katika hifadhi hizi kwa sababu haki ya kutumia neema hizi ni ya umma. Neema hizi zinapaswa kuwa huru sio tu wakati wa uchaguzi, lakini wakati wote. Wasimamizi hawana haki ya kuzuia neema hizi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ فِي الْكَلَأِ وَالْمَاءِ وَالنَّارِ»

“Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: katika malisho, maji na moto.” (Abu Dawud)

Hivyo basi, kazi ya watawala sio kuzifanya neema ambazo tayari ni za umma kuwa nyenzo za uchaguzi, bali ni kuzitumia kwa jinsi Uislamu unavyoelekeza, kujaribu kufukua hifadhi mpya hadi mahitaji yote ya watu yatimizwe.

Kwa kuongezea, jitihada za utafutaji zinapaswa kuharakishwa sio tu katika Bahari Nyeusi, bali pia katika Mediterania. Ni haki yetu ya kihistoria kuwa na kiasi kikubwa cha akiba ya mafuta na gesi asilia iliyothibitishwa katika bahari ya Mediterania. Ili kuepusha mivutano ya kisiasa na nchi za eneo hilo, shughuli za utafutaji zilizopungua zinapaswa kuanzishwa upya na shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia zinapaswa kufanywa katika bahari za kimataifa kwenye rafu ya bara la Uturuki na Cyprus. Upunguzaji kasi wa shughuli za utafutaji mafuta na gesi asilia ufanyike. Katika hatua hii, jambo pekee linalopaswa kuzingatiwa ni maslahi ya Waislamu, sio Marekani au Ulaya.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Emin Yildirim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu