Jumapili, 27 Jumada al-awwal 1445 | 2023/12/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Watoto Wauwa Watoto: Shutma Kali kwa Thaqafa ya Kiliberali

(Imetafsiriwa)

Habari:

Siku nyingine, mauaji mengine tena ya kijana na tineja katika barabara za London. Mnamo tarehe 27 Septemba, Elianne Andam wenye umri wa miaka 15, alipigwa risasi na kuuawa kwenye kituo cha basi mchana peupe nje ya kituo cha biashara kilichoko na shughuli nyingi huko Croydon, London alipokuwa akienda shule. Kijana wa miaka 17, ambaye anafikiriwa kujuana naye, ameshtakiwa kwa mauaji yake. Hii ni moja tu ya wimbi la mauaji ya vijana yanayotokana na vijana ambayo yanaisibu Uingereza. Siku 2 tu baadaye, mvulana wa miaka 16 alipigwa vibaya huko Luton. Wavulana watatu matineja wamekamatwa kwa mauaji yake. Ilifuatiwa na kudungwa kisu kwa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 17 huko Brighton mnamo Oktoba 5. Kijana wa miaka 16 amekamatwa kwa tuhuma za mauaji. Inaonekana kana kwamba wiki haipiti bila picha ya kijana aliyeuawa kuangaziwa kwenye kurasa za magazeti nchini Uingereza. Mnamo Juni mwaka huu, mvulana wa miaka 17, Victor Lee, alipatikana amedungwa kisu kwenye mtaro huko London Magharibi. Wavulana watatu wenye umri wa miaka 14, 15 na 17 walifikishwa kortini kushtakiwa kwa mauaji yake. Khaled Saleh, mvulana wa miaka 17 pia alidungwa kisu na kuuawa katikati mwa London mnamo Juni, ikidaiwa na mtoto wa miaka 16. Mnamo Aprili mwaka huu, Renell Charles, mwenye umri wa miaka 16 alidungwa kisu kifua mwake karibu na shule yake. Mtoto mmoja wa miaka 16 alishtakiwa kwa mauaji hayo. Na mwaka jana, mvulana wa miaka 15 alihukumiwa kifungo cha miaka 13 gerezani kwa mauaji ya Ava White mwenye umri wa miaka 12 katika Kituo cha Jiji la Liverpool mnamo Novemba 2021. Wakati huo alikuwa na umri wa miaka14 tu.

Maoni:

Kuna janga la mauaji ya vijana kwa vijana linaloisibu Uingereza. Kuanzia 2016-2018, kulikuwa na ongezeko la asilimia 77 la mauaji yaliyofanywa kwa visu na vijana chini ya umri wa miaka 18, na kutoka 2012-2019, ongezeko la 93% la idadi ya vijana chini ya umri wa miaka 16 walilazwa hospitalini kutokana na mashambulizi ya visu. Serikali, polisi na viongozi hawana taarifa kuhusu jinsi ya kumaliza orodha hii isiyo na mwisho ya misiba. Wengine wametoa wito kwa huduma bora za polisi na nguvu kubwa za kusimamisha na kusaka watu ili kuwatambua wale wanaobeba visu. Wengine wamependekeza hukumu kali kwa wale waliopatikana na hatia ya kubeba visu au uhalifu unaohusiana na kisu, na pia uwekezaji mkubwa katika vilabu vya vijana, shule na miradi ya jamii kujaribu na kuzuia vijana kutokana na kuingia katika uhalifu. Walakini, yote haya yanafeli kutambua na kushughulikia sababu za watoto kujihusisha na maisha haya ya kikatili, kuyachukulia maisha kirahisi rahisi, au kujibu swali - ni nini kimesababisha wengi katika umri mdogo kama huo kuthamini kidogo utakatifu wa Maisha ya binadamu kwamba wako tayari kuyachukua juu ya mambo madogo mno, bila kufikiria mara mbili na bila kuzingatia matokeo yoyote juu ya familia na marafiki wa mwathiriwa, au hata maisha yao wenyewe?

Sababu ya tatizo hili la kutisha ni mchanganyiko wa maswala kadhaa. Kwanza, mtoto anapokuwa hajajengwa na uelewa wa uwajibikaji kwa matendo yake kwa Muumba, au mwongozo wazi wa la sawa na la makosa, au matokeo kesho Akhera kwa matendo yao – basi matendo yao yataendeshwa kwa msingi wa manufaa ya kibinafsi, matamanio yao na matakwa ya hivi sasa – hata ikiwa hiyo itamaanisha kuchukua uhai. Fauka ya hayo, ikiwa hawaamini kuwa kila maisha yana utakatifu kwa sababu ni uumbaji wa Mwenyezi Mungu, ina athari kwa thamani wanayotoa kwa maisha ya mwanadamu. Mfumo wa maisha wa kiliberali wa kisekula umetelekeza dini ndani ya jamii na kukuza imani ya Mungu kama kitu kilichopitwa na wakati na kisicho na maana, na kusababisha vijana wengi kuachana na dini na imani kwa Muumba.

Pili, uliberali umeongeza uchoyo, fikra ya kibinafsi kati ya wengi ya 'mimi, mimi, na mimi', na kusababisha vijana wengi kuzingatia tu maslahi, matakwa na tamaa zao, kutojali athari za matendo yao kwa wengine.

Tatu, watoto wengi wanaohusika katika uhalifu wa visu wamekulia katika mazingira yenye sumu ya vurugu na unyanyasaji – iwe katika mitaa yao au nyumbani kwao. Wengine ni wahasiriwa wa unyanyasaji wenyewe. Kwa kweli, hii huondoa kwa kutojali vurugu, au kuwaongoza katika kufanya vitendo vya dhulma wenyewe. Kuna janga la unyanyasaji wa kinyumbani na uhalifu ndani ya jamii huria, unaosababishwa na watu wanaotenda vitendo kwa matamanio yao, bila kuzingatia matokeo yoyote ya matendo yao kwa wengine.

Nne, thamani ya kiliberali ya uhuru wa kuzungumza imeruhusu vurugu kufurahikiwa na kutukuzwa katika sinema, mitandao ya kijamii na muziki – iwe kwa makundi au vinginevyo – ambayo wengi wamelaumu kwa kuchangia vurugu za vijana.

Tano, uhuru wa kijinsia umesababisha tsunami ya familia zilizovunjika ambapo watoto wengi hukua bila baba nyumbani na mazingira ya kutokuwa na utulivu na kutokuwepo kwa ulinzi na msaada. Fauka ya hayo, katika familia nyingi kuna ukosefu wa muda wa wazazi kukaa na watoto kutokana na kina mama wasio na waume kujitahidi ili kutoa mahitaji kwa familia zao au wazazi wote wawili wanafanya kazi kwa muda mrefu. Matokeo yake, kuna ukosefu wa mazingira ya ulezi na uhusiano wa mzazi na mtoto mara nyingi huwa na shida au haupo. Matokeo ya haya yote ni kwamba watoto wengi huhisi kupuuzwa au kutelekezwa na kujiunga na magenge kwa maana ya kujihisi kuwa na uhusika, udugu au aina fulani ya unganisho la familia, kutafuta heshima, ulinzi, msaada na hadhi. Mauaji ya vijana kwa vijana mara nyingi huwa na uhusiano wa magenge. Kwa kuongezea, ukosefu wa mazingira ya nyumbani ya ulezi na upendo mara nyingi husababisha vijana kuhisi kuwa maisha yao hayana thamani au kusudi, na kwa hivyo kutumia wakati gerezani hakufanyi kazi kama kizuizi kikubwa cha mauaji.

Na mwishowe, ndani ya jamii za kibepari za kiliberali, kukataliwa kijamii, ukosefu mkubwa wa usawa katika ugavi wa mali na ufikiaji duni wa elimu bora umesababisha vijana wengi kupoteza tumaini la maisha yoyote mazuri au kiwango cha maisha ambacho kinaweza kupatikana bila kujihusisha na uhalifu, huku wengine wanahisi kwamba jamii haina uadilifu na kwa hivyo hujihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji ili kufurahiya maisha ya kitajiri, au kusonga mbele tu maishani. Hii ndio hasa hali ndani ya jamii ambazo fikra ya kupenda mali ni kubwa, na hadhi hufafanuliwa na utajiri na mali. Mtaalamu mmoja wa kielimu juu ya uhalifu wa vijana alisema, "Ikiwa watu wanahisi jamii sio adilifu, sio aghlabu kuvutiwa kucheza na kanuni na wana uwezekano mkubwa wa kushinikiza vurugu."

Mwishowe fikra ya uliberali – imani na mfumo wake – ndio ya kulaumiwa kwa kuunda janga hili la mauaji ya vijana kwa vijana na inahitaji kuwekwa kizimbani sambamba na wahusika wa uhalifu huu. Abu Hurairah aliripoti kwamba Mtume (saw) amesema:

«وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَيَأْتِيَنَّ عَلَى النَّاسِ زَمَانٌ لاَ يَدْرِي الْقَاتِلُ فِي أَىِّ شَىْءٍ قَتَلَ وَلاَ يَدْرِي الْمَقْتُولُ عَلَى أَىِّ شَىْءٍ قُتِلَ»

Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, wakati utafika ambapo muuaji hatajua ni kwanini amefanya mauaji hayo, na mwathiriwa hatajua ni kwa nini ameuawa. Inahisika kana kwamba tunaishi katika nyakati kama hizo, katika jamii ambazo matamanio ya mwanadamu yamekuwa ndicho kipimo cha la sawa na makosa badala ya hukmu na sheria za Yule aliyemuumba wanadamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu