Jumapili, 15 Muharram 1446 | 2024/07/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mgogoro wa Afya ya Akili kwa Vijana nchini Uingereza

(Imetafsiriwa)

Habari:

Rekodi ya watoto na vijana milioni 1.4 walitafuta usaidizi wa NHS kwa matatizo ya afya ya akili mwaka jana.

Ufichuzi huo ulizua wasiwasi kwamba msukosuko wa afya ya akili unaweza kuwa "kawaida mpya" kati ya walio na umri wa chini ya miaka 18.

Wasiwasi juu ya pesa ndio sababu maarufu zaidi kwa nini vijana (58%) wanapata madhara kwa afya yao ya akili.

Data tofauti iliyokusanywa na shirika la misaada la ‘Young Minds’ inaonyesha kuwa sababu kuu za wazazi kupiga simu kwa laini yao ya usaidizi ni kwamba mtoto anapambana na wasiwasi, kujidhuru, hasira au uchokozi, matatizo ya shule, ikiwemo ukosefu wa uhudhuriaji, na kudhibiti tabia.

Vijana huwa hawapati usaidizi wanaohitaji kutoka kwa huduma za afya ya akili ya mtoto na vijana, huku wengine wakikataliwa matibabu kabisa. (Gazeti la The Guardian)

Maoni:

Uingereza haina vifaa vya kukabiliana na migogoro ya afya ya akili kwa vijana. Kama jumuiya ya kiliberali ya kilimwengu ambayo imepitisha na kukuza kiwango cha kutamani zaidi na kupenda mali zaidi kwa ajili ya furaha, haishangazi kwamba uwepo wa wasiwasi unapatikana kwa wingi.

Hali ya usalama ambayo vijana walilelewa kuitegemea imepita. Utulivu wa kifedha ni jambo la zamani sasa ambapo mfumo wa uchumi wa ubepari unafichuliwa kuwa hauwezi na umeoza hadi msingi. Serikali haiwezi kuwaangalia raia wake, na kila mtu anajua.

Sura ya mamlaka ya kimaadili imefichuliwa kama uwongo. Sera ya mambo ya nje ni dhahiri inalenga kuhudumia ulafi wa kipote cha wachache; yote yakihalalishwa kwa visingizio hafifu vya kinafiki.

Hata usalama katika utambulisho wa mtu mwenyewe unatiliwa shaka sana leo, huku uonevu wa waziwazi ukitumika kunyamazisha mtu yeyote anayesubutu kutumia akili yake kuhoji mfumo potofu iliolazimishwa.

Jamii ya namna hii ambayo haina msingi madhubuti wa kiakili kwa ajili ya imani na maadili yake, na ambayo imekejeli dini zote na mambo ya kiroho hadi kukataliwa waziwazi, haina msingi wa kujenga shakhsiya za kizazi kijacho. Vijana wametelekezwa kwa mustakabali tasa (dystopian), ingawa mustakabali huo ni sasa.

Uislamu haukubali malengo hayo ya kimada katika maisha. Hauwapambanishi wazee dhidi ya vijana katika vita vya kuporomoka kwa maadili. Uislamu hauwatelekezi watu kwenye mashaka na kutokuwa na uhakika wa fikra za kimada. Uislamu unajenga shakhsiya za vijana kwenye msingi thabiti: Aqidah ya Kiislamu.

Uislamu unafafanua dori ya mwanadamu, dori za wanaume na wanawake, misheni ya vijana, maana ya uwajibikaji wa kibinafsi na wa pamoja, na mtazamo sahihi kwa mambo yaliyo nje ya udhibiti wetu.

Bila kufikiri hivyo kwa uwazi jamii za Magharibi zinatumbukia katika migogoro mirefu zaidi ya afya ya akili ambayo serikali haina uwezo, na sasa haitaki, kuwajibika, sembuse kurekebisha.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Yahya Nisbet

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Mzigo wa Fedha Na Madhara Yanaendelea... »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu