Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vita vya Fitna Vinaweza Tu Kwisha kwa Kuunganisha Pakistan na Afghanistan kama Dola Moja ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Habari:

Pakistan ilipoteza wanajeshi ishirini na watano katika Dera Ismail Khan wa Khyber Pakhtunkhwa, mrengo wa masuala ya vyombo vya habari wa jeshi (ISPR), ulisema mnamo tarehe 12 Disemba 2023. Tehreek-i-Jihad Pakistan (TJP), kundi jipya linaloshirikiana na Tehreek-i-Taliban Pakistan (TTP), ilidai kuhusika na shambulizi kwenye kituo cha ukaguzi.

 Maoni:

Pakistan imekuwa ikishuhudia ongezeko la mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama katika majimbo ya Khyber Pakhtunkhwa (KPK) na Baluchistan.  Wakati Taliban wa Afghanistan walipochukua udhibiti wa Kabul mnamo Agosti 2021, kulikuwa na matumaini kwamba masuala ya usalama ndani ya Pakistan yatapungua kwa kiasi kikubwa, ikiwa hayatatokomezwa kabisa.  Kundi la Taliban la Afghanistan lilijaribu kuwezesha mazungumzo kati ya dola ya Pakistan na Tehreek-i-Taliban Pakistan (TTP), ambayo yalitoa makubaliano mawili ya kusitisha mapigano kati yao. Walakini, usitishaji huo wa mapigano haukudumu zaidi ya miezi michache.

Vita hivi vya Fitna baina ya Waislamu vinaifaa Marekani. Kutokana na hili, Pakistan inasalia na shughuli nyingi katika kuzima wanamgambo katika mikoa yake ya Magharibi, kwenye mpaka wa Pakistan na Afghanistan.  Uhusiano kati ya Pakistan na Afghanistan bado ni wa wasiwasi, kwani Pakistan inashutumu Taliban ya Afghanistan kwa kuunga mkono TTP.  Hali hii inatoa nafasi kwa India kuelekeza umakini wake kwenye mipaka yake inayozozaniwa na China.  Haya yote husaidia sera ya Marekani ya kuwa na China.  Kwa hivyo, ni kwa maslahi ya Marekani kwamba mgogoro huu ndani ya Pakistan, na mvutano na Taliban wa Afghanistan, kuendelea.

Pia kuna sababu ya kindani inayochochea vita hivi vya Fitna. Makundi haya ya wapiganaji yanaichukulia dola ya Pakistan kama mshirika wa Marekani. Hakika, uongozi wa Pakistan uliweka kila rasilimali inayopatikana kwa Marekani, wakati wa karibu miaka ishirini ya kile kinachojulikana kama "vita dhidi ya ugaidi."  Hata baada ya Marekani kujiondoa kutoka Afghanistan, nchi ya Pakistan haijaacha utumwa kwa Marekani. Hii inaakisi katika sera yake juu ya Kashmir inayokaliwa kimabavu. Watawala wa Pakistan wamezihakikishia Marekani na India, kwamba hata baada ya India kuvuka mstari mwekundu wa mwisho, ambao ni unyakuzi wa Kashmir inayokaliwa kimabavu, wataendelea kuwazuia wanajeshi wa Pakistan.

Utawala wa Pakistan lazima ubadilishwe ili kukomesha vita hivi vya Fitna. Utasababisha tu madhara zaidi kwa Pakistan.  Operesheni zaidi za kijeshi hazitamaliza vita hivi katika maeneo ya kikabila. Marekani ilitambua hilo baada ya miaka mingi ya vita.  Uongozi wa Kiislamu, unaotawala kwa Uislamu, peke yake ndio unaoweza kumaliza hasara kwa pande zote mbili.

Waislamu wa Pakistan na Afghanistan wanapenda Uislamu na wanaichukia Marekani. Wanataka kuishi chini ya serikali ambayo inatabikisha Uislamu katika kila nyanja ya maisha. Wanataka kulizunguka eneo hili kwa biashara, elimu, afya, na kadhalika, bila vikwazo vyovyote. Wako tayari kuunganishwa chini ya dola moja ya Khilafah.

Khilafah itakata uhusiano wote na Marekani. Itasimamisha sheria za Uislamu katika kila nyanja ya maisha. Kwa hivyo, hakutakuwa na mgongano kati ya hisia na matarajio ya watu, na sera za watawala. Hili pekee ndilo litakalomaliza vita vya fitna ambavyo vinawadhoofisha Waislamu mbele ya maadui wao wa kweli, Marekani, India na umbile la Kiyahudi.  Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَاَطِيۡعُوا اللّٰهَ وَرَسُوۡلَهٗ وَلَا تَنَازَعُوۡا فَتَفۡشَلُوۡا وَتَذۡهَبَ رِيۡحُكُمۡ وَاصۡبِرُوۡا اِنَّ اللّٰهَ مَعَ الصّٰبِرِيۡنَ]

“Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri.”  [Al-Anfal 8:46]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

 Mhandisi Shahzad Sheikh – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu