Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Erdogan Alishinda Uchaguzi na Kuregea Madarakani, Lakini vipi kuhusu Uislamu!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Baraza Kuu la Uchaguzi (YSK) lilitangaza matokeo ya mwisho ya raundi ya pili ya uchaguzi wa rais uliofanyika nchini Uturuki Mei 28. Kufuatia hayo, mgombea wa Muungano wa Wananchi na Rais Recep Tayyip Erdogan alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 52.18 ya kura. Kemal Kilicdaroglu, mgombea wa Muungano wa Kitaifa, alipata asilimia 47.82 ya kura. Rais Erdogan atasalia madarakani kwa miaka mingine 5 hadi uchaguzi ujao. (Mashirika)

Maoni:

Rais Erdogan alishinda uchaguzi wa Uturuki, ambao umesababisha mvutano mkubwa na mgawanyiko katika jamii tangu tarehe ilipoamuliwa, licha ya mgogoro wa kiuchumi uliokuwepo nchini humo na athari mbaya za matetemeko makubwa ya ardhi yaliyotokea Februari 6. Ushindi wa uchaguzi huo ilifuatiwa na sherehe za shangwe katika baadhi ya nchi za Kiislamu na nchi za Ulaya, hasa za Waislamu nchini Uturuki waliompigia kura Erdogan. Upinzani, kwa upande mwingine, ulivunjika moyo sana.

Hakuna shaka kwamba jambo muhimu zaidi katika ushindi wa Erdogan ni ukweli kwamba sehemu ya Waislamu wa kihafidhina, ambayo ni uti wa mgongo wa jamii ya Kituruki, imemuunga mkono katika kila uchaguzi kwa motisha za Kiislamu, na kuacha kando vigezo vyengine vyote. Hii ni kwa sababu mpinzani mkuu wa Erdogan, Chama cha Wananachi cha Kijamhuri (CHP), ni chama kilichosajiliwa chenye chuki dhidi ya Uislamu. Ukatili uliofanywa na CHP dhidi ya Waislamu bado uko wazi katika kumbukumbu. Kwa sababu hii, Waislamu wa Uturuki hawajawahi kamwe kuifikiria CHP, mbunifu wa fikra ya kisekula ya Kikemali, fursa ya kutawala peke yake.

Kwa kufahamu hili, Erdogan na chama chake wameashiria kauli mbiu ya nchi na taifa kwa kuchochea hisia za Kiislamu katika mchakato mzima wa uchaguzi. Aliendesha kampeni ya upatilizaji fursa, akidai kwamba anapokea maagizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na taifa, huku wapinzani wake wakipokea kutoka kwa nchi za kimagharibi zenye chuki na Uislamu na mashirika ya kigaidi kama vile PKK. Vile vile wanazuoni wanaomuunga mkono Erdogan na viongozi wa maoni waliendelea kueneza dhana iliyojengeka kwamba iwapo Erdogan atashinda, Palestina, Umma na watu wote wanaodhulumiwa kote duniani watashinda. Waliwalingania Waislamu kwenye sanduku la kura la kidemokrasia kana kwamba wanawalingania kwenye jihad. Mwishowe, hisia za Kiislamu miongoni mwa Waislamu zilishinda mijadala na ahadi zote za upinzani na kumrudisha Erdogan kwenye ushindi.

Lakini je, kweli Rais Erdogan anawakilisha Waislamu wanaomuunga mkono? Je, anatimiza matakwa na matarajio ya Waislamu ambao wanaona karibu kila uchaguzi ni mapambano kati ya haki na batili? Je, anapigania utukuzaji wa haki na uangamizaji wa batili? Kwa ufupi, Erdogan anaposhinda, je Uislamu na Waislamu kweli wanashinda?

Hili ndilo suala kuu. Kila Muislamu mwenye akili timamu na moyo wa imani anapaswa kuzingatia nukta hii. Kama vile alivyoshughulishwa wakati akishiriki katika uchaguzi, anapaswa kujishughulisha na manufaa yote ya kimada baada ya uchaguzi na kujiuliza, "Ni nini kimebadilika katika suala la kuunda maisha ya Kiislamu?" Anapaswa kufikiria kuhusu maneno mazuri ya Khalifa Umar ibn Abdulaziz, ambayo yametoa mwanga juu ya zama zilizopita na za sasa. Kwani alisema: “Dola haipo kwa ajili ya kupata pesa, bali kuwaongoza watu kwenye njia ya haki (iliyo njema, ya kweli na nzuri).”

Ndiyo, ni nini kimebadilika? Je, Jamhuri ya Uturuki, ambayo Erdogan ameitawala kwa miaka 21, imeweza kuwafanya watu wetu kuona njia ya haki? Je, imeweza kuwaokoa watu wake kutokana na dhambi na dhulma na kuyafanya maisha ya dunia yao na akhera kustawi? Kwa mfano, je, ubwana ambao ni wa Mola Mlezi wa walimwengu wote umerudishwa kwa mmiliki wake? Je, ni maovu yapi aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu, kama vile unywaji pombe, riba, kamari, uzinzi, uasherati n.k, ambayo yanavifisadi vizazi, yameharamishwa? Je, kuna kazi yoyote iliyofanywa kuzuia uhalifu milioni 5 unaotendwa nchini Uturuki kila mwaka? Je, urafiki na dola za kikafiri za kimagharibi zinazoshambulia Uislamu kwa chuki kubwa nyoyoni mwao umemalizwa?

Je, kuna suluhisho lolote la Uislamu kwa matatizo ya watu wetu wanaoishi katika migogoro lililotekelezwa? La kusikitisha, hakuna hata moja ya haya ambayo yamefanywa. Wala litafanywa maadamu jamhuri ya kisekula ya Kimagharibi, ambayo kigezo chake pekee ni maslahi binafsi, angalipo. Kwa hakika, bango kubwa la Mustafa Kemal lililotundikwa kwenye ikulu ya rais baada ya ushindi wa Erdogan katika uchaguzi, ni waraka wa mfano wa jinsi Waislamu wanavyodanganywa.

Kwa hivyo, Uislamu haujashinda, wala hakuna ushindi wa kweli wa kusherehekea. Wapo Waislamu waliodanganywa na taaluma ya uhandisi na uchaguzi ukashinda kwa gharama yao. Lakini hii haina maana kwamba Waislamu wataendelea kudanganywa. Kwa sababu Waislamu hawakuipigia kura demokrasia ambayo Erdogan ameitetea, bali mijadala ya Kiislamu ambayo ameitumia kama chombo cha utumiaji watu. Kwa maana hii, ushindi wa Erdogan ni ushindi wa kirongo uliopatikana kwa kushindwa. Na zama za demokrasia na wapambe wake zitafikia kikomo katika sehemu ya kwanza ya msukosuko katika njia ya kuzikonga nyoyo za Waislamu kwa wabebaji da’wah waaminifu kwa Uislamu ambao wanafanya kazi kubwa sana kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida. Hatimaye, utawala wa Erdogan ni wa kufa, huku mapenzi kwa Uislamu katika nyoyo za Waislamu yatadumu hadi Siku ya Kiyama. Hivyo basi, mapenzi kwa Uislamu ndani ya nyoyo za Waislamu yatabadilika punde au baadaye kuwa mapinduzi ya fikra na kuuleta Uislamu wenyewe madarakani. Kisha karne ya Uturuki itakuwa karne ya Uislamu na Khilafah.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُالرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum-4-5]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammed Emin Yıldırım

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu