Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kanuni Sawa za Kiraia na Ukandamizaji wa Wanawake wa Kiislamu nchini India

(Imetafsiriwa)

Habari:

Chama tawala cha India, Bharatiya Janata Party (BJP), kimependekeza Kanuni Sawa za Kiraia (UCC) chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Narendra Modi.

Maoni:

Nchini India, wanawake wa Kiislamu kwa mara nyingine tena wanakuwa walengwa wa ajenda ya kisiasa ya chama tawala cha Bharatiya Janata Party (BJP) chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Narendra Modi. Pendekezo la Kanuni Sawa ya Kiraia (UCC) si chochote zaidi ya jaribio jipya la kudhibiti zaidi maisha ya wanawake wa Kiislamu na kuzuia desturi zao za Kiislamu.

UCC, iliyopendekezwa na BJP na makundi ya Mabaniani wenye itikadi kali, inalenga kutekeleza Kanuni Sawa ya Kiraia ambayo inajumuisha mkusanyiko wa sheria zinazosimamia masuala ya kibinafsi kama vile ndoa, talaka, kuasili mtoto (adoption), urithi kwa raia wote wa nchi, kwa kuzingatia mila za Kibaniani.

Jamii ya Waislamu nchini India imekabiliwa na ubaguzi na ukandamizaji mkali kwa karne nyingi. Kwa kutekelezwa kwa UCC, sheria za kibinafsi zinazosimamia haki za familia za Waislamu zitakomeshwa, huku sheria za kimila na matambiko ya za makabila ya Kibaniani zitathibitishwa tena. Hili si lolote zaidi ya jaribio la kufuta kitambulisho na mila za Kiislamu na kuwaingiza Waislamu katika mila kuu za Kibaniani zinazolazimishwa na serikali.

BJP na ajenda yake ya kitaifa ya Kibaniani daima imekuwa ikilenga kuwatenga Waislamu nchini India. Wamewasilisha UCC kama suluhisho la matatizo yanayodaiwa ndani ya jamii ya Kiislamu, kama vile ndoa za wake wengi na talaka. Hata hivyo, ndoa za wake wengi sio mila iliyoenea miongoni mwa Waislamu, kama inavyothibitishwa na takwimu za Utafiti wa Kitaifa wa Afya ya Familia wa 2006.

Ni wazi kwamba UCC haijaundwa "kuwawezesha wanawake wa Kiislamu," kama baadhi ya wafuasi wanavyodai. Badala yake, ni chombo kilicho mikononi mwa wazalendo wa Kibaniani kuwakandamiza wanawake wa Kiislamu na kuwalazimisha kufuata mila za Kibaniani zilizoingizwa katika sheria ya kitaifa.

Zaidi ya hayo, BJP kihistoria imemtumia "mwanamke wa Kiislamu" kama kitovu cha mradi wake wa ukuu. Kwa kujenga taswira ya wanaume wa Kiislamu kama tishio kwa taifa hilo la Kibaniani, wamejaribu kuimarisha udhibiti wa jamii ya Kiislamu na kuwaonyesha wanawake wa Kiislamu kama wahanga wasiojiweza wanaohitaji uokozi. Inaonekana kana kwamba wametabanni mbinu hizi za ukandamizaji na za kupotosha kutoka kwa wenzao wa Magharibi.

Matarajio ya siku za usoni kwa Waislamu nchini India ni ya kutisha. Mashambulizi haya yanayoendelea dhidi ya jamii ya Kiislamu na kitambulisho chake cha kitamaduni yatazidishwa tu. Kimya cha viongozi katika ulimwengu wa Kiislamu pamoja na wanazuoni wafisadi wanaopotosha ukandamizaji wa madhalimu dhidi ya Waislamu utawatia tu moyo washirikina hawa. Watu kama Sheikh Al-Issa, mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu, hivi majuzi alitembelea hekalu la Kibaniani nchini India na kusifu nchi hiyo kama mfano mzuri wa umoja ndani ya utofauti. Alidai kuwa Waislamu nchini India wanajivunia katiba ya India na akasifu kujitolea kwa Modi katika ukuaji wa uchumi jumuishi. Hata hivyo, Al-Issa alishindwa kuelezea ongezeko la ghasia dhidi ya Waislamu, ubaguzi na sera za chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.

Suluhisho pekee kwa Waislamu nchini India na kwengineko duniani ni kuunganishwa tena kwa Umma wa Kiislamu chini ya uongozi mmoja wa kisiasa: Khilafah Rashida. Hapo tu ndipo tunaweza kuutabikisha Uislamu na kuulinda, tukihakikisha kwamba utu, heshima na damu ya Waislamu vinaheshimiwa na kulindwa.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uholanzi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu