Jumatatu, 16 Muharram 1446 | 2024/07/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vijana wa Kashmir wanapotea katika Giza la Uraibu wa Madawa ya Kulevya bila Nuru ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 5 Juni, BBC iliripoti juu ya "ongezeko la kutisha la matumizi mabaya ya dawa za kulevya huko Kashmir". Wajana wa kiume zaidi na zaidi wanaweza kupatikana nje ya kituo pekee cha kutibu uraibu katika eneo la Kashmir linalosimamiwa na India, wakiwa kwenye foleni na wazazi wao kupokea dawa kutoka kwa Taasisi ya Afya ya Akili na Sayansi ya Nyuroni (IMHANS) ili kusaidia kupunguza dalili zao za kujiondoa katika uraibu na kuzuia maambukizi ya magonjwa ya kuambukiza. Mnamo Machi, waziri wa serikali hiyo ya majimbo aliliambia bunge kwamba karibu watu milioni moja katika Jammu na Kashmir - karibu 8% ya wakaazi wa eneo hilo - wanatumia dawa za aina fulani, ikiwemo bangi, opioids au sedative. Wataalamu wanahusisha hili na mambo kadhaa, ikiwemo uhaba wa kazi na masuala ya afya ya akili yanayotokana na kuishi katika eneo la mzozo.

Maoni:

Wataalamu wanaochanganua hali hiyo wanahusisha ukuaji huu kutokana na mambo kadhaa, ikiwemo uhaba wa kazi na masuala ya afya ya akili yanayotokana na kuishi katika eneo la mzozo. Kuna wanawake ambao wanazidi kukwama ndani ya mizunguko ya uraibu na hii ina athari za kutia wasiwasi kwa mustakabali wa muundo wa familia na watoto wa eneo hilo.

Ufisadi na ushirikiano wa utekelezaji wa sheria na wafanyibiashara wa dawa za kulevya pia ni tatizo kubwa eneo ambalo tayari linakabiliwa na hali ya machafuko ya kisiasa na vita kati ya India na Pakistan.

Tiba ya jinamizi hili la maradhi ya kijamii ni mfumo thabiti na wenye nguvu unaoondoa uhuru wa wahalifu kuendesha nchi, wakiwemo wanasiasa wa kitaaluma wenye maslahi binafsi kama nia yao pekee ya kutaka madaraka.

Madawa ya kulevya na ulevi ni haram na hakuna nafasi ya matumizi ya "burudani" kama ilivyojadiliwa katika Quran;

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالأَنصَابُ وَالأَزْلاَمُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ]

“Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.” [Al-Maidah: 90].

Adhabu kali ya ulanguzi wa madawa ya kulevya na unywaji wa madawa ya kulevya itatekelezwa ndani ya Khilafah pamoja na mfumo wa elimu mpana unaofundisha uzalishaji na Iman. Mfumo wa uchumi pia utaondoa matatizo ya kiuchumi ya ukosefu wa ajira na sera za umaskini zilizopo kutokana na usimamizi duni wa eneo hilo.

Rasilimali chache za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO) yanayofanya kazi katika eneo hilo si lolote ila ni bendeji tu kwenye saratani ya kuishi bila Dini changamfu ya Uislamu maishani.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu