Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mzigo wa Fedha

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kenya: Baada ya mswada wa fedha kupitishwa na kutabanniwa na Serikali, sera ya ushuru ilinyanyua kwa kiasi kikubwa wigo wote wa uchumi. Kutabanniwa huku kumezalisha upinzani mkali na hasa wenye utata kuhusu ongezeko la ushuru la 8% kwenye bidhaa za mafuta, ushuru wa nyumba wa 1.5% kwenye mapato, pia ushuru wa 1.5% ya kwa maudhui ya kidijitali na mengi zaidi.

Maoni:

Upinzani kutoka kwa Azimio la Umoja na wanaharakati wengine binafsi umeishia tu kupinga kutabanniwa bila ya kuwasilisha badali yoyote, kuashiria kufilisika kwa mfumo wa kibepari katika kuwaondolea watu mzigo huu mkubwa wa fedha. Kwa upande mwengine upinzani wa kisiasa unakosa ikhlasi katika kupigania maslahi ya watu bali unapigania tu umaarufu wa kisiasa pekee.

Utozaji ushuru kama chanzo kikuu cha mapato ya Dola yoyote ya Kibepari unaiacha serikali ya Kenya Kwanza bila chaguo lolote hasa baada ya deni kubwa la taifa kufikia karibu 70% ya Pato la Taifa. Baya zaidi mali zote za umma kama vile umeme, mafuta nk, zinamilikiwa na mashirika ya kibinafsi ambayo lengo lake ni kupata faida kutokana na mateso ya wananchi. Ushuru wa juu na ubinafsishaji wa mali za umma umefanya bili za matumizi ya umma kuwa mzigo wa kifedha bila huruma hata kidogo.

Utozaji ushuru kwa dhati huvunja moyo uzalishaji, suluhu ambayo ubepari ndio huiamini kutokana na uhaba wa rasilimali. Hili linazua swali kwa nini kulitoza ushuru suluhisho la uchumi ambalo ndilo msingi wa riziki? Dosari zilizo katika mfumo huu zinaufanya ushindwe kusimamia mambo ya watu. Kwa nini kutoja ushuru mapato ambayo yamefanyiwa kazi kuchangia Pato la Taifa? Jibu ni rahisi kwamba mali zote za umma zimebinafsishwa na kuwaacha raia chini ya huruma ya mashirika ambayo lengo lao pekee ni FAIDA.

Licha ya kuwa utawala wa Kenya Kwanza unaamini, ukusanyaji mkubwa wa kodi ndio suluhu, matokeo yake ni tofauti na matamshi ya kisiasa kwani ukosefu wa ajira utaongezeka, umaskini utaongezeka pia kushindwa kulipa mikopo pia kutaongezeka kwani mzigo wa fedha utafanya iwe vigumu kwa watu binafsi kulipa deni. Natija yake hili litapelekea kupotosha soko la mitaji kwani wengi wataficha pesa katika akaunti zilizofungwa hadi muda maalum (fixed deposit)  badala ya kuwekeza kwenye soko hilo. Miamala ya kibiashara kama nukta ya uchumi itapungua, wengi watarekebisha matumizi ili kufikia misingi na malipo ya bili kubwa za matumizi.

Uislamu, rehema kutoka kwa Muumba wa mwanadamu, uhai na ulimwengu, unasimama kama uthibitisho wa kihistoria wa jinsi wanadamu walivyoinuliwa kutoka kwenye minyororo ya utumwa wa riba na maumbo ya kisiasa ya zama zao hadi kwenye jamii yenye utendaji wa hali ya juu ambayo iliondoa umaskini na kufanya utafutaji riziki kuwa wenye kupatikana kwa urahisi bila kizuizi kutoka kwa Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume lakini badala yake ukawa msahilishaji mkuu wa kufikia riziki yenye heshima.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[مَّا أَفَاء اللَّهُ عَلَى رَسُولِهِ مِنْ أَهْلِ الْقُرَى فَلِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَى وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاء مِنكُمْ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ]

“Mali aliyo leta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri, ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Quran 59:7].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Omar
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu